Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Jinsi wasomi wanavyodhalilishwa Bungeni

Kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi
Mlianza na moto wa kulazimisha gang lenu liheshimiwe kisa mnatoka kanda yenye watu wengi lkn mkapigwa spana za kutosha sasa naona mmenywea kama mchicha kwenye maji ya moto.

Tuliza kiuno bibieee
Moto ni uleule

Prof Assad na Muhongo ni wajinga sana ,ndiyo wanaosababisha elimu kupuuzwa.

Ni bora usikilize mchango wa Kishimba utajifunza kitu kipya kuliko hao wapuuzi wawili.
Tumeshuka kiasi cha kumfananisha Prof. Assad na msukuma/kibajaj!! Yote hiyo kwa ufisadi na ujinga wa Ndugai anayeleta hata ushabiki wa mpira ndani ya bunge!! Fanya ushabiki wa mpira wakati unakunywa chai nje ya bunge na sio ndani ya bunge wee mgogo! Unanajisi chamber kwa utani wako wa kijinga.
 
Tanzania haina wasomi, ina watu walioenda shule kukariri,ndomaana watu wengi elimu zao haziwasaidii kabisa.

Mimi akija mtu akanambia amesoma, ana PhD, masters au degree alafu hana hela, au anaongea pumba ambazo hata mtu wa form 4 anaejielewa hawezi ongea.

Namuona mpumbavu tu.Hatuwezi kukaa kusikiliza hoja zako,hata kama ni pumba eti tukubali kisa umesoma.Mimi nina ka degree kamoja,ila Jana nilimuelewa sana Msukuma.
chuki nyingine hizi. Mwenye degree siyo msomi???
Wewe hujasoma bana tusibabaishane hapa.
Hawa wabunge wa darasa la saba wanaakili kuliko hao unaowaita wasomi
chuki hazitaisha bongo!! Sasa ndo ninaona kwa nini Mzungu alibagua miafrica kulingana na rangi zao. elimu zao. Mzungu angejichanganya tu nanyie weusi angekosa thamani.
Yale majamaa Makoloni sijui Makaburu yana akili sana.sasa tunayaona hayo.
Uzunguni Mswahili alikuwa hakanyagi.

Onyo Mkisoma kaeni huko huko ulaya kwa wasomi wenzenu msirudi.
Mkibisha njooni mdharirike na kundi la wajinga.km hivi
Hawa wabunge wa darasa la saba wanaakili kuliko hao unaowaita wasomi
jiwe ameharibu sana
 
Shida ipo kwenye vigezo vya kikatiaba vinavyompa raia sifa za kugombea ubunge, kwamba ni kujua kusoma na kuandika, hapa ndipo tulipokamatwa!

Katiba yetu ilishapitwa wakati, hivi sasa hata uteuzi wa baraza la mawaziri ambapo kigezo cha kwanza kuwa mbunge utaona karibu mawaziri wote ni wasomi, Kuna haja gani ya kuruhusu watu wa darasa la saba kuingia kugombea ubunge?
Huwezi kujenga hoja zinazohitaji kutafakari ukiwa katikati ya kundi kubwa la wajinga au average mind kama wengi wa lio huko bungeni

Muhongo alihoji swali zuri tuu je umeme utashuka bei baada ya bwawa kukamilika ? Na je utakuwa kama huduma au kama biashara? Haya maswali yakijibiwa italeta uhalali wa kuendelea na mradi au kutoendelea nao given its cost implications.

Kuna jinga lingine ni Liaskofu la huko Songea linasema ndege sio kwa biashara ni kwa huduma kwa hiyo serikali iendelee kununua nyingi zaidi.Watu dizaini hii wanaishi kwa sadaka ambazo ni jasho la wengine lakini anaongea pumba
 
Hayo masalia ya Magu ndio yalikuwa yamewaaminisha watu kwamba Kazi ya serikali ni Kazi ya mtu binafsi huku yakiiba pesa

Bora Mungu kaondoa jitu lilioanza kujigeuza Mungu mtu na kuabudiwa na wajinga walio wengi
 
hivi kama huna elimu utafanya upasuaji? utajenga madaraja? kama umeishia darasa la saba sio tatizo
Hata hilo bwawa sijui wwnaojenga ni hao kina Musukuma et all

Most of them ni wajinga na mburura wa kuzidi wanadhani the way Dunia inaenda hadi wao wanafanya tubiashara wanapata pesa basi wanajua hali imekuja tuu by nature.

