Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu☺️☺️☺️
Zaid ni kwa sababu ya kuwa ni vigezo duni vya elimu kwa ubunge. Tanzania ya leo kujua kusoma na kuandika kiswahili tu siyo kigezo cha kumnya mtu awe mbunge. Kuna haja ya kupandisha viwango vya elimu ya mbunge kuwa angalau diploma au digrii ya kwanza
 
Shida yetu ni kwamba hata hatusikilizi tukachambua hayo wasomi wetu wamesema nini. Mwandishi wa habari akitufanyia muhtasari tu na kutafsiri anavyopenda yeye au anavyoona gazeti litauzika, basi ndiyo na sisi tunaimba na kukariri hivyo hivyo.

Ulisikiliza alivyozungumza Prof kuhusu umeme wa maji?

prof anadai umeme wa maji ni uwekezaji wa muda mrefu kurudisha faida.

prof kashasahau wala hakumbuki kwamba wateja wa umeme tanzania ni masikini,na umeme wanaoumudu ndio huu huu wa bei chee.

tatizo prof kaamua kuwa dalali wa umeme wa gas,anajaribu kusakafia hoja yake ikae kisomi zaidi,tumemshtukia.
 
Tanzania haina wasomi, ina watu walioenda shule kukariri, ndio maana watu wengi elimu zao haziwasaidii kabisa.

Mimi akija mtu akanambia amesoma, ana PhD, masters au degree halafu hana hela, au anaongea pumba ambazo hata mtu wa form 4 anaejielewa hawezi ongea.

Namuona mpumbavu tu. Hatuwezi kukaa kusikiliza hoja zako, hata kama ni pumba eti tukubali kisa umesoma. Mimi nina ka degree kamoja, ila Jana nilimuelewa sana Msukuma.
Safi Sana, watu wanajua usomi ni kujaza ma certificate.. Educate comes from lattin name " Educo"which means draw from within. Maarifa yoyote unayoyatoa ndani kutokana na elimu uliyoyapata, yakaleta impact kwako na kwa jamii hiyo ndio huitwa elimu.
 
Mijadala kama hii ya kipuuzi inaipoteza taifa. Ivi tangia lini Phd holder, Masters holders, Bachelor holder awe dhaifu mbele ya darasa la saba graduate ?
 
Mimi sijaona kama wamedharauliwa, ninachoona ni kwamba tumekumbushwa kama tumeamua kutafuta makaratasi (vyeti) basi ya reflect kwenye mambo tunayoyafanya.

Sio unataka cheo sababu una makaratasi wakati matumizi ya kilichokua kwenye makaratasi huyajui na wala mahitaji ya mazingira huyajui
Mimi sijaelewa,kwani Muhongo na Assad ni wapi wametumia elimu yao vibaya?
 
Safi Sana, watu wanajua usomi ni kujaza ma certificate.. Educate comes from lattin name " Educo"which means draw from within. Maarifa yoyote unayoyatoa ndani kutokana na elimu uliyoyapata, yakaleta impact kwako na kwa jamii hiyo ndio huitwa elimu.
Kwamba wewe umefuatilia Kazi za Prof. Muhongo na umeona Elimu yake haina manufaa kwa jamii?
 
Usomi au elimu ndani ya mazingira yanayokutaka utende yatakavyo na si kwa ubunifu wako, bado tutawaona wenye elimu na wasomi hawana maana.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Binafsi hao wasomi wanastahili kufanyiwa hayo wanayofanyiwa,hawana msaada kwa taifa,ni hasara tupu,wasomi ndio wanaofunga mikataba ya kimangungo,ndio wanaoitia Shimon nchi hii,
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu☺️☺️☺️
Tatizo la hao ni sawa na hao wasomi wanasiasa...Wanatoa hoja si kwasababu taaluma inawaelekeza bali kwakua na wao wanataka ku defend interests zao ikiwamo kujificha kwenye koti la usomi kulipiza visasi...Hii ni common sense haihitaji kwenda shule....But two wrongs never make a right....Wasomi tumeanza kujidhalilisha wenyewe, ila wenzetu wameupaka rangi udhalilishaji huo...
 
Hivi kama huna elimu utafanya upasuaji? utajenga madaraja? kama umeishia darasa la saba sio tatizo
Lakini je ukiamua kufanya upasuaji hata sehemu ambayo haistahili hivyo ili tu uoneshe umahiri wako, tukufanyeje?

