Weusi tuna shida...nchi hii ina serikali, kisha Halmashauri, kuna MIPANGO MIJI etc.
Watu wanajitafutia eneo, wanaendeleza kama mchwa tu, huduma za kijamii zinapelekwa, jamaa wanaanza kuchukua kodi za majengo, baada ya miaka 10, wanakuja kusema tunapima maeneo hivyo hivyo ilivyojengwa...miaka 2 inayofuata, wanaanza bomoa bomoa kupitisha road.
Yote hayo ni ndani ya miaka pengine 20, baada ya mwaka 2000. Kipindi ambacho nchi tayari ina umri wa mtu mzima.
Sasa, ilipaswa kuwa, MAENEO YA MAKAZI, kusiwe na Duka, bar, genge, kanisa, msikiti n.k
- Acha makazi yawe makazi
- Tenga maeneo ya karibu, tena ikiwezekana opposite na makazi au vyovyote, weka huko biashara zote na majengo ya kiimani.
Hii itasaidia hata kupunguza matuta ya kipumbavu barabarani na vibao vya spidi 50.
- Nyumba huku, duka lipo upande wa pili wa road, bar iko upande mwingine...lazima uweke tuta hapo, kuna mlevi, kuna mtoto anayetumwa kwenda dukani n.k
Tunasubiri tuje tupangiwe na weupe! Sisi tunahamasishana kula kwa urefu wa kamba.