Jinsi Ya Kutega Bahati Kwenye Uwekezaji Wa Viwanja, Mashamba Na Majengo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
“Generally, real estate is cyclical. You have to buy in a way that lets you afford the cycles. And you have to know where you are in the cycle.”
Charles Brown

Kukaa na kusubiri soko ya ardhi na nyumba ziwe vizuri, ni kujipotezea muda wako wa thamani.

Wala huwezi kupiga hatua kwa kusubiri kununua nyumba kipindi ambacho bei ya nyumba ni nafuu.

Unachotakiwa kufanya ni kuwa katika uwekezaji wa ardhi na nyumba muda wote. Kila siku ujifunze na uendelee kununua, kupangisha na hata kuuza nyumba.

Kwa kufanya hivi itakuwa rahisi kwako kukutana na fursa ambayo itabadili kabisa kiasi cha kipato chako.

Utakutana na fursa itakayoongeza kiasi cha kipato chako maradufu kiasi kwamba hutategemea tena ajira yako au biashara.

Hakuna mtu yeyote atakaye kuita na kukuambia huku kuna fursa njoo uwekeze pasipokuwa na jitihada zako wewe mwenyewe.

Mzunguko wa soko la nyumba hauwezi kukusaidia kuonyesha lini unaweza kununua nyumba kwa bei nafuu.

Kwa kujifunza njia mbalimbali za kutengeneza pesa katika ardhi na nyumba, unaweka mtego wa fursa za ardhi na nyumba.

Mtego utanasa fursa endapo utafanyia kazi maarifa unayopata ya uwekezaji katika ardhi na nyumba.

Usisumbuke na soko, sumbukia fursa zinazokuja mbele yako. Kuwa katika uwekezaji wa ardhi na nyumba haina maana utakuwa unanunua na kuuza kila siku.

Bali ina maana utakuwa unajifunza kila wakati na kuendelea kupata koneksheni ya watu wanaowekeza katika ardhi na nyumba.

Unatakiwa kuendelea kushirikiana na watoa mikopo, mawakala, madalali, mawakili, washauri, na wahasibu.

Unatakiwa kuendelea kujifunza kuhusu uwekezaji katika ardhi na nyumba kila mara.

Kutafuta kununua nyumba kwa mwaka fulani ambao soko linaonekana lipo chini, ni njia ya hovyo ya kufikia uhuru wa kifedha kupitia uwekezaji wa ardhi na nyumba.

Usitafute mwaka au mwezi ambao nyumba zinazouzwa kwa bei nafuu.

Jicho lako lifanye kazi wakati wote kupata nyumba katika mkoa au wilaya au jiji unalotaka kuwekeza.

Ukikutana na fursa hakikisha inakuwa ya kwako. Na usiuze nyumba na ardhi bila sababu za msingi.

Ukinunua nyumba ya kupangisha, kwa mfano, hakikisha unaimiliki kwa zaidi ya miaka kumi (10).

Kwa kipindi cha miaka 10, nyumba yako itakuwa na thamani mara mbili ya thamani ya mwanzo (bei uliyonunua).

Huhitaji kufanya haraka ya kuuza nyumba yako ambayo umeipata kwa sababu ya maarifa bora uliyonayo.

Unachohitaji ni mbinu sahihi za kuifanya nyumba yako ikuingizie kiasi kikubwa cha kodi kila wiki.

Muhimu; kupata fursa katika ardhi na nyumba, fuatilia kila siku kuhusu ardhi na nyumba. Usitafute muda sahihi katika eneo sahihi. Tafuta eneo sahihi wakati wote.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom