Jinsi ya kuanzisha mazungumzo na mwanamke uliyekutana naye mara ya kwanza

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Mwanamke ambaye hamtakutana tena usipoongea naye kwa muda huo. Umemuona mwanamke na amekuvutia, sasa unajiuliza nini ukaongee naye ili muanze mazungumzo. Lengo lako lisiwe kupata namba. Lengo lako uweke ni kumfanya ajisikie hisia za raha kuwa na wewe.

Hivyo, hata akikupa namba inakua rahisi kukukumbuka. Usije ukachukua namba ya mwanamke bila lengo, mwambie mapema kuwa unataka mkutane hivyo akupe namba yake ili mpange kirahisi.

Pia ujue sio lazima uongee naye kwa lisaa ili akuelewe, hata dakika 2 zinatosha.

Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha anapata hisia za furaha kuongea nawe. Wanawake watu wa hisia sana, lakini kabla ya kwenda huko kote tambua jinsi ya kuanzisha mazungumzo.

Kuna njia mbili unaweza kutumia;

Njia ya kuzunguka
Njia hii unamfata mwanamke na kuongea naye kama vile rafiki, yaani vitu visivyomfanya akuhisi unamtaka haraka.

Mfano, unaweza kumuuliza “Dada samahani, saivi saa ngapi mana simu yangu imezima” au “Dada za saivi? Naulizia njia ya kwenda … ni wapi?” “Habari yako? … ivi iyo pochi umenunua wapi nataka nimnunulie mama kama hiyo.” Halafu unaongea naye kidogo kuhusu hicho ulichomuuliza.

Mfano, kuna umbali gani, nichukue tahadhari gani kuelekea huko, usafiri unaopatikana kirahisi ni upi?

Ukishaona anaongea nawe vizuri unaweza mwambia lengo lako la kumfata. Na badili mada na kuongea ukitakacho. Ongea naye mazungumzo ya kujuana, unafanya nini, unaishi wapi, una miaka mingapi kwenye kazi yako.

Uzuri wa njia hii, unatengeneza marafiki kirahisi na utapata namba nyingi na kirahisi pia.

Ubaya wa njia hii unaweza jikuta unajiweka kirafiki sana, na mwanamke hajui lengo lako. Mpaka uje kumuonesha mwanamke lengo lako ye anakua anakuchukulia rafiki na unaweza pata shida kumfanya awe mpenzi wako.

Njia ya moja kwa moja
Hii unamueleza kwanini umemfata bila kupepesa maneno wala macho. Utumie hii ukiwa unajiamini na unajua hutoyumbishwa na matokeo ya njia hii.

Mfano;
“Mambo? Umenivutia nimeona nije nikusalimie.”

“Umbo lako limenivutia nimeona nije niongee nawe.”

“Nakutaka mamy, umenivutia.”

“Nimekufata niongee nawe mana nakutaka.”

Kisha muulize jina lake, usisubiri akujibu hicho ulichomwambia.

Akikujibu mwambie nimefurahi kukuona, umpe na mkono ili azoee nyie kushikana mapema. Kisha ongea naye mazungumzo ya kujuana, unafanya nini, unaishi wapi, una miaka mingapi kwenye kazi yako. Pia umchombeze hapa na pale. Mfanye acheke.

Uzuri wa njia hii ni kwamba haina longolongo, mapema unajua kuwa huyu mwanamke pia amevutiwa nawe.

Ubaya wake ni kwamba utakataliwa haraka na kirahisi kama mwanamke hajavutiwa nawe na idadi ya wanawake watakao kukusikiliza ni wachache kulinganisha na njia ya kuzunguka.

Kumbuka wewe ndo uyaongoze mazungumzo. Yeye mwanamke hana sababu hata moja ya kuyaendesha mazungumzo sababu wewe ndiye uliyemfuata. Usikae kusubiri aweke neno au akujibu baadhi ya maswali, we jitahidi kusukuma mazungumzo mbele mpaka pale yatakapoishia.

Kupata namba ya mwanamke isiwe ndio ushindi, maana namba ni rahisi kupata. Ila jiwekee kuongea na mwanamke vile unavyotaka ndio ushindi.

Usiogope kukataliwa, chukulia kukataliwa ni kodi unayolipa kwa ajili ya wanaokukubali. Pia usiogope kukosea.

Share na wengine wapate kujifunza.
 
ila yote ni kupoteza muda tu mademu huwa tukienda kwa lengo la kutongoza huwa wanajua hata uzungukie wapi kwenye maongezi anajua tu kituo chako Cha mwisho Cha maongezi ni kipi, akikuona umekaa kiwaki anakupiga chenga nyingi balaa ila akikuelewa wala hakuna ugumu anakuonyesha shortcut chap tu
 
Kama una nia ya kutafuta mwanamke wa kuoa ndo unaweza kwenda kistaarabu ukamtongoza taratibu sabab unakua huna haraka nae mana lengo ni kumuoa ila hawa wa barabarn tu unamuita outing unampiga bia usiku mnene unaenda kula mzigo yan hat hujamwambia nakupenda
 
ila yote ni kupoteza muda tu mademu huwa tukienda kwa lengo la kutongoza huwa wanajua hata uzungukie wapi kwenye maongezi anajua tu kituo chako Cha mwisho Cha maongezi ni kipi, akikuona umekaa kiwaki anakupiga chenga nyingi balaa ila akikuelewa wala hakuna ugumu anakuonyesha shortcut chap tu
Thread imefungwa hapa mnaoendelea kupiga soga pigeni tu..
 
Labda mademu wa ulaya, Asia, na Urusi. Sio hawa wetu ambayo ukiwa na Crown ukavaa vizuri nguo zako za kariakoo na kupulizia perfume nzuri utashangaa yeye ndie anaomba namba yako.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Tatizo watu wanakariri maandiko ya Cosmopolitan, Vanity Fair, New York Magazine na machapisho mengine ya ughaibuni, wanayaweka kwenye Kiswahili au wanakariri point na kuandika Kiswahili, halafu wanafikiri dunia hiyo ndiyo hii yetu ya Mbagala Rangi Tatu!

Yani unasoma andiko limeandikwa Kiswahili lakini unaona kabisa limekaa ki ughaibuni ghaibuni hivi.
 
ila yote ni kupoteza muda tu mademu huwa tukienda kwa lengo la kutongoza huwa wanajua hata uzungukie wapi kwenye maongezi anajua tu kituo chako Cha mwisho Cha maongezi ni kipi, akikuona umekaa kiwaki anakupiga chenga nyingi balaa ila akikuelewa wala hakuna ugumu anakuonyesha shortcut chap tu
Ni kweli.
 
Pesaaaa pesaaa mbona hamna sehemu imetajwa kwenye uzi hebu acheni zenuu mnatutisha wajuba
 
Back
Top Bottom