JK ahaha kupandikiza kibaraka wake TUCTA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ahaha kupandikiza kibaraka wake TUCTA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 25, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Mgaya apata mpizani TUCTA


  na Datus Boniface


  [​IMG] MJUMBE wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA), Mussa Mnyeti ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Katibu Mkuu ndani ya chama hicho.
  Hadi sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Nicolas Mgaya, ambapo uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho unaratajiwa kufanyika Agosti mwaka huu.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mnyeti alisema nia, uwezo, na sababu anazo za kuwania nafasi hiyo.
  “Uwezo, nia na sababu ninazo za kuwania na kuwa Katibu Mkuu wa TUCTA, kwa ajili ya maslahi ya wanachama na wafanyakazi wote nchini Tanzania, vijana nawaomba wanikubali katika hili kwa ajili ya malengo hayo yaweza kufanikiwa,” alisema.
  Alisema sababu zilizomfanya kuwania ni pamoja na kuleta ushirikiano baina ya wafanyakazi na vyama vyao.
  Alitaja sababu nyingine ni kupigania haki, maslahi pamoja na usawa wa wafanyakazi wa ngazi zote.
  Katika maelezo yake alisema endapo akipata nafasi hiyo atapigania kima cha chini cha mshahara kiwe shilingi 315,000 ili kutimiza pendekezo la TUCTA.
  Alisema pia atapunguza kodi za wafanyakazi kutokana na makato mbalimbali yanatofanywa katika mishahara yao.
  Aidha aliahidi kuwapigia wafanyakazi kulipwa asilimia saba la pato la taifa.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Kweli JK ni kiboko.huku anawashawishi TUCTA wamkubali kwa kuwaahidi mishahara wafanyakazi bajeti ijayo na wao walivyo viruka njia wamemwalika katika sherehe ya MEI moSI.kumbe mwenzio anapanga kuwasarambatisha kwa kuwawekea mamluki.........poor TUCTA..............................................
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Kwa nini ni kibaraka wa JK? CV yake tafadhali...
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es SalaamMnyeti alisema niauwezona sababu anazo za kuwania nafasi hiyo.
     
  "Uwezo, nia na sababu ninazo za kuwania na kuwa Katibu Mkuu wa TUCTA,   kwa ajili ya maslahi ya wanachama na wafanyakazi wote nchini Tanzania,   vijana nawaomba wanikubali katika hili kwa ajili ya malengo hayo  yaweza  kufanikiwa," alisema.
     
  Alisema sababu zilizomfanya kuwania ni pamoja na kuleta ushirikiano baina ya wafanyakazi na vyama vyao.
     
  Alitaja sababu nyingine ni kupigania hakimaslahi pamoja na usawa wa wafanyakazi wa ngazi zote.
     
  Katika maelezo yake alisema endapo akipata nafasi hiyo atapigania  kima  cha chini cha mshahara kiwe shilingi 315,000 ili kutimiza  pendekezo la  TUCTA.
  Tueleze rekodi yako ya kuwapigania wafanyakazi inasemaje????????????????????????????? Kabla ya wafanyakazi kuamini ahadi zako...............
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Alisema pia atapunguza kodi za wafanyakazi kutokana na makato mbalimbali yanatofanywa katika mishahara yao.
     
  Aidha aliahidi kuwapigia wafanyakazi kulipwa asilimia saba la pato la taifa.
  Kwa hii si ni hoja tayari ipo mezani kwa serikali.........................mbona huna jipya??????????????????????????????????
   
 6. stanluva

  stanluva Senior Member

  #6
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kaka huyu alikuwa MKufunzi pale Monduli TC sijui kama ameacha, na alikuwa mkimbiza mwenge karibu muda wote alipokuwa pale TC. Pia ni kada wa CCM hata ukikutana naye utamkuta "amebeba Jembe na Nyundo {Joke)".
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Jakaya anataka kupandikiza mamluki hapo TUCTA ili awe boya lake na wafanyakazi wasiwe na sauti ya kupigania hakizao; watakuwa wajinga sana wakimtosa Mgaya wakati huu!! Ajenda iko pale pale lazima kumtoa Nicholas na kumuingiza Mussa, mnaiona hiyo wanajanvi halafu jamaa anahubili kupiga vita udini wakati yeye kwa vitendo vyake ndio muasis i wa huo udini!
   
 8. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ninamashaka na vyama vya wafanyakazi. Wanataka serikali ipunguze kodi katika mishahara ya wafanyakazi wakati vyama hivyo vinachota kutoka mishahara ya wafanyakazi makato ya kila mwezi bila kuwaonyeshea mapato na matumizi mwisho wa mwaka. vyama hivi vinapeleka wapi michango ya wafanyakazi?
   
 9. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Hawa nao nahisi pia ni mafisadi tu.Kila mwezi wanachukua fedha zetu lakini hata siku moja hawatuelezi ni namna gani wametumia,wezi tu!Kwanza mi nashangaa wananikata bila ridhaa yangu na faida yake wala siijui....UPUUZI MTUPU!
   
 10. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Musa Mnyeti chizi flani hivi, waliosoma UDSM kwa 2002 - 2006 watakuwa wanamkumbuka vizuri, kituko kikubwa alichowahi kukitoa ni pale alipochukua form ya kugombea uspika na akina msekwa na sitta akiwa mwaka wa tatu.
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Basi kweli atakuwa ni mamluki.
   
 12. S

  Songasonga Senior Member

  #12
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhhh tusiharibu uchaguzi Huu mzito tusiponde mtu ili kumbeba Mgaya. Angalizo tu huyu wala simjui vizuri huyu Mnyeti lakini asibambikiwe vitu kunyoosha njia ya Mgaya ambaye nilisikia Pia ana uhusiano mzuri tu na baadhi ya Mafisadi
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Ndiyo na Hapana, ndiyo kwasababu hakuna linaloshindikana duniani lakini hapana kwakuwa kila mtu anamfahamu jinsi asivyo makini, hupenda kutafuta umaarufu usio wa lazima, kifupi anaonekana ni chizi zaidi. Alipo pewa kuongoza mbio za mwenge ilikuwa ni kumjaribu kwa kazi nyingine za chama lakini alichemka sana, chama kikamsusa ndio maana kaishia kwenye ualimu, vijana wenzake wengi wamepewa nafasi katika chama au kazi nyingine za maana.
   
 14. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  JK ni mdini kwa vitendo na anatuhadaa wadanganyika kwa maneno .

  Angalia uteuzi wake, majaji, wakurugenzi, wakuu wa vyuo, mawaziri and you name them. Kwa hiyo Jk anatuhadaa kwa maneno ili tusahau kuhoji kuhusu uteuzi wake

  Angalia jinsi alivyowadanganya watanzania kuhusu maisha bora kwa kila mtanzania.= maisha bora yako wapi, leo kuna mfumuko wa bei.

  Wafanyabiashara wanakumbatiwa, wanapigwa busu wakati watanzania wanaumia na bei mbaya ya sukari.

  Sukari ni hitaji muhimu na lazima kwa masikini watanzania -
  Watanzania tunaumia saaanaaaa.

  Kukatwa kodi mara mbili mbili.... (PAYE na VAT) mfumuko wa bei na huku wafanyabiashara wanakwepa kodi na kuwanyonya watanzania.

   
 15. c

  ckam Member

  #15
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Watz sasa tupo kwenye mchakato wa mageuzi ya kiuongozi. Viongozi tunaowataka ni waadilifu na wachapakazi na wala si viongozi wa kupachikwa pachikwa na umamuluki ndani yake. Tutataka kuona yeye anauweza uongozi kiasi gani zidi ya Mgaya vinginevyo akaendelee kukimbiza mwenge maana hatapata!
   
 16. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Na Mgaya mwambieni aje CDM tutampa cheo ngazi za juu maana ameonyesha anaweza kukaa pande za huku kidogo. Ila ndo kufulia kwake kunaanza. Malaria huanza taaaaaratiiibu
   
 17. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hao wanaochagua viongozi tucta wakifanya kosa kumuacha Mgaya kiboko ya JK watakuwa wamekosea maisha yao yote!!Musa waachane nae kwa sasa maana anapandikizwa kuua Tucta!isiwe nguvu pia watauaa CWT kuweka watu wao....angalizo
   
 18. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sahihisho mkuu, 2002 - 2006 kwa Msekwa na Sitta kusema walikuwa UDSM naona kama ni typing error vile. Weka vizuri hapo.
   
 19. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #19
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  usahihi ni kwamba, Mnyeti aligombea uspika wa bunge la jamhuri yeye mnyeti akiwa mwaka wa tatu chuo. si kwamba wote walikuwa chuo na wakagomea uspika wa bunge la wanafunzi.
   
 20. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Una USHAHIDI NA ULICHO ANDIKA? TUWEKEE WAZI,USIPOTOSHE WENGI!
   
Loading...