Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Dol

Member
Mar 24, 2021
58
115
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu☺️☺️☺️
 
Tanzania haina wasomi, ina watu walioenda shule kukariri, ndio maana watu wengi elimu zao haziwasaidii kabisa.

Mimi akija mtu akanambia amesoma, ana PhD, masters au degree halafu hana hela, au anaongea pumba ambazo hata mtu wa form 4 anaejielewa hawezi ongea.

Namuona mpumbavu tu. Hatuwezi kukaa kusikiliza hoja zako, hata kama ni pumba eti tukubali kisa umesoma. Mimi nina ka degree kamoja, ila Jana nilimuelewa sana Msukuma.
 
Tutakapofikia hatua ya kuweza kujua maana halisi ya elimu

Tutafikia hatua ya kuweza kuheshimu na kuwaheshimu wote wenye elimu isiyo rasmi na elimu rasmi

Binafsi nathamini elimu rasmi kama ilivyo kwa ile isiyo rasmi lakini naamini kwamba elimu rasmi haimsaidii mtu kama hawezi kuitumia kuongeza thamani na ubora wa mazingira yanayotuzunguka

Hayo makaratasi yanaoyoitwa diploma, degree, masters, PhD yasitudanganye tukajihisi bora zaidi na kuanza kupandisha mabega juuuu sababu kuna wasiokua nayo na pia wanafanya vitu vikubwa tu
 
...
Hayo makaratasi yanaoyoitwa diploma, degree, masters, PhD yasitudanganye tukajihisi bora zaidi na kuanza kupandisha mabega juuuuu sababu kuna wasiokua nayo na pia wanafanya vitu vikubwa tuu
Unamfahamu anayeshikilia rekodi ya kupandisha mabega juu Tanzania kisa PhD? Sio tu aliwatukana wale watoto live bali aliwatimua kabisa! Eti vilaza!
 
... unamfahamu anayeshikilia rekodi ya kupandisha mabega juu Tanzania kisa PhD? Sio tu aliwatukana wale watoto live bali aliwatimua kabisa! Eti vilaza!

Kama unamuongelea JPM ujue tuu ameitendea haki kwenye miaka yake akiwa mwalimu, miaka 20 ya Uwaziri na sita ya urais.
Hajawahikuitumia PhD kama unavyoitumia wewe kwenye mitandao ilihali hakuna lolote ulilowahi kuifanyia jamii yako

Halafu acha kumlinganisha hayati John Pombe Joseph Magufuli na vitu vya ajabu ajabu

dudus elimika






Rest well our hero President John Pombe Joseph Magufuli
 
Nchi za watu elimu kubwa ya mtu inajipambanua kwa kile anakitoa kwa jamii inayomzunguka kukabiliana na changamoto mbali mbali.

Huku Afrika elimu za watu ni vyeti vingi acha wayaoge tu.
Prof mzima anashauri nchi iachane na uzalishaji wa nishati ya umeme kwa njia ya maji.
 
Shida ipo kwenye vigezo vya kikatiaba vinavyompa raia sifa za kugombea ubunge, kwamba ni kujua kusoma na kuandika, hapa ndipo tulipokamatwa!

Katiba yetu ilishapitwa wakati, hivi sasa hata uteuzi wa baraza la mawaziri ambapo kigezo cha kwanza kuwa mbunge utaona karibu mawaziri wote ni wasomi, Kuna haja gani ya kuruhusu watu wa darasa la saba kuingia kugombea ubunge?
 
Back
Top Bottom