Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Umeona sasa....kijana kama huyo huwez kumfananisha na mtu alosoma miaka yake mitatu ya ubabaishaji mwingi na chabo za kutosha

Kitu kingine watu wanachokosea au kusahau mbali na elimu kuna watu wanazaliwa talented iwe kwenye siasa au maeneo mengine yoyote yale, so unapokuta mtu yuko talented anaweza kuwork ethnically and successfully kuliko yulr ambae alipata GPA yake ya upper second tena ilojaa mazonge na harakati za ajabu..Mifumo yetu ya elimu sio rafiki kwenye soko la ushindani wa ajira,
Kweli kabisa. Pia kwenye ulimwengu wa sasa kuna kitu kinaitwa ''certification'' unamkuta mtu ni injinia wa civil au mechanical
lakini ukimpeleka kwenye kuomba kazi kwenye makampuni ya kimataifa,unaambiwa kama hajawa certified na mamalaka zinazotambulika hawaweza kumuajiri kwa sababu bima zao zinataka watu waliothibitishwa,unamkuta mtu hata kama ni mzuri kiasi gani anakosa kazi sababu ya kutothibitishwa.
Ni vizuri vyuo vikongwe kama UDSM vijikite kufanya mabo makubwa kama hayo ili wasomi wetu wawe na soko la ndani na nje ya nchi vinginevyo kupigana vikumbo na sisi la saba hakutaisha,maana mchango wao ktk jamii kama wasomi tusipouona usitegemee heshima.
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu
Ukitembea barabarani,mbwa wakaanza kukubwekea,usikimbizane Wala kuwafokea,fanya kama uwaoni
 
Back
Top Bottom