Uchambuzi Wa Kitabu; Getting Started In Real Estate Investing (Kuanza Kuwekeza Kwenye Majengo Ya Kupangisha Na Michael C Thomsett)

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Utangulizi.

Thomsett ameandika vitabu vingi kuhusu biashara na uwekezaji. Lakini kitabu kiitwacho Getting Started In Rental Income cha mwaka 2005 ndicho kitabu ninachokuletea uchambuzi wake leo.

Ameandika zaidi ya vitabu kumi miongoni mwa vitabu hivyo ni kuhusu uwekezaji kwa mtandao wa intaneti, uwekezaji kwenye hatifungani, uwekezaji kwenye hisa, kuwekeza mifuko ya pamoja, na jinsi ya kutawanya uwekezaji.

Kutoka kwenye kitabu cha GETTING STARTED IN RENTAL INCOME Thomsett ametushirikisha mambo ya msingi ya kuzingatia ili kuanza kumiliki majengo ya kipato chanya cha kila mwezi.

Thomsett anatushirikisha kuwa kodi ya nyumba inaweza kuingiza kiasi kikubwa cha kipato endelevu cha kila mwezi endapo utatumia mbinu bora.

Kitabu hiki kinajibu maswali mengi yakiwamo maswali yafuatayo;-

✓ Je unahitaji miaka mingapi kumiliki nyumba ili uweze kuuza kwa faida?.

✓ Je kutawanya uwekezaji katika majengo ni muhimu kiasi gani?.

✓ Je unaweza kutengeneza faida kwenye kununua na kuuza nyumba?.

✓ Je unaweza kupima kipato endelevu cha nyumba yako?.

✓ Kuna umuhimu gani wa kufahamu kipato endelevu cha nyumba yako?.

Thomsett ametushirikisha mambo mawili (2) ambayo ni muhimu sana kuzingatia katika uwekezaji wa ardhi na nyumba. Mambo hayo ni kama ifuatavyo;-

✓ Eneo ambapo nyumba ipo ni kiini cha thamani husika ya nyumba yako.

✓ Maarifa sahihi ni kiini cha kupata mafanikio makubwa sana ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Ukiwa na maarifa sahihi, lakini ukashindwa kuwekeza kwenye eneo lenye thamani kubwa huwezi kupata mafanikio makubwa sana kupitia uwekezaji huu.

Ukimiliki nyumba kwenye eneo lenye thamani kubwa lakini huna maarifa sahihi huwezi kupata mafanikio makubwa sana kwenye uwekezaji huu.

Sura Ya Kwanza.

Mbinu Ya Kizamani Ya Uwekezaji (Kumiliki Nyumba Kwa Miaka Mingi Na Kisha Kuuza).

Hapa mwekezaji humiliki nyumba kwa miaka mingi ili auze baada ya kupanda thamani. Kuna msemo usemao " soko huwazawadia wenye uvumilivu".

Thomsett ametushirikisha kuwa ukitaka kupata matunda ya soko lolote la ardhi na nyumba unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo;-

✓ Bei ya nyumba. Nunua nyumba kwa bei ya sasa na sio bei ya nyumba ya miaka ijayo.

✓ Eneo nyumba ilipo.

✓ Sifa za nyumba husika.

✓ Hali ya nyumba yako.

✓ Uhitaji wa aina ya nyumba unayomiliki. Hapa Thomsett anatushirikisha vitu vitatu kuhusu uhitaji; uhitaji wa mitaji fedha, uhitaji wa pango za kupangishwa na uhitaji wa ardhi na nyumba (huonekana kwenye bei za nyumba).

Faida Za Uwekezaji Wa Muda Mrefu.

Moja.

Ugumu wa kuuza na kununua viwanja na nyumba.

Hii hupelekea uwe na nidhamu ya mpango wako wa uwekezaji wa muda mrefu.

Nyumba au kiwanja unachotegemea leo kinaweza kuwa ni uwekezaji mzuri sana kwako.

Hisa huuzwa kwa haraka zaidi na kwa bei ya kueleweka ukilinganisha na uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Mbili.

Kupanda Bei.

Kwa kuangalia kwa muda mrefu, hisa na ardhi na majengo vyote viwili huongezeka bei au thamani kwa kuwiana.

Lakini, hisa hupanda na kushuka thamani ndani ya siku chache hadi miezi michache.

Hii hupelekea uwekezaji kwenye hisa kuwa hatari zaidi ukilinganisha na uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Kupanda na kushuka haraka kwa bei ya hisa, hufanya uwekezaji huu kuwa na hatari kubwa zaidi kuliko ardhi na majengo.

Tatu.

Kipato Endelevu (Rental income).

Wapangaji hulipia marejesho ya mkopo mzuri wa majengo. Hivyo unatakiwa kuchagua wapangaji bora sana.

Hii haipo kwenye uwekezaji katika hisa.

Nne.

Kuombea Mkopo Wa Majengo.

Unaweza kuomba mkopo wa kununulia nyumba hadi 100% ya bei (thamani) ya nyumba ya kupangisha unayotaka kununua.

Hii inawezekana hata kama hauna mtaji fedha wa kumudu kununua nyumba unayotaka.

Hii haiwezekani kwenye uwekezaji wa hisa.

Tano.

Bima ya majengo.

Uwekezaji kwenye ardhi na majengo humruhusu mmiliki kulipia bima ya majengo.

Bima hii ni kwa ajili kulipia fidia ya hasara kwenye thamani ya mtaji fedha uliowekeza kwenye nyumba husika.

Hii haiwezekani kwenye uwekezaji wa hisa. Hakuna utaratibu wa kulipia bima ya uwekezaji kwenye hisa.

Sita.

Faida ya kodi ya majengo serikalini.

Kodi ya majengo serikalini inaweza kuwa ndogo sana ukilinganisha na kodi ambayo mwenye nyumba hukusanya. Mara nyingi, kodi huwa chini kwa wawekezaji wengi wa majengo ya kupangisha.

Huwezi kupata punguzo la kodi serikalini kwenye uwekezaji wa hisa.

Saba.

Udhibiti binafsi wa uwekezaji (personal control).

Kwa kutumia maarifa na nguvu za mwenye nyumba inawezekana kuongeza thamani ya nyumba yake ndani ya miezi michache tu.

Inawezekana kuongeza thamani ya nyumba mara mbili ndani ya miezi 15 kwa kutumia maarifa yake na nguvu zake.

Haiwezekani kudhibiti hali ya soko la hisa kwa kutumia nguvu na maarifa ya mwekezaji.

Haiwezekani kuongeza thamani ya hisa kwa kutumia mbinu zako wewe mwekezaji.

Hasara Za Uwekezaji Wa Muda Mrefu Kwenye Ardhi Na Majengo.

Moja.

Udhibiti Binafsi.

Hii hupelekea kumiliki majengo yanayoingiza kiasi kidogo sana cha kodi ya mwezi.

Kwa sababu maarifa mabovu aliyonayo mwenye nyumba. Ili udhibiti binafsi uwe na manufaa kwenye uwekezaji wa ardhi na nyumba ni lazima mwekezaji au msimamizi awe na maarifa sahihi.

Pia, mwekezaji au msimamizi awe na uthubutu wa kutumia maarifa sahihi aliyonayo.

Mbili.

Ugumu Wa Kuuza Na Kununua.

Hii hupelekea kukosa mtaji fedha kwa kununulia nyumba au kiwanja kinachotengeneza kiasi kikubwa cha kipato endelevu ukilinganisha na nyumba uliyonayo sasa.

Mchambuzi,

Aliko Musa.

Mbobezi Wa Majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom