JK ana BIFU na Mwalimu Nyerere Foundation?

Boramaisha,
Asante kwa nyongeza yako. Butiku asingeweza kumwarifu Mkapa juu ya sherehe za Mwalimu Uganda kwa sababu Mkapa alikuwa amekata simu yake. Mkapa tangu alipoingia madarakani alimtenga Butiku kama mtu mwenye ukoma kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe na Ferdinand Ruhinda. Na zile sherehe za Uganda zilifanywa na serikali ya Uganda kwa hiyo kwamba Mkapa hakuarifiwa lawama ni kwa serikali ya Uganda na wala si Butiku.

Jasusi,
Nakubaliana nawe. Pamoja na kwamba sina information za kina kuhusu sherehe za Mwalimu Uganda lakini nakubaliana nawe kwamba Mkapa ilifika mahali hata waliomsaidia kufika Ikulu alianza kufarakana nao na watu wanasema ni kutokana na ushauri mbovu aliokuwa anapewa na huyo Ruhinda.
 
Zakumi said:
Mambo ya foundations tunaiga. Hivyo hazijaota mizizi kwetu ya jinsi ya kuziendeleza. Hivyo mambo mengine yanakuja kwenye mapungufu ya experience za kuendesha taasisi zenyewe.

Zakumi,

..kuna ukweli ktk hayo uliyoyasema.

..hii foundation irekebishe majukumu yake kwa kuangalia hali halisi.

..sidhani kama hii taasisi inaweza kushughulikia jukumu la kutafuta amani ktk eneo la maziwa makuu.

..hivi kweli hawa watendaji waliobaki wa MNF wanaweza kumuweka kitako mhuni kama Generali Nkunda na akawasikiliza?

..Mwalimu Nyerere hayupo tena kwa hiyo ni vizuri Taasisi nayo ikajipanga upya kuzingatia ukweli huo. ndiyo maana wengine tukapendekeza ianzishwe Presidential library ya Mwalimu Nyerere.
 
jokaKuu,
Mpango wa presidential library nimewahi kuusikia. Bado haijaamuliwa kama iwe ndani ya Foundation, au iwe kwenye Nyerere&Karume memorial ambayo serikali inapanga kujenga au iwe Butiama. BTW ilinistua kidogo kusikia kuwa serikali inatafuta "An American designer" kutayarisha hiyo memorial. Why an American, I asked myself.
 
...na kwa kuwa jk ni mtu wa visasi ..hawezi kumsamehe nyerere kwa hilo...bado anaamini kuwa mwaka 1995...alimshinda mkapa na ni nyerere ndiye aliyemkata ....

Nimekukubali mkuu, sasa wajipanga vipi kumshawishi kuondoa visasi, au wapendelea aendelee hivyo. Inaelezwa na Vitabu Vitakatifu kuwa ukikaa kimya huku jirani yako anaharibikiwa nawe unajumuishwa kwenye dhambi siku ya hukumu
 
Zakumi,

..kuna ukweli ktk hayo uliyoyasema.

..hii foundation irekebishe majukumu yake kwa kuangalia hali halisi.

..sidhani kama hii taasisi inaweza kushughulikia jukumu la kutafuta amani ktk eneo la maziwa makuu.

..hivi kweli hawa watendaji waliobaki wa MNF wanaweza kumuweka kitako mhuni kama Generali Nkunda na akawasikiliza?

..Mwalimu Nyerere hayupo tena kwa hiyo ni vizuri Taasisi nayo ikajipanga upya kuzingatia ukweli huo. ndiyo maana wengine tukapendekeza ianzishwe Presidential library ya Mwalimu Nyerere.

Kipindi cha uhai wake nadhani Nyerere the man na Mwalimu Nyerere Foundation vilikuwa vitu sawa. Aliitumia Foundation ku-channel energies zake. Hivyo mission statements za foundation zilikuwa zinatokana na personality yake.

Kwa sasa hayupo. Hivyo haiwezekani kutumia personality kuendesha taasisi yenye kubeba jina lake. Lakini inaonyesha kuwa bado kuna watu wanaotaka kutumia personality ya mwalim kuendesha MNF.

Kwa maoni yangu binafsi Library na foundation zinaweza ku-exist kwa pamoja. Kinachotakiwa tu ni mission statement na uwezo wa waanzishaji kuendesha vyombo hivyo bila kutegemea serikali.
 
Mustafa jaffer sabodo...wazimu gani ulifanya atoe million 800 kuchangia hii foundation? kuna kitu hapa...wakuu tunaomba data..
 
Nimekukubali mkuu, sasa wajipanga vipi kumshawishi kuondoa visasi, au wapendelea aendelee hivyo. Inaelezwa na Vitabu Vitakatifu kuwa ukikaa kimya huku jirani yako anaharibikiwa nawe unajumuishwa kwenye dhambi siku ya hukumu

Jk ni mtu wa visasi na wala hashauriki. Subiri uone atakayofanya term ya pili (kama akichaguliwa). Yale aliyojaribu kufanya Mwinyi (siongelei kuingiza nchi jumuiya ya kiislam hapa) yatakuwa cha mtoto.
 
Kipindi cha uhai wake nadhani Nyerere the man na Mwalimu Nyerere Foundation vilikuwa vitu sawa. Aliitumia Foundation ku-channel energies zake. Hivyo mission statements za foundation zilikuwa zinatokana na personality yake.

Kwa sasa hayupo. Hivyo haiwezekani kutumia personality kuendesha taasisi yenye kubeba jina lake. Lakini inaonyesha kuwa bado kuna watu wanaotaka kutumia personality ya mwalim kuendesha MNF.

Kwa maoni yangu binafsi Library na foundation zinaweza ku-exist kwa pamoja. Kinachotakiwa tu ni mission statement na uwezo wa waanzishaji kuendesha vyombo hivyo bila kutegemea serikali.

Mkuu Dakta Salim ana uwezo wa kutumia personality hiyo akipewa nafasi na waliohodhi taasisi hiyo...hata Jaji Warioba angeweza kwa kiasi fulani...au yule Profesa aliyekuwa mkwe wa Nyerere...
 
Back
Top Bottom