JK amteua Jaji Kiongozi mpya

JK amteua Jaji Kiongozi mpya

..

..

rais jakaya kikwete ameweka rekodi mpya katika utumishi wa idara ya mahakama nchini kwa kuwateua majaji wapya 20 wa mahakama kuu ya tanzania kwa mpigo.

Katika uteuzi huo umekwenda sambamba na mkakati wa kutoa nafasi kwa wanawake ambao umekuwa ukionekana zaidi katika nafasi za kisiasa kwa kutenga nafasi maalumu kwa wanawake, asilimia 30 ya walioteuliwa kuwa majaji ni wanawake.

Wanawake walioteuliwa ni alice chingwile ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa mkurugenzi msaidizi mambo ya katiba na sheria katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.

Wanawake wengine ni imani aboud aliyekuwa mkurugenzi msaidizi, utawala katika ofisi ya rais menejimeni ya utumishi wa umma; stella mugasha aliyekuwa mwanasheria mkuu tume ya uchaguzi (nec) na aisha nyerere, aliyekuwa hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa kilimanjaro.

Pia wamo aishiel sumari ambaye alikuwa mkurugenzi msaidizi idara ya mashitaka katika ofisi ya mwanasheria mkuu; na mwanaisha kwariko aliyekuwa msajili wa wilaya, mahakama kuu ya tanzania kanda ya iringa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na idara hiyo jana na kusainiwa na naibu msajili mwandamizi wa mahakama ya rufani, sophia wambura, imetaja wengine walioteuliwa kuwa ni wakili wa kujitegemea, aloyse mujulizi na mkurugenzi wa mashtaka nchini (dpp), geoffrey shaidi.

Wengine walioteuliwa ni msajili wa mahakama ya rufani, augustine mwarija, kaimu naibu msajili wa mahakama hiyo, zaiduni chocha na msajili wa mahakama kuu ya tanzania, augustino shayo.

Pia katika uteuzi huo wa kihistoria yumo jaji wa mahakama kuu ya zanzibar, sekieti kihiyo. Wengine ni msajili wa wilaya mahakama kuu ya tanzania, kanda ya arusha, shabani lilla na mkurugenzi mahakama za wilaya-rufani, lawrence uzia.

Taarifa hiyo iliwataja wengine kuwa ni mkurugenzi wa katiba na haki za binadamu, frederick werema, naibu mwenyekiti mahakama ya kazi, kakusulo sambo na mkurugenzi wa mahakama za mwanzo, mahakama ya rufani, agathon nchimbi.

Wengine ni msajili wa baraza la ushindani, amiri mruma na kamishna tume ya haki za binadamu, robert makaramba.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, uteuzi wa majaji hao wapya unaanza mara moja na taarifa kuhusu tarehe ya kuapishwa kwao na rais itatolewa baadaye.

Uteuzi huo wa kihistoria kutokana na wingi wao kwa mpigo, ni utekelezaji wa ahadi ya rais aliyoitoa wakati akihutubia bunge desemba 30, mwaka huu alipoahidi kwamba angeteua majaji wengi ili kukidhi upungufu wa majaji pia kuongeza uwezo wa idara ya mahakama kutekeleza majukumu yake.

Kumekuwako na kilio cha muda mrefu juu ya ucheleweshaji wa kesi mahakamani hususani mahakama kuu kutokana na upungufu wa majaji. Kasoro hiyo imekuwa ikielezwa kwamba ni kikwazo katika kutoa haki kwa raia.
 
..yeyote yule anayedai Jaji Jundu hakustahili nafasi ya Ujaji Kiongozi anapaswa kutuletea wasifu na CV za Majaji/Wanasheria ambao anaona wako more qualified.

..vilevile ingesaidia kama akitueleza kidogo kuhusu hukumu[au kesi walizoshiriki] mbalimbali zilizotolewa na Jaji huyu, na mchango wake ktk taaluma ya sheria. pia atueleze wanasheria[majaji,mawakili] wenzake wanamchukulia vipi Jaji huyo.

NB:
..ufafanuzi mdogo: ili mwanasheria aweze kutetea kesi mahakama kuu anapaswa kufaulu mtihani wa uwakili wa mahakama kuu.

..majaji wa mahakama kuu na wanasheria wa serikali hawahusiki na mtihani huo.

..kutokufanya mtihani huo hakumaanishi kwamba mhusika ni in-competent, bali tu hakuwa na nia ya kutetea kesi mahakama kuu.
 
Jobo haipendezi kupandikiza chuki za kidini.umeona kabisa kuwa jaji jundu ana uzoefu wa miaka 32 toka 1977 akiwa state attorney.

Unataka nini zaidi ya uzoefu huo wa miaka 32? DPP-FELESHI amepewa majukumu makubwa wakati akiwa amemaliza digri yake ya sheria-LLB mwaka 1996 huyo ndio ungemlaumu Rais kikwete kumpa madaraka ya ukurugenzi mkuu wa mashtaka huku akiwa hana uzoefu lakini kwa vile ni mkristu umekaa kimya.

nimetoa hoja ya kuwa Tido Mhando hana uzoefu wa menejiment na hana elimu ya kuwa mkurugenzi mkuu TBC hapo ndipo ungemlaumu Jk kwa udini kama Tido Angekuwa muislam.

Mzee Mkapa alimpa Erio kuwa mkurugenzi mkuu wa PPF wakati hana uzoefu na ujuzi ulikuwa wapi kulalamikia teuzi za upendeleo? tena ni mpwa wake.

Rita Mlaki alikuwa mfanyakazi wa kawaida Teggry Plastic kiwanda cha wahindi Pugu Road, Mzee wetu mkapa akampa ukuu wa wilaya na baadae uwaziri.

Hoja za Mwanakijiji wakati mwingine zinakuwa na utata mkubwa, kwenye salamu za mwaka mpya za redio yake alisema na kumtaja jina DR.Dau kuwa si kiongozi wa maana na hatamwacha na kulikuwa na thread alizochangia sana kueleza mapungufu yake, haijapita miezi miwili toka salamu za mwaka mpya zikikamia kupambana na DR.Dau ghafla ameandika makala kwenye Jarida lake la Cheche ya kumpamba na kusema ndiye kiongozi mwenye uwezo na uzoefu wa kuongoza Bandari yetu.

swali ambalo najiuliza ni kuwa mtu aliyekuwa hana maana na hajui kazi yake mwezi uliopita leo anatolewa mfano wa kuwa mtendaji bora mwenye uwezo wa kuokoa jahazi la taifa letu linalozama.
Mwanakijiji licha ya kuwa MwanaJF lakini ni mwandishi wa magazeti mbalimbali nchini inapotokea anaandika hiki leo na kesho anakana alichoandika jana yake anaishushia hadhi taaluma ya uandishi na yeye mwenyewe.
 
kanda2 said:
DPP-FELESHI amepewa majukumu makubwa wakati akiwa amemaliza digri yake ya sheria-LLB mwaka 1996 huyo ndio ungemlaumu Rais kikwete kumpa madaraka ya ukurugenzi mkuu wa mashtaka huku akiwa hana uzoefu lakini kwa vile ni mkristu umekaa kimya.

..alipohojiwa na happyness katabazi, DPP Feleshi alisema yafuatayo:

DPP-FELESHI said:
Nimezaliwa Julai mosi, mwaka 1967, katika Kijiji cha Malya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, nikiwa mtoto wa mwisho kati ya watoto tisa wa familia yetu ya mzee Mussa Mbuki Feleshi na mama yangu Ruth N'gweshemi.
Baba yangu alikuwa mchungaji wa Kanisa la African Inland Church na mama alikuwa mama wa nyumbani.

Baba yangu alifariki mwaka 1973 kwa ajali ya gari na mama yeye alifariki mwaka 1991, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Nimesoma Shule ya Sekondari Shinyanga, baadaye nilijiunga na Shule ya Sekondari Galanos mkoani Tanga ambako nilisoma kidato cha tano na sita.

Baada ya kumaliza kidato sita nilijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT Ruvu).
Nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1991, nikichukua shahada ya kwanza ya sheria na kuhitimu mwaka 1994. mwaka 2003 nilirudi tena Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusoma shahada ya uzamili ya sheria (Masters in Law), nilihitimu mwaka 2005.
Kabla ya kuteuliwa kuwa DDP, nilikuwa Mwanasheria wa Serikali na kituo changu cha kazi kilikuwa mkoani Mwanza.

