Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,535
- 8,620
Majuzi tumeazimisha miaka kumi bila mwalimu..yalikuwa ni maazimisho makubwa kwa kila hali,kikubwa si sherehe zinazoambatana na protokali bali kikubwa na hisia zilizojaa mioyoni mwa wananchi walio wengi juu ya Baba wa TAIFA.
Taasisi ya mwalimu nyerere ..iliasisiwa na mwalimu ikiiwa pamoja na mambo mengine ni kuendeleza yale aliyokuwa akiyaamini ...mwenyekiti wa kwanza wa taasisi ni mwalimu nyerere mwenyewe,kabla ya kumuachia Dr salim..,wajumbe wa bodi wapo wafuasi wa mwalimu kama kina butiku,warioba,mongela na wengine...Pamoja na kukabiliwa na ukata taasisi hii inayo heshima afrika labda nyuma ya taasisi nyingine kama MANDELA FOUNDATIONS na MO IBRAHIM foundation..,angalau inalo la kujivunia ,imekamilisha amani ya burundi kupitia upatanishi wake.
Taasisi kama ya mandela moja ya vyanzo vikuu vya mapato ni michango ya wahisani na kuungwa mkono na serikali husika.mfano sherehe za kuzaliwa mandela ni kati ya chanzo kikuu cha mapato....nadhani hata hapa Nyerere day ingetosha kuwa siku ya kuichangia taasisis kwa hali na mali....lakini nahisi imekuwa wahanga wa siasa za visasi.
Wenye macho na akili[hata za kawaida] wameona juzi ..namna kwenye maandalizi ya miaka kumi ya mwalimu ..taasisi ya mwalimu ilivyotengwa na serikali.Wakati taasisi ilijikakamua kuandaa hafla dar na mihadhara kumkumbuka mwalimu,ambapo katika cakula cha jioni ...serikali ilimtuma waziri mkuu,....hali ilikuwa tofauti butiama kwani viongozi wa taasisi ya mwalimu nyerere hawakualikwa au awakupewa umuhimu kwenye shughuli ile ya kitaifa,ile ilikuwa kasoro kubwa kwa waandaaji!
Wakati wa uwekaji wa mashada ..pale butiama mwenyekiti wa taasisi dr salim na katibu wake butiku hawakuwepo pale kwenye mwalimu maoseleum...,hata warioba na mongela waliokuwa pale waliweka mashada kuwakilisha waliofanya kazi na mwalimu....,Je hatuna sababu ya kuamini kuwa hali ile ilipangwa ?? je kikwete hawapendi viongozi wa mwalimu nyerere foundation...?...haiwezekani taasisi iliyo na jukumu la kuweka hai mawazo na imani a mwalimu isiwepo au isialikwe na watu tushindwe kuona hilo kwa jicho la tatu!!
Hata pale uwanjani ...hakuoneka kiongozi wa mwalimu foundation yeyote kutambulishwa...,na hataa safari hii tena warioba alisahauliwa hadi baadaye ndio akatambuliswa safari hii kama waziri mkuu mstaafu..wakati wanatambulishwa mwakilishi wa watoto wa mwalimu na wajukuu.
sitaki kuamini kama visasi vya uchaguzi wa mwaka 2005..ndio mwendelezo wa haya......