JK ana BIFU na Mwalimu Nyerere Foundation?

Companero:

Hivi huwezi kujibu hoja bila kutaja handler yangu?
icon8.gif
Hivi ndivyo watanzania mlivyofiliska kimawazo. Na mfano mkubwa ni JF. Thread nyingi ikiwemo hii zipo personal na sio kwenye issue.

Hivi mnashindwa nini kukata issues?

Mkuu, tehe tehe, acha kuendeleza trademark ya kuuongopea umma - rudi kwenye issue (i.e. MNF), stop taking it personally, kata issue hiyo!
 
Suala la MNF lawama hapaswi kutupiwa JK. Utete wa MNF unatokana na siasa za ndani za humo. Na tukitaka kuzijua tuangalie historia ya kilichowaondoa watu muhimu katika taasisi hiyo hasa baada ya Mwalimu JK kufariki. Pia turejee makala hii ya wazi iliyoandikwa gazetini mwaka 2008:

Salvage foundation to uphold Nyerere legacy

By Alfred Ngotezi

To most of us, the establishment of the Mwalimu Nyerere Foundation (MNF) in 1996, represented a deliberate effort to pass on the ideals of founding President Mwalimu Julius Nyerere.

The project stood as tall as its initiator, whose integrity, honesty, foresight and intelligence remain awe-inspiring today, about 10 years since he died.

However, it has had its share of ups and downs.

Its executive secretary, Joseph Butiku, recently said it is currently in the financial doldrums.

He said:

''The foundation is facing hard times and relies on external donations for day-to-day operations. Because of this handicap, we have failed to start construction of our new 10-storey building.''

The stalled $10.3 million (Tsh12.3b) building was meant to be a self-financing project for the foundation, with a memorial library for one of Africa's most revered politicians.

The building would also have a spacious commercial hall, a business car park, and rental offices. But, so far, all this remains a pipe dream.

Explaining the scenario, Butiku said the story goes back to 2003, when the foundation sought to raise Sh800 million through donations from corporate organisations and individuals, but only realised half of that.

''To raise the remaining sum, we decided to extend the request to every Tanzanian, an idea which got us into trouble,'' he said.

He explained that the Prime Minister of the time, Frederick Sumaye, was not amused by the idea and instantly blocked it.

Sumaye, who ran for the top job and lost at the CCM nomination stage in 2005, reportedly bunged the MNF initiative allegedly to thwart former African Union secretary general Salim Ahmed Salim's presidential bid.

Whether this is true or not, only time will tell. But Butiku insists it is an opportunity that went begging.

''If we had gone ahead with the plan, we would have raised Sh20 billion, apart from promised assistance from the US, not to mention the project's $200,000 (Tsh240m) expected annual income,'' he is quoted as saying.

Unless proved otherwise, these are shocking revelations. However, journalism is a game of balancing.

One-sided allegations are not necessarily true until they are weighed in the light of the response of the accused.

In view of this, it would be fair to look at the other side of the coin. Butiku's critics accuse him of mismanagement of the Foundation, citing alleged withdrawal of funds for unplanned purposes.

The Foundation chairman, Dr Salim, it is alleged, has on several occasions had to pay the workers' salaries from his own pocket.

An impeccable source, who sought anonymity, claimed that Butiku has personalised the institution and runs it with an iron-fist.

Others accuse him of turning the organisation into an opinionated platform, drawing incessant criticism from the establishment. Butiku has all along denied these charges.

As the two sides trade more and more accusations, those of us on the periphery may never know the exact nature of this rigmarole.

Perhaps yet another investigating committee could help us here. But even before we come to the river to cross the bridge, as it were, the fact of the matter is that without smooth financing, the MNF will die sooner than later.

I personally do not see why we should kill such an enviable foundation.

For, letting it die would amount to doing a disservice to all the people who hold Mwalimu Nyerere and what he stood for in high esteem, and it's millions in Africa and throughout the world.