Hivi sasa ninasoma Shaha ya Udaktari wan Sheria PhD in Law Criminology and Penology. Nina mke mmoja, Suzana Majija, ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Nyamagana mkoani Mwanza na tuna watoto wanne.

ndugu zangu,

..unapost ujumbe wowote mfanye angalau na research kidogo.

..the bar has been set very high. there is no room for errors when posting in this thread.
 
ndugu zangu,

..unapost ujumbe wowote mfanye angalau na research kidogo.

..the bar has been set very high. there is no room for errors when posting in this thread.

Ayayayayayaiiii...aiseee ngoja (w)aione hii.....yaani hao jamaa wamekosea...Lord hammercy to what is coming to them
 
Nyani Ngabu,

..kuna haja gani ya kuzungumzia elimu ya mtu wakati hata mwaka alio-graduate huujui?

..kila mtu anajua kwamba hii thread ni noma, kwahiyo kila unacho-post lazima uwe na uhakika nacho.
 
Joka Kuu.
Unakubali kuwa JUNDU ameanza kufanya kazi 1977 kwenye fani ya sheria na ana miaka 32 kwenye hiyo fani hadi sasa?uzoefu huo bado hautoshi?

Feleshi nilichanganya baina ya 1994 na 1996 ila bado uzoefu wake ni mdogo kulinganisha miaka 32 ya Jundu inayosemwa kuwa ni michache na hana uzoefu kwenye fani ya sheria kama sikosei wakati Dpp Feleshi akiwa na miaka saba, Jaji Kiongozi Jundu alikuwa tayari ana practice Sheria kama Mwanasheria wa serikali.pia umenipa somo zuri sana kama watu wangeona Feleshi Mussa Feleshi ndio Dpp wangesema ni muislam lakini umeweka wazi kuwa baba yake alikuwa mchungaji wa kanisa.

Naamini hakuwahi kupita kwenye mtihani wa mawakili kama Jundu.wakati Dpp anamaliza chuo kikuu 1994 Jundu amekuwa mwanasheria kwa miaka 17 na amewahi kuwa mkuu wa vitengo vya sheria kwa nyakati tofauti.
 
kanda2,

..nakubaliana na wewe kwamba Jaji Jundu alimaliza LL.B yake mwaka 1977.

..kuna namna mbili ya kuangalia uzoefu wa Jaji Jundu kwa wadhifa huu wa Jaji Kiongozi.

..unaweza kukusanya miaka yake yote tangu ame-graduate.

..vilevile, kwasababu sasa hivi ameteuliwa kuongoza Majaji, unaweza kuangalia uzoefu wake tangu ameteuliwa na Mkapa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

..Baba Mzazi wa Feleshi ambaye alikuwa mchungaji wa kanisa alifariki mwaka 1973. wakati huo DPP Feleshi alikuwa na umri wa takriban miaka 6.

NB:

..kwani Jaji Kiongozi Fakihi Jundu ni Muislamu?

..hivi ikitokea kwamba siyo Muislamu utaendelea kumtetea?

..na wenzako wanaomshutumu kwasababu wanaamini ni Muislamu watafanyaje?
 
Huu ni uongo wa mchana mchana.

Rais Kikwete ameteua majaji 31 (kwanza aliteua ishirini mwaka 2006, halafu 11, mwaka jana, 2008).

Katika hao 31, kuna watano ndio walitoka kwenye uwakili binafsi:

Jaji Zainabu Muruke,
Jaji Upendo Msuya,
Jaji Kassim Nyangarika,
Jaji Crecencia William Makuru, na
Jaji Aloyisius Mujulizi.

Katika hao watano, wanne wana majina yanayoelekea kuwa ya kidini (Kiarabu na Kiingereza), mawili yakiwakilisha kila moja ya dini mbili, Kassim na Zainabu, pamoja na William na Aloyisius. Wa tano, Upendo, ana jina la Kiswahili, aweza kuwa kokote.

Umetoa wapi wewe habari kwamba jaji Thomas Mihayo ndio Mkristo pekee kutoka katika uwakili binafsi?

