Jirani yangu kuna kanisa la walokole

Jirani yangu kuna kanisa la walokole

Nilisema misikiti na makanisa yavunjwe ni upumbavu kila mtu aswali na kumuomba mungu nyumbani mwake DINI azijaleta faida yoyote hata moja...misikiti 2 na makanisa 2 kia wilaya yanatosha au kwa kuanziatunaweza kuamlisha siku ya ibada iwe moja tu kama ilivyo amriwa waislamu ijumaa tu kisha misikiti ifungwe kelele za kuitwana swala zisiwepo nq wakristo ni siku moja tu kwa week.
Kwanini misikti ivunjwe na makanisa yavunjwe? Basi hata uwanja wa mkapa uvunjwe maana wakicheza Yanga na Simba maeneo ya jirani huipata Pata kwa adha na fujo za wasshabiki
 
Adhana dakika 2 tu sio kero, kero kama amewasha maspika wanatia makasida au madufu. Hilo Hilo halikubaliki..lkn kama anatoa mawaidha Hilo ni kero dogo sana maana anaongea mtu mmoja tu na wengine husikiliza. Kuongea mtu mmoja sio kero

Haya si ndiyo ya nyani kutoona nanihii?
 
Fika ofisi ya Kata iliyopo karibu na wewe, muone Mtendaji Kata nae atakuunganisha na wahusika wa Kitengo cha Mazingira

Ni kosa kisheria kuweka sauti juu ya kiwango kinachoruhusiwa kwenye eneo la Makazi, kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya 2004..CHUKUA HATUA!
 
Haya si ndiyo ya nyani kutoona nanihii?
Hatusemi kengele za kanisani za asubuhi au j2. Tunaongelea kuwasha maspika usiku , mchana na jioni kwa wiki nzima tena full. Au hujafahamu?
 
Hatusemi kengele za kanisani za asubuhi au j2. Tunaongelea kuwasha maspika usiku , mchana na jioni kwa wiki nzima tena full. Au hujafahamu?

Tuongelee vyote hadi bar, Sherehe, viwanja vya mipira, nk. Tukifanya hivyo na kuuweka ubinafsi pembeni suluhu itapatikana. Kwenye hilo apongezwe Kagame asiyeangalia makunyanzi!
 
Tuongelee vyote Hadi bar na viwanja vya mpira. Tukifanya hivyo na kuuweka ubinafsi pembeni suluhu itapatikana. Kwenye hilo apongezwe Kagame asiyeangalia makunyanzi!
Kagame kafanyaje?
 
Upuuzi ni upuuzi tu ila ngoja Malaria 2, Ritz na wenzao walete muongozo.
Kwa mujibu wa sheria za mazingira. Kuna standard db imewekwa kama kiwango cha sauti kinachovumilika kwenye makazi ya watu na juu ya hapo inakuwa ni kerere kisheria.

Wawapeleke mahakamani au aanze kuwashauri. Hata Waslam wanavyoitana kusali usiku kwa vipaza zauti huwa wanatunyima haki ya kusinzia. Kama ilivyo Bar.

Lakini kwa sababu ya uvumilivu wa kidini huwa tunapotezea. Ila kama wanakukera unaweza kuonana na kiongozi na kumpa madhara au hatua unazoweza kumchukulia. Viongozi wengi wa makanisa ni waelewa. Wakorofi wengi huwa ni waumini chawa ambao wanauelewa finyu kijamii
 
Nifanyeje?
Usiku na mchana ni kwaya tu, wakati mwengine wanatia kanda na kuwasha maspika ya nje wao wapo majumbani.
Hawana Jumamosi, jumapili au ijumaa , siku zote wao ndio hivyo.
Kuna shule karibu nao wanaipata Pata.
Tufanyeje? Tuhame mpaka shule nayo tuihamishe?
Na hapo lazima kanisa liwe la mabati😁
Sijui ndio agreed architectural design🤣
 
Kwanini misikti ivunjwe na makanisa yavunjwe? Basi hata uwanja wa mkapa uvunjwe maana wakicheza Yanga na Simba maeneo ya jirani huipata Pata kwa adha na fujo za wasshabiki
Umesoma nilicho andika...? Misikiti inatakiwa kuwa sehemu maharumu tu na makanisa ni hivyo hivyo bora kuwa na makanisa na misikiti michache mikubwa kuliko uchafu wa makanisa na misikiti kila uchochoro
 
Kagame kelele ni kelele tu iwe garage, msikiti, kabisa, mahubiri, sherehe, bar, mpira nk. Zote hizo ni KERO mbali na makazi ya watu!
Yeye kakaa madarakani miaka mingapi? Sio kero kwa watu? Basi hata vyoovya kunya viwekwe mbali na makazi ya watu yananuka
 
Nilisema misikiti na makanisa yavunjwe ni upumbavu kila mtu aswali na kumuomba mungu nyumbani mwake DINI azijaleta faida yoyote hata moja...misikiti 2 na makanisa 2 kia wilaya yanatosha au kwa kuanziatunaweza kuamlisha siku ya ibada iwe moja tu kama ilivyo amriwa waislamu ijumaa tu kisha misikiti ifungwe kelele za kuitwana swala zisiwepo nq wakristo ni siku moja tu kwa week.
Mbona husemi bar nazo ziwe mbili kila Wilaya?
Mlokole akienda kanisani kila siku ni tatizo ila mlevi akienda bar kila siku sio tatizo?!!
 
Umesoma nilicho andika...? Misikiti inatakiwa kuwa sehemu maharumu tu na misikiti ni hivyo hivyo bora kuwa na makanisa na misikiti michache mikubwa kuliko uchafu wa makanisa na misikiti kila uchochoro
Makanisa kila j2 ok, lkn misikiti kila saa 3 au 5 unatakiwa uswali..ukiweka mbali na watu si itakuwa kero?
 
Mbona husemi bar nazo ziwe mbili kila Wilaya?
Mlokole akienda kanisani kila siku ni tatizo ila mlevi akienda bar kila siku sio tatizo?!!
Ulisha wai kusikia taifa lolote limeingia kwenye machafuko kwa sababu ya uchochezi wa bar?....dini na madhehebu ni vitu hatari kwa taifa vikiendekezwa taifa linaweza kuangamia ...tumia akili
 
Yeye kakaa madarakani miaka mingapi? Sio kero kwa watu? Basi hata vyoovya kunya viwekwe mbali na makazi ya watu yananuka

Vyao kunuka ni vya uswahilini vya waungwana hunukia!

Kukaa madarakani ni kama CCM hudhani ni KERO Kwa wengine?
 
Ulisha wai kusikia tsifa lolote limeingia kwenye machafuko kwa sababu ya uchochezi wa bar dini na madhehebu ni vitu hatari kwa taifa vikiendekezwa taifa linaweza kuangamia ...tumia wkili
Madawa ya kulevya hujawahi kusikia? Vita vyake bikubwa
 
Makanisa kila j2 ok, lkn misikiti kila saa 3 au 5 unatakiwa uswali..ukiweka mbali na watu si itakuwa kero?
Ujui uislamu kuswali misikitini ni ijumaa zaidi swala 5 siyo msikitini wew unadhani waarabu awafanyi kazi awaendeshi meli awa safiri kwa ndege awaendi vitani huko msikiti hskuna ila swala zipo pale pale hata kipindi cha muhammad wewe unadhani kwa vimisikiti vichache na vidogo vya kipindi kile vingetosha waislamu wote wa muhammad...tambua tofauti ya swala 5 na msikiti ...swala siyo msikiti na msikiti siyo swala ...kumbuka wapo wafungwa kwenye majela ya duniani na hakuna misikiti je kwa mujibu ya uislamu awatakiwi kuswali swala 5 kwa sababu ya kukosa msikiti
 
Back
Top Bottom