For our leaders, such action could be construed as putting the last nail in the coffin of Mwalimu's good governance and rule of law beliefs and practices.

I, therefore, urge the leadership of the MNF, especially its board, to put their heads together, with a view to coming up with a viable survival plan.

Rather than rely on a few donors like Dr Salim to sustain the fund, they should devise ways of reaching out to more people both locally and internationally.

Clearly, any feasible plan to turn the MNF into a self-financing project would attract donations from all over the world.

I would be surprised if Nyerere admirers like former South African President Nelson Mandela, Ugandan President Yoweri Museveni, and Rwandan President Paul Kagame, to name but a few, would not wish to chip in.

That is apart from many Tanzanians, who still believe that Mwalimu deserves their support in life and death because he never stole their money.

Yet as earlier seen, the MNF's woes may be right in the ship not in the sea. Therefore, the best way forward is to identify its prevailing weaknesses, with a view to charting a prosperous future for the institution.

This suggestion may sound vitriolic to some of the interested parties, but unfortunately, that is the way forward, given that Mwalimu belonged, nay, belongs to us all.

The most important issue is to ensure that Nyerere's impressive human qualities do not die with him.

One of the ways to sustain his virtues is to support his Foundation.

The ball lies squarely in the court of the institution's board of directors.

Source: http://www.thecitizen.co.tz/newe.php?id=4879
 
Mkulu PM, heshima mbele sana:-

- Maneno yako mengi ni msumari isipokuwa tu conclusion yako iko hewani, Nyerere Foundation baada ya kifo cha Mwalimu, walijiingiza kwenye mambo mengi sana ambayo yalikuwa ni kinyume na matakwa ya watawala na sometimes wameenda mbali hata kuhusika na uvunjaji wa sheria as opposed na mwenendo wa taaisisi hiyo chini ya Mwalimu.

- Kuna maovu mengi kule hayasemwi hadharani ambayo Butiku, aliyafanya akidhani kwamba he is untouchable na kuwaudhi sana wapambe wa Mkapa mengi ni aibu hata kuyasema hapa, ndipo kwa mara ya kwanza Mkapa akazuia mgawo wa Shillingi Millioni 300 ambazo serikali ilikuwa ikiipatia Foundation ile annually, na ilikuwa hasa baada ya Butiku kupeleka sherehe za Mwalimu kwenye bunge la Uganda bila kuiarifu serikali ya Mkapa, kitu ambacho kilitafsiriwa kama ni sometype of a blackmail's set up kwa Mkapa na Butiku alijipiga kisu cha mwisho pale alipoanzisha ziara za kutembelea mikoa kusikiliza shida za wananchi, lakini infact akiwa kwenye kampeni za Salim na urais.

- Mkapa kwa makusudi akamtuma Warioba kule Foundation kuangalia mahesabu, ilikuwa aibu sana jinsi hela za wananchi zilivyoliwa hovyo bila uwajibikaji, yakazuka magomvi mazito sana mpaka Warioba akaombwa aondoke haraka sana, wakulaumiwa sio serikali ila ni Butiku na kundi lake kule Foundation kwa ubadhirifu mkubwa sana, infact waliwtakiwa wawe Segerea ila kwa vile ni bongo wapo nje na wanailaumu sana serikali on ufisadi ule ule kama wao kule Foundation na cha ajabu wanapata na wananchi wa kuwa-support, only in Tanzania!

Respect.

Field Marshall Es!

FMES,
Nakuheshimu kwa michango yako lakini unaongeza chumvi mno na wakati mwingine unachoandika si ukweli wenyewe ama hali halisi.

Butiku hajawahi hata mara moja kumfanyika kampeni SALIM. You should learn more about the MNF inside 'politics' kuweza kuliona hilo. Salim ni mtu mwadilifu ambaye anapenda kufanya mambo yake systematically bila kuvunja sheria ama kupindisha pindisha. Alikuwa na timu yake ya campaign iliyokuwa na mabalozi 4, Mkufunzi wa Chuo Kikuu mmoja na mama mmoja ambaye alijitumbukiza humo kwa maslahi binafsi na hivi sasa ni Mbunge. Salim asingeliweza kumtumia Butiku kwenya campaign zake na nina uhakika kwamba hakuwahi kuketi kupanga ama kuzungumza lolote kuhusu Butiku kumfanyia campaign.

Pia tatizo la Butiku katika uendeshaji Taasisi zaidi liko katika ubinafsi, uwezo mdogo wa uongozi na matumizi ya fedha bila kufuata utaratibu uliowekwa. Huwezi ukamwita Butiku mwizi bali mbadhilifu. Nasikia akiona fedha anaitumia bila kufuata budget.

Mkapa na Butiku walikuwa marafiki wa kupika na kupakua (family friends) haieleweki kilitokea nini mpaka wakafikia hatua ya kuwa maadui. Nadhani FMES unaweza kutuhabarisha zaidi kuhusu hilo maana you are always well informed ukiacha chumvi unazokoleza mno wakati mwingine.
 
..binafsi napendekeza ianzishwe Julius Nyerere Presidential Library.

..halafu majukumu ya MNF yawe-scalled down na kubakia na shughuli ya kuendesha na kuratibu maktaba hiyo.

..wakina Warioba,Butiku,... wana shughuli zao binafsi za kujikimu kiasi kwamba ni vigumu kuwa na muda na nguvu za kutosha kushughulikia masuala ya MNF.

NB:

..napendekeza maktaba hiyo ijengwe ndani ya Chuo Kikuu cha DSM ambacho kilianzishwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

I beg to differ,

Mwalimu alikubali kuanzisha Taasisi yenye kubeba jina lake akiamini kwamba ndio sehemu pekee itakayoweza kusimamia na kuendeleza yale aliyoyaamini na kuyaanzishwa. Naam Maktaba ya Mwalimu ni muhimu lakini kuyaendeleza yale mema na ambayo bado relevant na yataendelea kuwa hivyo - aliyokuwa anayoaamini, anayasimamia na kuyapigia kelele kwa manufaa ya Taifa, Afrika na Dunia ya Tatu kwa ujumla; nadhani uwepo wa Taasisi ni muhimu zaidi ili kuweza kuyashughulikia hayo.

Kulegalega kwa Taasisi kunatokana na uongozi hafifu. Pamoja na kuwa na Bodi yenye kusheheni waliokuwa karibu sana na Mwalimu, Taasisi imeshindwa kufanya yale Mwalimu aliyotarajia. Naambiwa kosa lililofanyika ni kumfanya Executive Director wa Taasisi kuwa pia ni Board Member. Kwa maana hiyo basi inakuwa vigumu sana kwa Bodi kumchukulia hatua ama kumdhibiti ED ambaye pia ni mwenzao kwenye Bodi! Endapo itakuwepo haja ya kumkosoa ED na utendaji wake unadhani nini kinaweza kutokea? Tukumbuke pia kwamba hao wote ni 'wamoja' lazima wataoneana aibu na kwa bahati mbaya hilo la kuoneana soni linaimaliza Taasisi.
 
Hivi kile KIGODA cha Mwalimu kinachokaliwa na akina Prof. Shivji hakiwezi kuunganisha nguvu, maarifa na uongozi na MNF tukapata kitu kizuri tu kinachoendanaendana na heshima na hadhi ya Mwalimu?
MNF inashindwa hata na EOTF na WAMA ambazo hata uwepo wake tu haustahili. Hatumtendei haki Mwalimu kwa kuyaangalia madhambi na mapungufu ya akina Butiku.
 
Ameanziwa sana mpaka na wasiwasi si muda mrefu wajinga watamfanya mungu (mungu aepushe)
1. Uwanja wa ndege unaitwa kwa jina lake
2. Maonyesho ya sabasaba kwa jina lake
3. Shule, barabara, etc
need more...mbio za mwenge kila mwaka...duuu
need more..foundation ipewe ..priority na serikali duu...
need more...mchakato wa wa kuwa st. uko ukingoni..duu..
By the way what good he did for a country:
a) Blah blah za umoja, kama vile alikuwa mwenyewe Akh!
Failure is always hero for our people poleni sana...nashukuru kama JK ataachana na hili Libabu nuksi...
Lakini old bagamoyo road ina jina la baba mdogo wa taifa kwa hiyo siyo kila kitu kina jina la mwalimu
 
hakuna sababu yeyote ya msingi kwanini mwalimu nyerere foundation iwe na ukata; nahisi kuna tatizo katika utendaji wa taasisi hii kwani inaendeshwa kama vile ya kifamiliana ndio maana haishamiri kama vile watu wengi walivyotegemea. Mandela foundation inaendeshwa na professionals walioajiriwa kwa uwezo wao na wale waliofanya kazi na mzee madiba wao sio watendaji bali wako kwenye board ya foundation; hivyo basi kila kitu kinatekelezwa kiutaalam unlike the mwalimu foundation where butiku by virtue of being a relative wa mwalimu amejiweka kuwa mtendaji mkuu. Pia swala la fedha kutotumika vyema wakati foundation inasimamia mgogoro wa burundi ilileta credibility problem kwa foundation!
hilo ndilo tatizoo kubwaa la nyerere foundation...

Kwa bahati mbaya mkapa hatakubali kuwa mkiti ili kuiokoaaaaaaa taasisi hiii.
 
I beg to differ,

Mwalimu alikubali kuanzisha Taasisi yenye kubeba jina lake akiamini kwamba ndio sehemu pekee itakayoweza kusimamia na kuendeleza yale aliyoyaamini na kuyaanzishwa. Naam Maktaba ya Mwalimu ni muhimu lakini kuyaendeleza yale mema na ambayo bado relevant na yataendelea kuwa hivyo - aliyokuwa anayoaamini, anayasimamia na kuyapigia kelele kwa manufaa ya Taifa, Afrika na Dunia ya Tatu kwa ujumla; nadhani uwepo wa Taasisi ni muhimu zaidi ili kuweza kuyashughulikia hayo.

Kulegalega kwa Taasisi kunatokana na uongozi hafifu. Pamoja na kuwa na Bodi yenye kusheheni waliokuwa karibu sana na Mwalimu, Taasisi imeshindwa kufanya yale Mwalimu aliyotarajia. Naambiwa kosa lililofanyika ni kumfanya Executive Director wa Taasisi kuwa pia ni Board Member. Kwa maana hiyo basi inakuwa vigumu sana kwa Bodi kumchukulia hatua ama kumdhibiti ED ambaye pia ni mwenzao kwenye Bodi! Endapo itakuwepo haja ya kumkosoa ED na utendaji wake unadhani nini kinaweza kutokea? Tukumbuke pia kwamba hao wote ni 'wamoja' lazima wataoneana aibu na kwa bahati mbaya hilo la kuoneana soni linaimaliza Taasisi.

Wakuu heshima mbele. Hapa nina swali. Mara nyingi taasisi zinapoanzishwa huwa na katiba au aina yoyote ya mwongozo katika uendeshaji. Sasa kwa MNF nafasi kama za Executive Director na nyinginezo ni za kudumu? Ninamaanisha kiutendaji hawana kipindi maalum cha kuwa madarakani halafu wengine kuchaguliwa au kuteuliwa?
 
Muanzisha mada angetuambia kwanza huo ufisadi wa akina Butiku (kama si ES wengine wasingeujua) then ndio akatoa lawama zake kwa watawala. Hivi kumtoa fisadi kwenye utendaji na kumpeleka kwenye Bodi ya Wadhamini ndio kumuenzi kwenyewe Nyerere?!
 
Sasa mnamuebnzi vipi Mwalimu Nyerere kama mambo yote aloanzisha ikiwemo hiyo Taasisi yake hamvienzi?? Natamani kuona mawazo ya Nyerere yakienziwa kupitia Nyerere Foundation na siyo vinginevyo.
 