Tuongozwe na ethics...Unapokuwa na conflict of interests hutakiwi kuhusika na hilo jambo hata kama wewe ni bingwa katika hiyo field...Hao wasomi wote walikuwa na conflict of interest na wamefanya kitu ambacho ni unethical!
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu
Wewe pia sio msomi bila shaka.. kama ni msomi usingesema hilo bali ungewashangaa wasomi wenzako kama kina Muhongo kuongea kwa viwango duni kama vile.
Huwezi sema uzalishaji umeme kwa njia ya maji umepitwa na wakati..wakati nchi kama norway inatumia maji kwa umeme kwa asilimia kubwa sana na nchi zingine bado zinapambana kujenga mabwawa ya maji.
Alichoomgea yule prof uchwara wa geology hakiendani na taaluma yake.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
zima kifanywe kwanza na wajiolojia na alikuwa anaeleza kwamba badala ya kuelekeza nguvu zote kwenye umeme wa maji ni wakati sasa wa kuangalia pia uzalishaji wa umeme kupitia vyanzo vingine ni kwasababu ameshaoversee impact zake akatoa mfano tukiwekeza kwenye wind, gas, geothermal, coal na nyinginezo ambazo ni very essential kwa ulimwengu wa sasa je hapo hajatumia usomi wake? tumefuatilia ni consultancy ngapi anazifanya kwa taifa hili za kijiolojia na hata tumseme hakuna anachofanya kama msomi? na je hawa wasomi waliopo bungeni tukisema waondoke bungeni tuwaache wakina msukuma tu unadhani tutakuwa na nchi ya aina gani? Mtu anapayuka wasomi wanaliletea taifa hasara je tujiulize kuna waziri au naibu asiye msomi? kuna makatibu wakuu na wasaidizi wasio wasomi? na je project zote zinazoendelea na kujengwa zinafanywa na wasio wasomi? Hayo makampuni wanayoyaleta kufanya project kubwa na wanarecruit wasomi wakubwa wa hapa nchini ni wajinga? Tulipofikia kama taifa ni pabaya kuanza kudharau wasomi. Inasikitisha sana
 
PHD ya kukariri duu. Hii Elimu imefikia hukuu. ila kujua utamu wa ngoma ingia uchezee
 
sio bungeni tu hata huku mtaani jiran darasa la 7 anamali mara 100 ya profesa mtaa huo huo, huu sio udhalilishaji?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mijadala kama hii ya kipuuzi inaipoteza taifa. Ivi tangia lini Phd holder, Masters holders, Bachelor holder awe dhaifu mbele ya darasa la saba graduate ?
Mbona wasomi chama cha ccm wamonyesha udhaifu mkubwa mjengoni.
 
Kuna kitu gani cha maana wanachoweza kuongea zaidi ya kupamba,kushambulia na kutukana.
Wanaweza kusoma ripoti ya CAG na kuilewa wale?
Wanaweza kuzichambua sheria kandamizi?
Wanaweza kuilewa bajeti wale na kueleza mapangufu?
Wanaweza kujadili uchumi ktk global world wale.
CCM ifike mahala ituondolee wabunge darasa la saba, hawana faida yoyote zaidi ya kusaini posho.
Taifa linapata hasara tu kendelea kukumbatia watu wenye uelewa mdogo wa dunia ya utandawazi.
Prof Muhongo hajachambua kiundani hoja yake pengine ana mengi ya kueleza kama atapewa nafasi,hawezi kuwa mjinga kiasi hicho yule ni mtaalamu wa nishati kwa hio tusibeze tu af mbele ya safari tukaje kugundua ukweli.
Kina kibajaji wangekuja na data zinazopinga kauli ya muhongo au wangeomba data kwa muhongo ili alishawishi bunge kwa evidence.
Inawezekana Muhongo anazo tafiti,sisi wengine tunakurupuka tu kwa mihemko.
Ukimpinga Muhongo umpinge kwa data sio maneno matupu.
Umeongea ukweli kabisa alipoongea Prof Assad kuwa bunge ni dhaifu hakukosea na hakupewa muda aeleze ni kwanini bali alishambuliwa na kuondolewa na hata Muhongo kila hoja ya kitaalamu anayotoa anapingwa na kushambuliwa bila hata kuichambua hoja hiyo kwa undani Mwalimu nyerere alifikiria mbali sana aliposema adui yetu mkubwa ni UJINGA
 
kwasasasa wasomi ndiyo wapinzani
1618556813138.png
 
Haya ndio madhara ya wataalamu na wasomi wetu kukimbilia siasa na kuacha taaluma zao. Ona sasa wanavyozodoana na wanasiasa wasio wasomi. Wangebaki kwenye taaluma zao vyuoni na kwengineko na kuwaacha wanasiasa katika siasa yasingewakuta haya😀
Siasa pia ni taaluma tunatakiwa kujua kwanza nini maana ya siasa ndipo tuendelee na mengine.
 
Back
Top Bottom