Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Eti msukuma na lusinde wawe hoja kisa tu wameishia darasa la saba na wao wanajiona ni muhimu.

Hivi wanaelewa hata sera ya Elimu kweli kuwa serikali inapigana walau mtanzania awe na elimu gani.

Hawa ni kuwatungia sheria cha kigezo cha elimu ili watoke tu humo ndani. Hata kama kuna wasomi ambao sio wazalendo ndiyo ilivyo kwao wasio na shule.
 
Kuna kitu gani cha maana wanachoweza kuongea zaidi ya kupamba,kushambulia na kutukana.
Wanaweza kusoma ripoti ya CAG na kuilewa wale?
Wanaweza kuzichambua sheria kandamizi?
Wanaweza kuilewa bajeti wale na kueleza mapangufu?
Wanaweza kujadili uchumi ktk global world wale.
CCM ifike mahala ituondolee wabunge darasa la saba, hawana faida yoyote zaidi ya kusaini posho.
Taifa linapata hasara tu kendelea kukumbatia watu wenye uelewa mdogo wa dunia ya utandawazi.
Prof Muhongo hajachambua kiundani hoja yake pengine ana mengi ya kueleza kama atapewa nafasi,hawezi kuwa mjinga kiasi hicho yule ni mtaalamu wa nishati kwa hio tusibeze tu af mbele ya safari tukaje kugundua ukweli.
Kina kibajaji wangekuja na data zinazopinga kauli ya muhongo au wangeomba data kwa muhongo ili alishawishi bunge kwa evidence.
Inawezekana Muhongo anazo tafiti,sisi wengine tunakurupuka tu kwa mihemko.
Ukimpinga Muhongo umpinge kwa data sio maneno matupu.
Hujasikiliza vizuri hoza za msukuma,kwa ufupi Huyu pro hamna kitu alikuwa waziri alifanya nini cha maana,hamna kitu usitetee udhaifu.
 
Tupe evidence kuwa msomi ni mahususi kufanya kazi vyuoni tu?
Wasomi hawafungwi na usomi wao, wanaweza kufanya kazi popote bila kuvunja sheria.
Hivi wasomi wote Tanzania wakafanye kazi vyuoni, hivyo vyuo vinazo hizo nafasi?
..Mkuu nashukuru kwa angalizo lako..siku ushahidi kuwa wasomi ni lazima wafanye kazi vyuoni tu..lengo langu lilikuwa ni kuonesha kuwa kwenye siasa hasa hizi za Tanzania ambazo zimejijenga katika cheap popularity...Kwa wasomi wa kweli haziwafai....ila kama ni kwa ajili ya kuchumia tumbo kama Prof fulani na yule Prof fulani....sawa!
 
Hawadhalilishwi wanajidhalilisha wenyewe kama huyu pro alikuwa waziri wa nishati ,moja kwa moja anaingia kwenye baraza la mawaziri bila kizuizi,hizi hoja anazokuja nazo sasa huoni kama ni hasira za kukosa uwaziri!?
 
Kwahiyo kina Kibajaj na Musukuma kasheku wanafuata nyayo za kiongozi wao?
Wewe jamaa nimekufutilia mda mrefu sana nimegundua wewe jamaa huna bifu na Hayati JPM Bali una chuki binafsi na watu wa kanda ya ziwa hasa Wasukuma na Waha. Kuna Uzi ulinifanya nikuone Boya kabisa. Ulimwita Makamu wa Rais Mpango kwamba ni Mrundi na ukamdharirisha Zitto Kabwe kwamba arudi Burundi kisa tu wewe unatokea Nyanda za Kaskazini. Bure kabisa.
 
Bunge la.majungu na umbea ndio limeasisiwa na Jiwe kupitia kibaraka Supika. Hili ndilo bunge wanalojisifia CCM kushinda kwa kishindo
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu

Sasa mkuu si wamebaki wenyewe mle ndani/CHAMA kimoja wacha wabaguane hivyoWASOMI Vs KANJANJA....Mitano tena tumechelewa sana....
 
hida ipo kwenye vigezo vya kikatiaba vinavyompa raia sifa za kugombea ubunge, kwamba ni kujua kusoma na kuandika, hapa ndipo tulipokamatwa!
Bila shaka. wale wazee wa KK tatu wanapitia hapa. Dunia hii ya smart economy haitaki tena wabunge wa darasa la saba.