FMES,
Nakuheshimu kwa michango yako lakini unaongeza chumvi mno na wakati mwingine unachoandika si ukweli wenyewe ama hali halisi.

Butiku hajawahi hata mara moja kumfanyika kampeni SALIM. You should learn more about the MNF inside 'politics' kuweza kuliona hilo. Salim ni mtu mwadilifu ambaye anapenda kufanya mambo yake systematically bila kuvunja sheria ama kupindisha pindisha. Alikuwa na timu yake ya campaign iliyokuwa na mabalozi 4, Mkufunzi wa Chuo Kikuu mmoja na mama mmoja ambaye alijitumbukiza humo kwa maslahi binafsi na hivi sasa ni Mbunge. Salim asingeliweza kumtumia Butiku kwenya campaign zake na nina uhakika kwamba hakuwahi kuketi kupanga ama kuzungumza lolote kuhusu Butiku kumfanyia campaign.

Pia tatizo la Butiku katika uendeshaji Taasisi zaidi liko katika ubinafsi, uwezo mdogo wa uongozi na matumizi ya fedha bila kufuata utaratibu uliowekwa. Huwezi ukamwita Butiku mwizi bali mbadhilifu. Nasikia akiona fedha anaitumia bila kufuata budget.

Mkapa na Butiku walikuwa marafiki wa kupika na kupakua (family friends) haieleweki kilitokea nini mpaka wakafikia hatua ya kuwa maadui. Nadhani FMES unaweza kutuhabarisha zaidi kuhusu hilo maana you are always well informed ukiacha chumvi unazokoleza mno wakati mwingine.
Boramaisha,
Asante kwa nyongeza yako. Butiku asingeweza kumwarifu Mkapa juu ya sherehe za Mwalimu Uganda kwa sababu Mkapa alikuwa amekata simu yake. Mkapa tangu alipoingia madarakani alimtenga Butiku kama mtu mwenye ukoma kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe na Ferdinand Ruhinda. Na zile sherehe za Uganda zilifanywa na serikali ya Uganda kwa hiyo kwamba Mkapa hakuarifiwa lawama ni kwa serikali ya Uganda na wala si Butiku.
 
Jasusi na wakuu wengine,
Wakuu zangu, kama mjuavyo mimi ni mshabiki mkubwa wa mwalimu. Lakini kusema kweli sidhani kama walifikiria vizuri kupanga malengo ya foundation hii kulingana na uwezo wa viongozi wake kwa sababu baada ya mwalimu hakuna mtu Tanzania ambaye anaweza kusikika hata hapa Afrika.

Kama Foundation hii ingekuwa chini ya AU labda hapo ingekuwa na nguvu kiasi fulani yaani baada ya Nyerere kufariki angeshika Mandela au kiongozi anayeheshimika zaidi Afrika au Duniani iwe hata mshindi wa Peace Noble..
Nikiwa na maana baada ya Nyerere kiongozi mwingine ambaye anaheshimika kwa kiwango cha juu zaidi ndiye angechaguliwa kuongoza chombo hiki,other tha that, mkuu wangu Foundation hii ni Upotezaji wa muda na fedha tu kiutendaji kwa sababu Uongozi wake haukuchukua mtazamo mpana na nje ya Tanzania. Kifupi Malengo ya Nyerere foundation ni makubwa kuliko uwezo wa viongozi wake.
Leo hii, Tanzania hatuna ubavu tena wa kuhubiri, ku promote Peace, Unity and Human centred Development. Ni makosa ambayo mwalimu huyarudia kila mara yaani siku zote mwalimu alikuwa mchovu kwa kuchagua mrithi wake.. Nyerere foundation ni jina kubwa lenye malengo makubwa lakini ukitazama viongozi wake haufanani kabisa na foundation hiyo..
 
mkandara,

Naamini viongozi wengine wa kariba ya nyerere, ama wanaokaribiana nae wapo humu humu mwetu. Kama, tatizo ni kwenye uongozi wa taasisi libadilishwe hilo, lakini kudhani kwamba taasisi haiendi kwa kuwa hakuna mtu maarufu wa kuisimamia ni kiza cha fikra.
 
