tume ya haki za binadamu yapata katibu mtendaji
tume ya haki za binadamu na utawala bora imepata katibu mtendaji mpya ambaye ni wakili wa kujitegemea, upendo msuya (50), aliyeapishwa na rais jakaya kikwete, jana ikulu.
msuya, mwenye uzoefu wa masuala ya sheria kwa zaidi ya miaka 25, aliteuliwa na rais kikwete kushika wadhifa huo, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na gad mjemmas, aliyeteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu ya tanzania mwishoni mwa mwaka jana.
Waliohudhuria sherehe fupi ya kuapishwa kwa msuya ni pamoja na makamu wa rais, dk. Ali mohamed shein, waziri mkuu, edward lowassa, waziri wa nchi ofisi ya rais (siasa na uhusiano wa jamii), kingunge ngombale-mwiru, waziri wa katiba na sheria, dk. Mary nagu, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora, jaji robert kisanga.
Viongozi wengine waliohudhuria katibu mkuu kiongozi (ikulu), philemon luhanjo, katibu mkuu wizara ya katiba na sheria, sazi salula, na mkurugenzi mkuu wa takukuru, edward hoseah, makamishna wa tume ya haki za binadamu na baadhi ya maofisa waandamizi wa tume hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuapishwa kwake, katibu mtendaji huyo mpya alisema moja ya masuala muhimu atakayoanza nayo ni kuhakikisha majukumu ya tume yanatangazwa vya kutosha kwa wananchi, ili wajue namna ya kuitumia katika matatizo ya ukiukaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
uzoefu wa kisheria na masuala ya utawala alionao msuya unatokana na kuwa hakimu mkazi katika mahakama za kivukoni na kisutu (1983-1991), mkurugenzi wa idara ya mahakama za mwanzo (1992- 1996), wakili wa kujitegemea (1996 hadi sasa), wakili wa serikali na msajili wa makampuni na masuala ya hatimiliki katika serikali ya botswana (1998 – 2004).