Pia lengo la elimu ni kutoa service kwa watu hususani hao vilaza na sio kutafuta pesa,elimu sio business enterprise kwamba utagain profit
 
Elimu ya kimapokea ni kirusi, inawezekana ni shambulio la kifikra dhidi ya jamii ya weusi

Musukuma na Lusinde wana akili kuzidi Muhongo na Assad, na wana akili kweli kwa maana ya uwezo wa kukabiliana na mazingira.

Muhongo na Assad ukiwapora makaratasi ndio basi tena

Nawashauri maprofesa hawa wajikite kufanya kazi za kitaaluma(Walizomudu kukariri) huku kwenye siasa wanajiaibisha
Mbona hatuwaoni wakishiriki kujenga bwawa au hospital au huko wizarani kupanga mahesabu ya uchumi wa nchi?
 
Jiulize kwanza kama wote wanaofanya upasuaji na kujenga madaraja tangu enzi za Adam, Musa na manabii wengine wote walikua na makaratasi yanaitwa diploma, degree, masters, PhD???

Halafu uelewele maana ya elimu
Kumbe walikuwa na nini? Jibu swali mbona hatuwaoni huko alikosema mdau wakionyesha hiyo elimu yao?
 
Msukuma na kibajaji wanajua kujenga hoja ila tu ni mpangilio umewashinda . Wakati wa kuongea wao wanakaa kimya na wakati wa kukaa kimya wao wanaongea . Kipaji cha kuzaliwa wanacho ila wangepalilia na elimu ya darasani .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Darasa la saba wengi wameingia bungeni kwa rushwa,fitna, majungu,ushirikina na pesa.
Watanzania wengi ni darasa la saba hivyo hawana hasara kuchagua darasa la saba.
CCM inaongozwa na darasa la saba katika ngazi za mashina na hao ndio chanza cha kupeleka wabunge darasa la saba.
Kuwaondoa darasa la 7 bungeni inabidi uwaondoe wajumbe darasa la saba, wengi wao ni vingunge huko kwenye matawi ole wako ukagombee hio nafasi ya ujumbe watakutoa roho peupe .
Mammb Yatabadirjuka yenyewe taratibu, ila tunasafari ndefu sana.
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu☺️☺️☺️
Sijui unataka kumaanisha nini kwani hata wasomi wenyewe unaowaongelea wanajishuku kuwa hawajui kitu.

Bila shaka utamkumbuka mmoja ambaye ni Profesa a.k.a Profesa Majalalani ambaye alisimama kumshukuru Rais "kumwokota" toka JALALANI (UDSM) na kumleta kwenye siasa. Msukuma na Lusinde hawajakosea kitu, wako sahihi.
 
Hivi kwani hawa wasomi waliopo bungeni wamelisaidia nini taifa. Hasa hao wanaoshambuliwa? Wanachoelezwa ni kuwa watumie usomi wao kwenye masuala yenye tija kwa taifa na sio kusababisha kudhalilika
 
Kwa hiyo Wewe unampinga mheshimiwa Mwinyi, Una shauri kichaa akichukua nguo zako akakimbia nazo, na wewe umkimbize tu, kengele la kanisa katokiki likinging’inia?
Nadhani hujanielewa..Mimi nasema ili kina lusinde na msukuma waache kejeli zao Kwa wasomi inabidi hao wasomi wa step up na kuonesha usomi wao katika kujenga hoja zinazoleta ufumbuzi wa matatizo yaliyojaa kila Kona ya nchi hii..lakini wakiendelea kufanya madudu wakati Wana CV zilizosheheni,, kina kibajaji wataendelea kuwapopoa na usije ukashangaa huko mbeleni zodoazodoa ikahamia huku mitaani kwetu..Kwa wakurugenzi,makatibu wakuu na wale viongozi waandamizi wanaotumbua Kodi zetu Kwa kutembelea ma V8 wakati hawajatatua kero za wananchi Kwa kutumia dhamana walizopewa kutokana na elimu zao.
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu☺️☺️☺️
Hao unaowaita wasomi tumeshudia mara kadhaa wakijitoa ufahamu kwa lugh rahisi ni unafiki . They have degraded themselves by not keeping their words
 
Msukuma na kibajaji wanajua kujenga hoja ila tu ni mpangilio umewashinda . Wakati wa kuongea wao wanakaa kimya na wakati wa kukaa kimya wao wanaongea . Kipaji cha kuzaliwa wanacho ila wangepalilia na elimu ya darasani .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Lusinde na Msukuma wanapendeza walivyo kwani wangelisoma wangekuwa wajinga na wezi. Hilo linathibitishwa na aina ya wasomi walioko Bungeni ambao wengi wao wametia usomi wao kapuni na kugeuka kuwa WASAKA-TONGE.