Taasisi ya Mwalimu Nyerere, hata kama haipewi ushirikiano wa kutosha toka serikalini, hawana sababu ya kukwazika. Taasisi yenyewe, kwa kuamini katika kazi za nyerere ni mtaji tosha. Japo, fikira za kijamaa zina mipaka yake, lakini swala la kujitegemee bado ni la msingi sana na wananchi wanaweza kuchangia kwenye hilo. Taasisi ichague tafiti za kufanya, isomeshe watu kwa jina la mwalimu, na itengeneze programu za kijamii kusukuma fikira za kizalendo. Na inawezekana kabisa, taasisi ikanzisha michango midogo ya wananchi, ama wapate mashamba, ama wawe na waumini wa itikadi ama mwalimu kuichangia - swala hapa ni taasisi kutoa mwongozo wa nini inataka kufanya sasa.
 
mkandara,

Naamini viongozi wengine wa kariba ya nyerere, ama wanaokaribiana nae wapo humu humu mwetu. Kama, tatizo ni kwenye uongozi wa taasisi libadilishwe hilo, lakini kudhani kwamba taasisi haiendi kwa kuwa hakuna mtu maarufu wa kuisimamia ni kiza cha fikra.
Mkuu mimi sikubaliani na mtazamo wako... ni mawazo yangu na nakuomba yatazame kwa mapana hayo.

Nyerere Foundation inatakiwa mtu ambaye anaweza kuishawishi dunia. Tumeona Foundation kubwa kama ya Mama Mama Theresa, Bush, Clinton, Gore na wengineo zikifahamika dunia nzima kwa sababu kiongozi wake ni mmoja ya watu wanaoheshimika. Baada ya Salim kuondoka AU (OAU), Nyerere Foundationa haikuwa na nguvu tena na sidhani kama inafamika nje ya mipaka yetu acha mbali humu nchini kwetu.

Jukumu la kutangaza na kuhubiri UMOJA, AMINI na Maendeleo ya Binadamu inachukua nguvu kubwa zaidi mchango uliopo wa Foundation hiyo. Mathlan hawakuwa na kambi sehemu zilizoathirika na mambo hayo iwe Sudan, Kongo, Rwanda, Sri lanka, Palestina, Burma, Nigeria, Sierra Lionne, na hata Tarime ambako majuzi tu kumetokea rabsha za ndani, hivi kweli wanachokifanya ni kipi...

Ebu wewe nambie one accomplishment ambayo foundation hiyo imeweza fanya mbali na ile ya Rwanda na Burundi wakati mwalimu akiwa hai!..Tenaa basi vita yao kubwa ilianza tu baada ya kifo cha mwalimu..Unawez nambia kilitokea nini!

Je, ni nani kweli anaweza kuwa balozi mzuri wa Foundation hii nje baada ya mwalimu pamoja na kwamba unasema viongozi wazuri wapo ndani nchini. Kina nani? hao marais wetu wenyewe kina Mkapa, Mwinyi na Kikwete wote record yao wenyewe mbaya hasa huko Zanzibar..
 
Swala hapa ni kukubaliana ni mtu mwenye kariba gani kuendesha Taasisi ya Mwalimu! Je ni cheo cha thamani ambacho kitawafanya watu wakikimbilie kama sehemu ya mapumziko yao baada ya kupata uzoefu wa kutosha? Tuamue kama kiongozi huyo uwezo wake uwe kuimarisha taasisi kifedha ama kiitikadi! Je kwa itikadi ya taasisi viwili hivyo vinabebana. Uongozi wa taasisi unachukua dhana ya kijumuiya ya afrika ama ni dhana na utanzania? Mchango wa taasisi utambulike kwa nani? Ni sisi wenyewe kujifurahisha kwamba tumuenzi mwalimu, ama kuendeleza imani yake juu ya afrika moja, na haki sawa za binadamu nje ya mipaka yetu! kwangu mimi hayo nayaona ni maswala ya msingi, na yataifikisha taasisi mbali kama yataangaliwa si kwa upana tu, bali na kuwa makini kwenye malengo na itikadi ya taasisi nje ya mwalimu kama binadamu
 
