KERO Makete: Walimu 17 watishiwa kushtakiwa

KERO Makete: Walimu 17 watishiwa kushtakiwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WALIMU 17 WATISHIWA KUFUNGULIWA MASHITAKA KWA KUTAKA KUHAMA CHAMA CHA WALIMU WILAYANI MAKETE, MKOANI NJOMBE

Makete – Wakati haki ya kujiunga na kujiondoa kwenye vyama vya wafanyakazi ikiwa imehifadhiwa katika Katiba ya Tanzania na kanuni za kimataifa za kazi, hali ya kustaajabisha imejitokeza Wilayani Makete ambako Walimu 17 wa shule ya sekondari Matamba wanakabiliwa na tishio la kufunguliwa mashitaka na mwajiri wao kwa kushirikiana na uongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani humo.

Tishio hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa CWT Wilayani Makete, ndugu Nkwama, alipokuwa akizungumza na walimu hao kupitia kwa mwakilishi wa chama tawini. Mwenyekiti alisema ana nia ya kuwafungulia mashitaka walimu 17 hao kwa sababu wanataka kuhama chama – hatua ambayo yeye anadai inakwenda kinyume na “makubaliano” baina ya chama chake na uongozi wa serikari ya wilaya kupitia ofisi ya afisa utumishi. Kwa mujibu wa Mwenyekiti Nkwama, makubaliano hayo yanataka chama kimoja tu ndicho kiendeshe shughuli zake wilayani Makete.

Akiongea kwa sauti ya kujiamini, Mwenyekiti Nkwama alidai wazi kuwa chama chake kina nguvu na “kimeishika serikali ya wilaya” kwa sababu kinafadhili vikao vya kuwapandisha walimu madaraja na kugharamia shughuli nyingine za ofisi ya mkurugenzi wa wilaya. Alisema, atakutana na mkurugenzi ili kuzuia uhamaji huo pamoja na kuwachukulia hatua Kali walimu husika.Ili kuthibitisha uhakika wake, Mwenyekiti alimwambia mwalimu kwa njian ya simu Fatson Mwampashe, kuwa ikiwa hata mwalimu mmoja tu atafanikiwa kuhama chama, yeye (Mwenyekiti) atamlipa Shilingi 20,000.

Kauli hiyo ilichukuliwa kama ishara ya dharau dhidi ya jitihada za walimu kutumia haki yao ya kikatiba – au kama ushahidi wa kujiamini kupindukia katika uwezo wake wa kuzuia mchakato huo.

Sababu za walimu kutaka kuhama: Sio siasa, ni uchumi

Walimu 17 hao wameshangazwa na kufadhaishwa na tishio hilo. Katika mahojiano, mmoja wa walimu hao (aliyependa kutotajwa kwa usalama) alisema waliamua kuomba kuhama chama si kwa sababu za kisiasa, bali kwa sababu za kiuchumi.

“Tunachotaka ni kutumia haki yetu ya kikatiba. Lakini pia tunatafuta nafuu ya kimaisha. Chama tunachotaka kuhamia kinakata Sh 5,000 tu kwa mwezi, ilhali CWT inakata Sh 34,700 kwa mwezi. Hiyo ni tofauti ya Sh 29,700 – kiasi kikubwa kwa mwalimu wa wilayani,” alisema mwalimu huyo.

Aliongeza: “Kwa mfano, Sh 29,700 kinatosha kununua mtungi wa gesi unaoweza kutumika kwa mwezi mzima. Hivyo fedha itakayookolewa itatosha kugharamia nishati safi ya kupikia kwa mwaka mzima", ikiwa kiasi Cha 297000 kwa mwez ni zaid ya annual increment, kwanini wao wadharau kiasi hicho. Alihochi mwalimu huyo.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 20(1) cha Katiba ya Tanzania, kila mtu ana haki ya kujumuika na wengine, ikiwemo haki ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi. Pia, Sheria ya Mahusiano ya Kazi (2004) inalinda haki ya mfanyakazi kujiondoa kwenye chama chake kwa hiari bila adhabu.

Tukio hili Makete linaibua maswali muhimu:
· Je, makubaliano kati ya chama na serikali ya wilaya yanaweza kupuuza Katiba?
· Je, ni kwa nini Mwenyekiti wa chama anaona kufanikisha kutokuhama kwa walimu kama “ushindi” ?
· Je, chama kinachotumia fedha kugharamia vikao vya kupandisha madaraja watumishi ambao ni wajibu wa mwajiri kama nyenzo ya kudhibiti walimu bado ni chama cha wafanyakazi au tawi la utawala?
 
Back
Top Bottom