Kama kuna aina yoyote ya ujinga umetendeka nchi hii ikiwemo vitendo vya kifisadi na uozo mwingine wowote, umesababishwa na wanaojiita wasomi na kamwe sio la-saba.
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu☺️☺️☺️
Mkuu nimekuelewa vizuri sana na hoja zako nzuri,shida inakuja kwa hawa wasomi nadhani wanaamka na pombe kichwani,Mapendekezo ya pro,ni kama anajitukana alipeea nafasi tena wizara hiyohiyo alifanya cha maana gani cha kukumbukwa!?Wacha aumbuke!
 
"Elimu ni ufunguo wa maisha" hii ni kauli ambayo wengi wengi tumeisikia sana katika juhudi zetu za kutafuta maarifa na ujuzi kwa ajiri ya maisha yetu. Lakini kwa mazingira ya Tanzania elimu imekuwa kitu kingine tofauti kama vile nongwa, kejeli, dhihaka na masimango.

Hakuna kitu kinachouma na kusikitisha kama bunge ambacho ni chombo kinachotunga sheria kuongozwa na ushabiki badala ya weledi Watanzania tujitathimini.

Kitendo cha Wabunge wa darasa la saba kuwashambulia wasomi wakiongozwa na spika sio cha kiungwana na wala hatafika popote maana hakuna ya kuwa na weledi.

Ni muda sasa Wasomi wajitizame kwenye kisha waangalie kama niwaminifu kwenye taaluma zao. Wasomi waaminifu na taaluma zao hawawezi kukubali kudhalilika sababu tu wametoa mawazo tofauti na wengine.

Kitendo cha akina Msukuma na Lusinde kupayuka bungine kumsema mtu kwa "defense mechanism'' bila kutoa hoja ni wazi kabisa bunge halithamini weledi badala ya ushabiki na umbea.

Tanzania mama yangu☺️☺️☺️
wasomi wanajidhalilisha wenyewe kwa kujenga hoja za hovyo hovyo.dunia sasa hivi iko kiganjani na mbaya zaidi hao darasa la saba wengi wao ndo wajasiriamali wakubwa sasa msomi unapochangia kwa nadhalia kubali tu hao wa darasa la saba kwa kuwa ni wazoefu ktk nyanja za biashara watakuchallenge tu hivyo wasomi wajipange wanapotaka kuchangia hoja bungeni.
 
ssue sio elimu kubwa au ndogo.

Bunge la Ndugai ni bunge la vijembe. Linaakisi haiba ya Ndugai, mtu wa mipasho, misuto, na viutani vya kijinga jinga.

Jana ilikuwa kwa wenye elimu, kesho kutwa inaweza kuwa kuwalima vijembe maaskofu. Au wapinzani, au wakaguzi wa mahesabu au wanahabari.

Ni bunge la upashkuna, wa chochote kile.
 
Msukuma na kibajaji wanajua kujenga hoja ila tu ni mpangilio umewashinda . Wakati wa kuongea wao wanakaa kimya na wakati wa kukaa kimya wao wanaongea . Kipaji cha kuzaliwa wanacho ila wangepalilia na elimu ya darasani .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Kuna kitu gani cha maana wanachoweza kuongea zaidi ya kupamba,kushambulia na kutukana.
Wanaweza kusoma ripoti ya CAG na kuilewa wale?
Wanaweza kuzichambua sheria kandamizi?
Wanaweza kuilewa bajeti wale na kueleza mapangufu?
Wanaweza kujadili uchumi ktk global world wale.
CCM ifike mahala ituondolee wabunge darasa la saba, hawana faida yoyote zaidi ya kusaini posho.
Taifa linapata hasara tu kendelea kukumbatia watu wenye uelewa mdogo wa dunia ya utandawazi.
Prof Muhongo hajachambua kiundani hoja yake pengine ana mengi ya kueleza kama atapewa nafasi,hawezi kuwa mjinga kiasi hicho yule ni mtaalamu wa nishati kwa hio tusibeze tu af mbele ya safari tukaje kugundua ukweli.
Kina kibajaji wangekuja na data zinazopinga kauli ya muhongo au wangeomba data kwa muhongo ili alishawishi bunge kwa evidence.
Inawezekana Muhongo anazo tafiti,sisi wengine tunakurupuka tu kwa mihemko.
Ukimpinga Muhongo umpinge kwa data sio maneno matupu.
 
Back
Top Bottom