Mkuu, tehe tehe, acha kuendeleza trademark ya kuuongopea umma - rudi kwenye issue (i.e. MNF), stop taking it personally, kata issue hiyo!

Companero:

Tehe tehe, kama kawaida yangu issue nisiyoijua sitihi mguu. Nasoma kile wengine wanachoandika. Lakini huchoki kuibua handler yangu hata kwenye mada nisizojitikita.

Anyway, mtoa mada aliunganisha doti kuwa JK ana bifu na MNF. Kila nikisoma habari za wenye kujua kinachotokea jikoni sioni uhusiano wowote hule.

Kwa maoni yangu binafsi, JK anaweza kuwa anapoboronga. Lakini tujaribu kuunganisha kuboronga kwake na issue zinazomuhusu. Kushindwa kufanya hivyo ni kuleta udaku.
 
Boramaisha,
Asante kwa nyongeza yako. Butiku asingeweza kumwarifu Mkapa juu ya sherehe za Mwalimu Uganda kwa sababu Mkapa alikuwa amekata simu yake. Mkapa tangu alipoingia madarakani alimtenga Butiku kama mtu mwenye ukoma kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe na Ferdinand Ruhinda. Na zile sherehe za Uganda zilifanywa na serikali ya Uganda kwa hiyo kwamba Mkapa hakuarifiwa lawama ni kwa serikali ya Uganda na wala si Butiku.

Jasusi:

Kuna posti nilisoma hapa ambazo zinaonyesha kuwa wakina Butiku walimfagilia sana Mkapa kwa Mwalimu hili awe mgombea wa Urais?
 
Jasusi na wakuu wengine,
Wakuu zangu, kama mjuavyo mimi ni mshabiki mkubwa wa mwalimu. Lakini kusema kweli sidhani kama walifikiria vizuri kupanga malengo ya foundation hii kulingana na uwezo wa viongozi wake kwa sababu baada ya mwalimu hakuna mtu Tanzania ambaye anaweza kusikika hata hapa Afrika.

Kama Foundation hii ingekuwa chini ya AU labda hapo ingekuwa na nguvu kiasi fulani yaani baada ya Nyerere kufariki angeshika Mandela au kiongozi anayeheshimika zaidi Afrika au Duniani iwe hata mshindi wa Peace Noble..
Nikiwa na maana baada ya Nyerere kiongozi mwingine ambaye anaheshimika kwa kiwango cha juu zaidi ndiye angechaguliwa kuongoza chombo hiki,other tha that, mkuu wangu Foundation hii ni Upotezaji wa muda na fedha tu kiutendaji kwa sababu Uongozi wake haukuchukua mtazamo mpana na nje ya Tanzania. Kifupi Malengo ya Nyerere foundation ni makubwa kuliko uwezo wa viongozi wake.
Leo hii, Tanzania hatuna ubavu tena wa kuhubiri, ku promote Peace, Unity and Human centred Development. Ni makosa ambayo mwalimu huyarudia kila mara yaani siku zote mwalimu alikuwa mchovu kwa kuchagua mrithi wake.. Nyerere foundation ni jina kubwa lenye malengo makubwa lakini ukitazama viongozi wake haufanani kabisa na foundation hiyo..

Mkandara:

Mambo ya foundations tunaiga. Hivyo hazijaota mizizi kwetu ya jinsi ya kuziendeleza. Hivyo mambo mengine yanakuja kwenye mapungufu ya experience za kuendesha taasisi zenyewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom