Kuna kijana mmoja mdogo kabisa (miaka 24-26) Mitaa ya Bugando hospital, ni fundi mzuri wa umeme wa magari, yaani habahatishi kazi zake. Baada ya kutembelea sana maeneo yake ya kazi, nilijaribu kumfanya rafiki yangu, sasa kuna siku nikamuuliza alisomea wapi huo ufundi, akanambia yeye ameishia darasa la 4,ila maisha yake yote amekulia garage, nilishangaa sana.
Sasa eti huyo dogo uje umringanishe na mtu alisoma mpaka form six, Kisha akajifunza ufundi wa magari kwa miaka 3 na kufanya field ya miezi mitatu

?
Ndomaana wazungu hawataki kabisa habari ya makaratasi, wao wanaangalia fani na uzoefu wako katika fani husika, cheti ni kigezo cha mwisho kabisa.