Hizi mbinu ni very effective na ni rahisi sana maana huhitaji ujuzi mkubwa wa ICT zaid ya kujua kutumia. Ndo social engineering yenyewe. Watu wengi sana wanaingia kingi, hadi wataalam wa ICT wenyewe.
Kuna siku nilipata pm ya 'mdada' anataka nimpe namba yangu ya simu ili kuniunga na kundi la wajasiliamali la whatsApp. Mimi siposti kuhusiana na mambo ya ujasiliamali, alijuaje nitakuwa interested? Lazima uwe na alarm kichwani ili uweze kuruka huo mtego. Japo sina cha kuficha,siwezi kuwarahisishia maisha ktk kunitafuta.
Kwa Social engineering hata benki zinaingia kingi pamoja na kwamba ni taasisi ambazo ni very security conscious.