Jinsi ya kutambua habari na taarifa potofu Mtandaoni-Taarifa tam tam au yenye kutia hasira.-Vidokezo kutoka kwa Wataalamu wa Saikolojia

Nkaburu

JF-Expert Member
Mar 23, 2023
660
784
Je Ushawahi kukutana na Taarifa tamu tamu mtandaoni au taarifa ambazo zilikufanya ujisikie kutamani, hasira, chuki, au hofu?

Basi hauko peke yako.

According to Scientist, wataalamu wa saikolojia, watu wengi ni wahanga wa wa habari potofu mtandaoni.

Hatahivyo, cha muhimu ni kutokupanic au kunyamaza au ku share bila ya kufanya tathmini.

Ikiwa mada inazua hasira, chuki au hofu-hiyo wekea red flag kwanza, Usihiriki mara moja. Tafuta ukweli na undani wa Taarifa hiyo.

Ikiwa mada unakufanya usikie kucheka au inakufanya ujiskie vizuri, inaweza kuwa ni mbinu inayotumiwa na wapotoshaji ili kukufanya ushiriki maudhui yao.

Angalia vyanzo habari na ukweli kabla hujaanza kuhemeka na kuchangia. Yaani verify kabla hujashiriki. Hatimaye mada au ujumbe unathibitisha kike ambacho tayari unaamini, basi unaweza kushiriki bila ya kukagua ukweli.

Take a minute y'all na uangalie ukweli wake. Fact check before sharing. Check your sources.

Nimesukumwa baada ya Kuona na kusoma Taarifa Potofu zinazosambaa mtandaoni
 
Back
Top Bottom