Sasa, kufuatana na viwango vya hii thread, ambayo ina mambo nyeti, shutuma kali, hatari, za udini, upendeleo, na teuzi zisizo zoefu dhidi ya Rais (hili lilidhihirika uongo), ukisema lisilo sahihi na likawa kichocheo cha kushambulia Rais kwa mambo nyeti, hatari, ni sawa na upotoshaji wa makusudi. Uongo.

Na pia kwa viwango vya thread hii, ukisema uongo unawajibika, bila kuumauma maneno, wala kubadilisha, kukaza au kulegeza sauti.

Sasa Jobo umeongopa. Wajibika.

Jobo,
Kubali kuwa umeongopa na wewe, omba msamaha ili ulinde heshima yako. Huyo ambaye unaemtetea tayari amekiri alidanganya na ameomba msamaha.
Please do the needful to avoid impeachment.
 
Nyani Ngabu,

..kuna haja gani ya kuzungumzia elimu ya mtu wakati hata mwaka alio-graduate huujui?

..kila mtu anajua kwamba hii thread ni noma, kwahiyo kila unacho-post lazima uwe na uhakika nacho.

Siyo hii thread tu...ni forum nzima...hiyo ndiyo standard.....kama hujui hilo jaribu uone....
 
kanda2,

..nakubaliana na wewe kwamba Jaji Jundu alimaliza LL.B yake mwaka 1977.

..kuna namna mbili ya kuangalia uzoefu wa Jaji Jundu kwa wadhifa huu wa Jaji Kiongozi.

..unaweza kukusanya miaka yake yote tangu ame-graduate.

..vilevile, kwasababu sasa hivi ameteuliwa kuongoza Majaji, unaweza kuangalia uzoefu wake tangu ameteuliwa na Mkapa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

..Baba Mzazi wa Feleshi ambaye alikuwa mchungaji wa kanisa alifariki mwaka 1973. wakati huo DPP Feleshi alikuwa na umri wa takriban miaka 6.

NB:

..kwani Jaji Kiongozi Fakihi Jundu ni Muislamu?
Namsaidia Kanda2, Yes Fakihi Jundu ni Mwislam, tena mzaliwa wa Tanga,
..hivi ikitokea kwamba siyo Muislamu utaendelea kumtetea?
Kanda2 ameweka wazi uzoefu wa Jundu, na amekuwa anamtetea yoyote as long as ana sifa za kutetewa, kisichokubalika ni kuonekana hafai kwa kuwa tu ni Muislam. sasa kama nawe unaona kanda2 kaweka wasifu wa Jundu kwa kuwa tu ni mwislam itakuwa vilevile

..na wenzako wanaomshutumu kwasababu wanaamini ni Muislamu watafanyaje?

Watajibu wenyewe!!!
sawa Mkuu?
 
Jobo haipendezi kupandikiza chuki za kidini.umeona kabisa kuwa jaji jundu ana uzoefu wa miaka 32 toka 1977 akiwa state attorney.

Unataka nini zaidi ya uzoefu huo wa miaka 32? DPP-FELESHI amepewa majukumu makubwa wakati akiwa amemaliza digri yake ya sheria-LLB mwaka 1996 huyo ndio ungemlaumu Rais kikwete kumpa madaraka ya ukurugenzi mkuu wa mashtaka huku akiwa hana uzoefu lakini kwa vile ni mkristu umekaa kimya.

nimetoa hoja ya kuwa Tido Mhando hana uzoefu wa menejiment na hana elimu ya kuwa mkurugenzi mkuu TBC hapo ndipo ungemlaumu Jk kwa udini kama Tido Angekuwa muislam.

Mzee Mkapa alimpa Erio kuwa mkurugenzi mkuu wa PPF wakati hana uzoefu na ujuzi ulikuwa wapi kulalamikia teuzi za upendeleo? tena ni mpwa wake.

Rita Mlaki alikuwa mfanyakazi wa kawaida Teggry Plastic kiwanda cha wahindi Pugu Road, Mzee wetu mkapa akampa ukuu wa wilaya na baadae uwaziri.