Kitu kingine kinachonisikitisha ni kitendo cha nchi hii yenye masikini milioni 14 waliotopea tunadharau elimu mapema hii. Ushenzi uliopitiliza.

Wachumi na wadau wa maendeleo wanasema elimu ina nafasi ya asilimia 70 kumwondoa mtu katika umaskini. Sisis tunaidharau daaah . . . Halafu bunge letu lina wabunge dizaini ya Msukuma.

Maendeleo tutayasikia kwenye bomba
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu☺️☺️☺️

Mkubwa ukiangalia vigezo vya kuwa mbunge utaona kuwa ni vya chini sana. Hili ndio tatizo la kwanza, na hili si kosa la mwenye elimu kunniga kwenye ulingo wa kujibizana na wasio na elimu.

Lakini la pili ni kuwa, kwa mfumo wetu wa sasa siasa inalipa kuliko elimu. Ndio maana utaona maprofesa na madokta wanaacha taaluma zao na kazi zao wanajiingiza kwenye siasa.

Kwenye hili ntakuwa wa kwanza kuwatetea Lusinde na Msukuma, ni sheria zeste na kanuni zetu ndio zimetufikisha huko. Kigezo cha kupa mbunge ni miaka 18, élimu ya msingi, ugombee kupitia chama, au uteuliwe.
 
Mimi binafsi namuelewa sana Musukuma kwa sababu anajua kujenga hoja yake in a simple way ikaeleweka. Ila sasa hao wanaojikuta maprofesa au madokta wakati mwingine speech zao huwa zinaniacha na mshangao sana. Na mara nyingi huwa najiuliza ni kwamba hawaelewi kweli au ni kwamba wana mtu wanayemtumikia hadi wanakuwa wanautweza weledi wao kiasi hicho?.

Hao maprofesa wanashindwa kujibu hoja kwa hoja wanaishia kulalama ati wamedhalilishwa😃😃😃

Wasomi walioelimika kamwe hawawezi dhalilishwa kwa hoja.....
Ila wanaojiita wasomi sababu ya makaratasi huku hoja zikiwashinda wanajidhalilisha wenyewe.
 
Hao maprofesa wanashindwa kujibu hoja kwa hoja wanaishia kulalama ati wamedhalilishwa

Wasomi walioelimika kamwe hawawezi dhalilishwa kwa hoja.....
Ila wanaojiita wasomi sababu ya makaratasi huku hoja zikiwashinda wanajidhalilisha wenyewe.
duh
 
Mkubwa ukiangalia vigezo vya kuwa mbunge utaona kuwa ni vya chini sana. Hili ndio tatizo la kwanza, na hili si kosa la mwenye elimu kunniga kwenye ulingo wa kujibizana na wasio na elimu.

Lakini la pili ni kuwa, kwa mfumo wetu wa sasa siasa inalipa kuliko elimu. Ndio maana utaona maprofesa na madokta wanaacha taaluma zao na kazi zao wanajiingiza kwenye siasa.

Kwenye hili ntakuwa wa kwanza kuwatetea Lusinde na Msukuma, ni sheria zeste na kanuni zetu ndio zimetufikisha huko. Kigezo cha kupa mbunge ni miaka 18, élimu ya msingi, ugombee kupitia chama, au uteuliwe.
Nasikia darasa la 7 hupita kiujanja,umafia ulozi,rushwa nk.mbunge wa Rungwe alienguliwa baada ya kuhisiwa anatoa rushwa ni la 7.
Lusinde na msukuma huwa hawana hoja na uchambuzi bali kushambulia watu.
Kuna makabila bado yanachagua wabunge darasa la saba.
 
Back
Top Bottom