Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Elimu ya kimapokea ni kirusi, inawezekana ni shambulio la kifikra dhidi ya jamii ya weusi

Musukuma na Lusinde wana akili kuzidi Muhongo na Assad, na wana akili kweli kwa maana ya uwezo wa kukabiliana na mazingira.

Muhongo na Assad ukiwapora makaratasi ndio basi tena

Nawashauri maprofesa hawa wajikite kufanya kazi za kitaaluma(Walizomudu kukariri) huku kwenye siasa wanajiaibisha
 
hivi kama huna elimu utafanya upasuaji? utajenga madaraja? kama umeishia darasa la saba sio tatizo

Jiulize kwanza kama wote wanaofanya upasuaji na kujenga madaraja tangu enzi za Adam, Musa na manabii wengine wote walikua na makaratasi yanaitwa diploma, degree, masters, PhD???

Halafu uelewele maana ya elimu
 
Tatizo watu mnachanganya siasa na usomi wa mtu, wale ni wanasiasa na ni wasomi pia, msomi anaeweza simama akaongea pumba lakini nafsi inamsuta kabisa ila kwasababu inambidi asimame na aongee hivyo basi watu kumuona kama mjinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The fact kwamba hao wasomi walidharauliwa na wasio na elimu na wao wakakaa kimya mpaka hii post ikaja hapa, kunaleta mashaka na uwezo wao wa kutumia elimu Yao..na kibaya zaidi wameshindwa kutumia elimu Yao kuji defend against ya attacks za standard seven leavers.

SASA wataweza kutetea nchi pale mikataba iliyoandikwa Kwa ustadi Mkubwa na wasomi wabobezi wanaotumia small prints kuibia wajinga punde itakapoletwa kujadiliwa?

Yanayoendelea hapa nchini Kwa SASA inabidi yawe documented vizuri ili baadae vizazi vijavyo vijifunze namna ya kutokuwa wajinga.
 
The fact kwamba hao wasomi walidharauliwa na wasio na elimu na wao wakakaa kimya mpaka hii post ikaja hapa, kunaleta mashaka na uwezo wao wa kutumia elimu Yao...
Mimi sijaona kama wamedharauliwa, ninachoona ni kwamba tumekumbushwa kama tumeamua kutafuta makaratasi (vyeti) basi ya reflect kwenye mambo tunayoyafanya.

Sio unataka cheo sababu una makaratasi wakati matumizi ya kilichokua kwenye makaratasi huyajui na wala mahitaji ya mazingira huyajui
 
Wameyataka wenyewe kama mtu ana uwezo wa kwenda kufundisha chuo kikuu chochote Duniani anawezaje kuwa kapu moja na Lusinde na Musukuma, wangekuwa wasomi kweli wangeachana na siasa uchwara wangejikita kwenye research consultancy na kufundisha huko duniani , wengi wao ni wachumia tumbo tu, mnakumbuka kuna mmpoja alitumbuliwa ukuu wa mkoa wa Morogoro alitoa povu kuwa kamalizwa sijui hana pakwenda mara kakosa sijui nini
 
Jiulize kwanza kama wote wanaofanya upasuaji na kujenga madaraja tangu enzi za Adam, Musa na manabii wengine wote walikua na makaratasi yanaitwa diploma, degree, masters, PhD???

Halafu uelewele maana ya elimu
Duuuu, nimekuogopa kama unafikia hatua ya kudharau elimu na mapokeo yake
 
Tanzania haina wasomi, ina watu walioenda shule kukariri,ndomaana watu wengi elimu zao haziwasaidii kabisa.

Mimi akija mtu akanambia amesoma, ana PhD, masters au degree alafu hana hela, au anaongea pumba ambazo hata mtu wa form 4 anaejielewa hawezi ongea... Namuona mpumbavu tu.Hatuwezi kukaa kusikiliza hoja zako,hata kama ni pumba eti tukubali kisa umesoma.Mimi nina ka degree kamoja,ila Jana nilimuelewa sana Msukuma.
Mkuu hata uko nchi zilizoendelea kuwa na PhD and Master degree sio kigezo cha kuwa na pesa..la kwa hili la kushindwa kuongea au kuongea pumba nakubalina nawe
 
Jiulize kwanza kama wote wanaofanya upasuaji na kujenga madaraja tangu enzi za Adam, Musa na manabii wengine wote walikua na makaratasi yanaitwa diploma, degree, masters, PhD???

Halafu uelewele maana ya elimu
Nenda pale MOI kamtafute bingwa wa upasuaji ambaye hajasoma na hana hivyo vyeti unavyo vidharau na kuvikebei.

Katafute kuanzia mlango nambari 1-10 madaktari woote ni maprofesa na kweli kwa kutumia elimu yao wanafanya kazi ya uhakika.

Haiingii akilini eti leo hii kwa ushabiki wa mavyama na itikadi ukufanye uidharau elimu na kuwabeza waliosoma.
 
tatizo watu mnachanganya siasa na usomi wa mtu, wale ni wanasiasa na ni wasomi pia, msomi anaeweza simama akaongea pumba lakini nafsi inamsuta kabisa ila kwasababu inambidi asimame na aongee hivyo basi watu kumuona kama mjinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lkn tusifikie kuwadharau waliosoma.
 
Huwa nacheka sana ninapowasikiliza wasomi wa Tanzania hasa wale PhD holder!!....ujinga mtupu!!
Sio wote mkuu...wale waliojitoa akili na kuendekeza matumbo yao na kushadidia siasa uchwara ndio wanaowaponza wengine hat hizo PhD zisionekane za maana....wenye akili zinazofanafa na PhD zao bado wako baadhi hasa huko vyuoni!
 
The fact kwamba hao wasomi walidharauliwa na wasio na elimu na wao wakakaa kimya mpaka hii post ikaja hapa, kunaleta mashaka na uwezo wao wa kutumia elimu Yao..na kibaya zaidi wameshindwa kutumia elimu Yao kuji defend against ya attacks za standard seven leavers..SASA wataweza kutetea nchi pale mikataba iliyoandikwa Kwa ustadi Mkubwa na wasomi wabobezi wanaotumia small prints kuibia wajinga punde itakapoletwa kujadiliwa?!..Yanayoendelea hapa nchini Kwa SASA inabidi yawe documented vizuri ili baadae vizazi vijavyo vijifunze namna ya kutokuwa wajinga.
Unaelewa sana mkuu, kuna dilemma of professionalism
 
Nenda pale MOI kamtafute bingwa wa upasuaji ambaye hajasoma na hana hivyo vyeti unavyo vidharau na kuvikebei.

Katafute kuanzia mlango nambari 1-10 madaktari woote ni maprofesa na kweli kwa kutumia elimu yao wanafanya kazi ya uhakika.

Haiingii akilini eti leo hii kwa ushabiki wa mavyama na itikadi ukufanye uidharau elimu na kuwabeza waliosoma.
Tatizo hawa wasomi wamechagua kutumikia taifa kule ambako elimu zao hazistahili....wangebaki tu vyuoni...huku kwenye siasa kunawafanya washindwe kufikiri kwa level zao....
 
..Tatizo hawa wasomi wamechagua kutumikia taifa kule ambako elimu zao hazistahili....wangebaki tu vyuoni...huku kwenye siasa kunawafanya washindwe kufikiri kwa level zao....
Sipati picha Bashiru atakuwa anajisikiaje
 
Back
Top Bottom