Hoja za Mwanakijiji wakati mwingine zinakuwa na utata mkubwa, kwenye salamu za mwaka mpya za redio yake alisema na kumtaja jina DR.Dau kuwa si kiongozi wa maana na hatamwacha na kulikuwa na thread alizochangia sana kueleza mapungufu yake, haijapita miezi miwili toka salamu za mwaka mpya zikikamia kupambana na DR.Dau ghafla ameandika makala kwenye Jarida lake la Cheche ya kumpamba na kusema ndiye kiongozi mwenye uwezo na uzoefu wa kuongoza Bandari yetu.

swali ambalo najiuliza ni kuwa mtu aliyekuwa hana maana na hajui kazi yake mwezi uliopita leo anatolewa mfano wa kuwa mtendaji bora mwenye uwezo wa kuokoa jahazi la taifa letu linalozama.
Mwanakijiji licha ya kuwa MwanaJF lakini ni mwandishi wa magazeti mbalimbali nchini inapotokea anaandika hiki leo na kesho anakana alichoandika jana yake anaishushia hadhi taaluma ya uandishi na yeye mwenyewe.

Tatizo unafikiri tofauti yangu na mtu ni personal, it is not. Hata kesho ukisikia nimeandika kumsifia Lowassa unaweza ukashangaa kwa sababu utafikiri nilichosema huko nyuma ilikuwa chuki. Sina. Halafu mimi sijawahi kujiita mwandishi wa habari ni watu wengine wananiita hivyo.
 
Chuma,

..ukisoma posting ya kanda2 utaona anashutumu teuzi za Wakristo ambao kwa maoni yake ni incompetents.

..anatumia teuzi hizo kama kinga kwa Raisi asihojiwe na wananchi anapoteua Muislamu ambaye wananchi hao wanadhani ni incompetent.

..halafu badala ya kutetea uteuzi wa Jaji Jundu kwa kuwasilisha wasifu wake, kazi alizozifanya, na rekodi yake kama mwanasheria, muda mwingi unatumika kushambulia watu wengine.

..nadhani unaweza kutetea uteuzi wa Jaji Jundu bila kuingiza masuala ya imani yake.
 
Mwanakijiji.
Watu wengi wanajua wewe ni mwandishi kwa vile unaandika kwenye magazeti,anayefundisha shuleni huitwa mwalimu hata kama yeye hajajiita mwalimu.anayeandika kwenye magazeti ataitwa mwandishi kutokana na maandishi yake anayoandika kwenye gazeti hata kama yeye hajajiita Mwandishi.wewe ni mwandishi hata kama hujajiita kazi zako za kiandishi.

Suala la DR.Dau ulisema kuwa uwezo wake ni mdogo wa kiutendaji na taratibu nyingi anapindisha za kuendesha shirika la Nssf.Uliandika kwa kina kwenye mjadala wa Nssf vs DR.Masau uko humu humu Jf.

kama mtu hana uwezo wa kiutendaji na amevuruga shirika la hifadhi ya jamii,ghafla unasema kafanya mambo makubwa kwenye shirika hilo na apewe dhamana ya kuongoza mamlaka ya bandari kutokana na umahiri wake na kipawa cha uongozi,jee nishike kauli ipi? hii uliyoandika kwenye cheche ya kusema DR.Dau ni mtendaji wa mfano kwa watanzania au ile ya kwanza ya kusema kuwa hana kitu anaendesha shirika kienyeji? au salam zako za mwaka mpya kwenye KLH News za kusema utapambana nae bila kuogopa kitu?

Naamini uliposema hana uwezo wa kuongoza Nssf na utapambana nae ulisema kwa maslahi ya Taifa si personal na kauli hii ya Cheche la wiki hii kuwa ana uwezo na ujuzi mkubwa apewe Bandari umesema kwa maslahi ya Taifa.

swali kama mtu ambaye ulisema hana uwezo kiutendaji miezi miwili iliyopita leo unataka taifa limpe dhamana ya Kuongoza bandari yetu?

Swala la Jaji jundu tuliache sasa tujadili Jaji mpya kachaguliwa na Rais Kikwete anaitwa Catherine Opiyo amechaguliwa leo kwenda mahakama ya Rufaa.tupeni wasifu wake,dini yake, ameolewa au bado,kwanini kamchagua Mwanamke ameacha wanaume
 
Chuma,

..ukisoma posting ya kanda2 utaona anashutumu teuzi za Wakristo ambao kwa maoni yake ni incompetents.

..anatumia teuzi hizo kama kinga kwa Raisi asihojiwe na wananchi anapoteua Muislamu ambaye wananchi hao wanadhani ni incompetent.

..halafu badala ya kutetea uteuzi wa Jaji Jundu kwa kuwasilisha wasifu wake, kazi alizozifanya, na rekodi yake kama mwanasheria, muda mwingi unatumika kushambulia watu wengine.

..nadhani unaweza kutetea uteuzi wa Jaji Jundu bila kuingiza masuala ya imani yake.

Jokakuu, Kanda2 alichofanya ni comparison analysis na sio kushutumu teuzi za wakristo....Kama watu wanamhoji Rais kwa kuteuwa mwislam, kwanini hawakuhoji alipoteuliwa mkristo ambae ana sifa za chini....!!

kanda2 katuletea ushahidi kuonesha uzoefu wa JUndu ktk Fani ya sheria, na nafikiri ukifuatilia kwa makini kina nani walianza kutoa hoja za Udini wa JK kumteua Jundu, so usitegemee atakaekuja kutetea ataacha kufuta nadharia potofu. Unapojibu Hoja, kwanza unaondoa uchafu uliowekwa then unaendelea kutoa hoja zinazotakiwa.
 
Tatizo unafikiri tofauti yangu na mtu ni personal, it is not. Hata kesho ukisikia nimeandika kumsifia Lowassa unaweza ukashangaa kwa sababu utafikiri nilichosema huko nyuma ilikuwa chuki. Sina. Halafu mimi sijawahi kujiita mwandishi wa habari ni watu wengine wananiita hivyo.

Bado nasubiri jibu lako, Ulitutangazia kuwa DR.Dau hafai na afukuzwe kazi na decemba 31 kwenye salamu zako za mwaka mpya ulisema kuwa utapambamba nae kwa maslahi ya Taifa.
swali kuna lipi la maana kalifanya hapa katikati kiasi cha wewe kumpigia debe awe Mkurugenzi wa Bandari?au uliyokuwa ukiyasema huko nyuma ilikuwa ni issue zenu za personal? au hivi sasa una maslahi yako binafsi kwa huyu bwana ndio maana unampigia debe?
Hujajibu hoja.
 
Naona unatafuta ligi isiyo ya lazima:

Suala la DR.Dau ulisema kuwa uwezo wake ni mdogo wa kiutendaji na taratibu nyingi anapindisha za kuendesha shirika la Nssf.Uliandika kwa kina kwenye mjadala wa Nssf vs DR.Masau uko humu humu Jf.

Sijawahi kusema mahali popote juu ya uwezo wa Dr. Dau kuhusu utendaji na kuwa taratibu nyingi amependisha. Huu ni uongo. Tofauti yangu na Dr. Dau ilihusiana na vifo vya watoto Tabora, ujenzi wa jengo lililohusika katika vifo hivyo, na nilisema kati ya watu wanaotakiwa kuwajibishwa/kuwajibika kwa hilo wa KWANZA ilikuwa ni Dr. Dau kwa sababu ndiye Mkurugenzi Mtendaji. Period. Msimamo huo ningeuchukua kama Mkurugenzi angekuwa Sospeter Paulo, David Mattaka, au Andrew Chenge!

Kauli yangu hiyo na msimamo huo bado ninausimamia kwani ripoti ile ilionesha wazi kuwa NSSF inawajibika kutokana vifo hivyo. Na zaidi ya yote nilisema hata Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF Bi. Blandina Nyoni awajibike pia.

Msimamo huo ni sawa na ule niliochukua kwenye ATCL ambapo David Mattaka na Mustaffa Nyang'anyi nilipendekeza wawajibike/wawajibishwe. Hili linatokana na principle siyo chuki binafsi.

Katika salamu zangu za mwaka mpya na maandishi yangu kuhusu suala lile utaona nilisema wazi kuwa sina tatizo lolote la Dr. Dau kwenda sehemu nyingine au kupangiwa kazi nyingine kwani kwangu haikuwa kuhusu uwezo kwa sababu nitakuwa mwongo nikisema kuwa NSSF chini ya Dr. Dau haijafanikisha mambo kadha wa kadha.

