Nadhani Ridhiwani ni kiongozi bora, nitamuunga mkono

Nadhani Ridhiwani ni kiongozi bora, nitamuunga mkono

zee_latown

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2026
Posts
523
Reaction score
925
Wanjamvi na geniuses wa HnM sakamu!

Nimetafakari sana, nimewaza na kuwazua. nikahitimisha kuwa hakuna kisicho na dosari. Mhe. Ridhiwani Kikwete ni kiongozi bora, ni bora ndiyo, na siku hapo mbeleni akitangaza nia ya kujaribu kugombea Urais, nitamuunga mkono 100%. Sababu zangu zipo hapo chini:

Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)

1. Kuharakisha Ajira Mpya: Aliamuru Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuharakisha na kuweka wazi michakato ya usaili wa nafasi za kazi zaidi ya 12,000 zilizotolewa na serikali ili kupunguza mrundikano na urasimu kwa vijana.

2.Mifumo ya Serikali Mtandao: Alihamasisha taasisi za umma kutumia mifumo salama ya kidijitali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa haraka na gharama nafuu.

3. Kuwajibisha Watumishi: Alisimamia uadilifu na uwajibikaji kwa kufuatilia kwa karibu kero za watumishi wa umma na kuhakikisha haki zao zinalindwa.

Wizara ya Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu

1. Kutetea Haki za Wafanyakazi: Alishirikiana kwa karibu na mashirika ya wafanyakazi kama Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kusikiliza changamoto zao ili kuboresha maslahi na mazingira ya kazi nchini.

2.Usimamizi wa Mifuko ya Jamii: Alihimiza ufanisi wa utendaji wa taasisi za hifadhi ya jamii kama vile Mfuko nwa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili kuhakikisha mafao yanatolewa kwa wakati kwa walengwa.

Hizo pamoja na sababu nyingine nyingi, zinaniwia kuvutiwa na huyu Mheshimiwa kuwa namba moja miaka ya mbeleni, ili atatue changamoto mbali mbali za wananchi.

Nitamuunga mkono asilimia zote.
 
Binafsi namfahamu ridhiwani tangu akiwa mwenyekiti wa faculty of law UDSM
Akiishi hall 6
Yule bwana anabebwa na mfumo ni mtu wa hovyo sana.
Ningeandika visa vingi alivyokuwa alifanya chuo yeye na nehemia lakini nikwambie tu rizione ni mtu wa hovyo anayebebwa na jina la babake
 
Binafsi namfahamu ridhiwani tangu akiwa mwenyekiti wa faculty of law UDSM
Akiishi hall 6
Yule bwana anabebwa na mfumo ni mtu wa hovyo sana.
Ningeandika visa vingi alivyokuwa alifanya chuo yeye na nehemia lakini nikwambie tu rizione ni mtu wa hovyo anayebebwa na jina la babake
people commit wrongs, learn, and change
 
Back
Top Bottom