La pili ni hata hivyo umeshindwa kusoma kilichotoka kwenye kijarida cha Cheche na hutaona maoni yangu. Sijampigia debe aende Bandari, sina sababu ya kufanya hivyo, na kwa taarifa tu aendelee kukaa hapo hapo NSSF kama ushuhuda, kama vile Mattaka anavyoendelea kukaa ATCL au Idris Tanesco.

Bandari atapelekwa mtu mwingine kabisa unless waamue kumpeleka Dr. Dau.

Nadhani nimejibu maswali yako.
 
Mie siwezi kusema wewe ni muongo ila kumbukumbu zimo humu.unachokisema sio kweli kuwa kwenye suala la Jengo la Tabora ndio umetofautiana na DR.Dau nimesoma sana thread ya DR.Masau vs Nssf na ulikosoa mambo mengi hadi ajira za Nssf kuwa ni kienyeji sana, unaweza kuweka link ya salam zako za mwaka mpya KLH News ili kila mtu asikie ulichokisema.

kumezuka watu wa aina mbali mbali ambao dakika moja wanasema hivi na muda si mrefu wanabadilika. tunao kina Tambwe Hizza walikuwa wakipita na kutuambia kuwa CCM si chama na matusi mengi ghafla wanaisifia CCM wakati katiba na uongozi wa CCM ni ule ule waliotukana jana, yaani hakuna kilichobadilika ila ni mambo binafsi ya mtu.

Habari zako za toleo la cheche la wiki hii zimenitia shaka kwani umekuwa kama kinyonga unabadilika kila uchwao.
 
Mie siwezi kusema wewe ni muongo ila kumbukumbu zimo humu.unachokisema sio kweli kuwa kwenye suala la Jengo la Tabora ndio umetofautiana na DR.Dau nimesoma sana thread ya DR.Masau vs Nssf na ulikosoa mambo mengi hadi ajira za Nssf kuwa ni kienyeji sana, unaweza kuweka link ya salam zako za mwaka mpya

Ni wewe umesema kuwa ati niliwahi kusema Dr. DAu hafai na kuwa nilihoji uwezo wake. Kumbukumbu hizo umesema zimo humu. Ni jukumu lako kuzitafuta na kuzionesha hapa kama ushahidi kwani mimi nimekuita wewe muongo kwani sijawahi kusema hivyo. Mjadala mzima upo hapa.

Hata hilo la ajira ni maneno yako kuwa ni "kienyeji sana" sikusema hivyo. Kama unaamini nimesema tafuta ushahidi uko hapa, kwanini tuandikie mate?

Kuhusu salamu zangu za mwaka mpya bila ya shaka unajua zilipo unaweza kuweka link wewe mwenyewe ili watu wasikilize kama ushahidi dhidi yangu.

Habari zako za toleo la cheche la wiki hii zimenitia shaka kwani umekuwa kama kinyonga unabadilika kila uchwao.

unazitilia mashaka habari za GT pia kuhusu hiyo hiyo Bandari zilizokuja siku kadhaa baada ya mimi kuandika kuhusu ufisadi huko?
 
Huu ni uongo wa mchana mchana.

Katika hao 31, kuna watano ndio walitoka kwenye uwakili binafsi:

Jaji Zainabu Muruke,
Jaji Upendo Msuya,
Jaji Kassim Nyangarika,
Jaji Crecencia William Makuru, na
Jaji Aloyisius Mujulizi.

Bro, huyu Upendo Msuya ni yupi? Kuna wakati fulani nikiwa bongo, Mzee mmoja wa "system" akawa ananipa stori kuhusu Kiongozi wa nchi anavyofanya mambo kienyeji. Akanipa mfano wa dada/mama mmoja ambaye (to the best of my memory) alikuwa anamiliki Antelope Safaris - kampuni ambayo ofisi zake ziko Millenium Tower, Kijitonyama. Huyu mama ilikuwa ateuliwe "within few days" kushika wadhifa fulani nyeti (based on the principle of camaraderie or personal affairs). I suspect ni huyu Upendo Msuya. Someone should know what I am trying communicate.
 
Back
Top Bottom