britanicca
Platinum Member
- May 20, 2015
- 18,063
- 47,048
- Thread starter
- #321
HawaweziNawe je, kwa thread kama hii sio ndiyo umewachokoza wakutafute? Hivi ndiyo kuwa makini? Japo asante kwa thread!
HawaweziNawe je, kwa thread kama hii sio ndiyo umewachokoza wakutafute? Hivi ndiyo kuwa makini? Japo asante kwa thread!
Duh si hatari hiiInawezekana kufanya yale yasiyowapendeza 'wakuu' kwenye mtandao na wasikukamate. Anza kwa kupata simcard feki. Hili ni rahisi. Waweza hata kutengeneza kitambulisho bandia halafu ukasajilia line. Picha waweza weka inayofanana na wewe kwenye hicho kitambulisho-cha msingi isiwe halisi. So kwa gharama isiyozidi 20,000/- unapata line feki.
Hatua ya pili unahitaji email account fake. Usitumie majina wala tarehe ya kuzaliwa ambayo ni halisi. Kama namba ya simu itahitajika wakati wa kutengeneza account, tumia ile ya line feki. Hili lifanyike Internet cafe. Tena ukienda huko cafe fanya kazi moja tu ya kutengeneza akaunti na usifungue mtandao mwingine ambako una taarifa zako halisi.
Hiyo laini itumike kwenye simu moja tu na hiyo simu isiwekwe lain nyingine. Hiyo lain isipige wala kutuma sms namba yoyote na hata vocha ziwekwe za kukwangua sio za kununua online. Inapendeza pia kama simu ni untraceable. Sasa waweza kuwa 'huru' mtandaoni kwa kutengeneza akaunti nyingine nyingi tu ambazo zote zinaunganishwa na email fake uliyotengeneza.
Japo smartphone na simu ya kawaida hutoa location ya mtumiaji kwa kumhusianisha na mnara wa karibu anaotumia au GPS, bado haitoi exact location ulipo kiasi cha mtu kukufuata ulipo.
Kwa upande wa serikali, serikali ipo nyuma sana katika haya masuala ya mtandao. Ianze na kuunganisha database zote-kuanzia RITA, NIDA, UHAMIAJI, NECTA, MAKAMPUNI ya Simu, etc. Tufikie mahali kwa kutumia namba ya simu tu, serikali inaweza kujua mtu amezaliwa lini, ana elimu gani, hali yake kiafya ikoje na you wapi. India ni mfano wa nchi ambazo ukifanya uhalifu mtandaoni wanaweza wakakukamata ndani ya saa 1 kwakuwa wameunganisha database zao. Yaani kitendo cha kumpa muuza duka namba yako ya simu, anapata details zako zote.
Japo sheria yetu ya makosa ya mtandao 'inatisha' sana watu, bado haijafikia zile za nchi zingine ambako hadi internet cafe lazima zifungwe cctv ili kudhibiti wale wanaofanya uhalifu kwa kutumia internet cafe. Tena unakuta sheria inakataza hadi kutumia software za aina flani na hata kuangalia kama server iko online(ping) ni kosa.
Mwisho wanasheria wetu bado hawajajijengea uwezo wa kusimamia kesi za makosa ya kimtandao kwa sababu wanaamini ushahidi wa mtandao hauna chembe ya shaka kumbe kimsingi hakuna ushahidi wenye loopholes nyingi kama ule wa mtandao. Ndo maana watu wanatishwa na kuhukumiwa kwa makosa ambayo sehemu nyingine unashinda kirahisi.
Update:
Hongera kwa serikali kwa kuthibiti mianya ktk usajili wa line za simu. Haiwezekani tena kutumia line bila kusajili wala huwezi kujisajili kwa kutumia kitambulisho chochote isipokuwa cha uraia, passport na leseni ya udereva ambavyo vyote vina taarifa zako muhimu ikiwemo biometric. Hivyo kufanya uhalifu bila kugundulika imekuwa ngumu zaidi.
Bado kuna loophole ktk line zinazopotea. Ukipoteza line kwa kudondosha au simu kuibiwa inaweza ikatumika kufanya uhalifu wa kimtandao. Pia vitambulisho vya uraia, leseni na passport zinazopotea zinaweza kutumika kusajili lain feki maana sidhani kama wale vijana wanaosajili wako makini kiasi cha kuangalia vizuri picha. So tuwe makin na vitambulisho vyetu, vikipotea toa taarifa polisi na polisi wahakikishe kitambulisho kilichopotea hakisajili line mpya.
Disclaimer:Lengo la post hii ni kuelemishana ili kuepuka upotoshaji kuhusiana na masuala ya mtandao. Heshimu sheria za nchi.
Hapo ndo wanaanza kukupumbaza wakutie kwenye mikonoHawa wanaongeaga ngono tuu,hawana madhara na social media
HahahaHumu kuna mtindo uliingia wa kuanzisha 'Whatsapp Group'za memba wa JF
Wengine wapya wanakamatwaNjia hizi watawashika amateur tu
Nimecheka sana hahaHizi mbinu ni very effective na ni rahisi sana maana huhitaji ujuzi mkubwa wa ICT zaid ya kujua kutumia. Ndo social engineering yenyewe. Watu wengi sana wanaingia kingi, hadi wataalam wa ICT wenyewe.
Kuna siku nilipata pm ya 'mdada' anataka nimpe namba yangu ya simu ili kuniunga na kundi la wajasiliamali la whatsApp. Mimi siposti kuhusiana na mambo ya ujasiliamali, alijuaje nitakuwa interested? Lazima uwe na alarm kichwani ili uweze kuruka huo mtego. Japo sina cha kuficha,siwezi kuwarahisishia maisha ktk kunitafuta.
Kwa Social engineering hata benki zinaingia kingi pamoja na kwamba ni taasisi ambazo ni very security conscious.
Yanini niumize kichwa ilhali sifanyi kosa.
Isije ikawa na wewe ni intelijensia unafanya research kujua uelewa wa watu jinsi mnavyofanya kazi maana mahaka ya cyber crime na mafisadi zimekosa washtakiwa.
Wapinina dada zng wawili JF, sa wewe ushaanza kuntisha!
Kama wewe kila nikikuangalia nakuhisi hisi! sijui why!Asante kwa taarifa
Kazi kweli kwelinimemalizia uchunguzi wangu wakujua jinsi gani kauli ya rais kwamba watumia Mitandao wakiamua wanakupata nimetenga week nzima, kwanza kwa kuweka target yamaeneo ya kufanyia research yangu,
Taasisi nilizopita ni tatu, nimeenda wale wanaogawa gate ways kwa mitandao mingine ambao wako pale samora avenue, shirika kongwe la simu,
Pili nikaenda pale derm complex kijito nyama kuna ule mtandao wa wanafunzi,
Tatu nikaenda kule Mandela road taasisi ipo karibu na university road, kabla hujafika kituo cha simu 2000 kama watokea mwenge,
Taasisi zote hizo Nina watu wa karibu kizuri zaid taasisi mbili nimezifanyia kazi mda mrefu tu, najuan mambo mengi ya tracking,
Sasa tafiti yangu ilikuwa ni kwa zile forums ambazo server zake haziko nchini au Ni vigumu kupata IP address zao kutokana na anonymous issues,
Nimefanya kujua ni kwa njia ipi wanaweza kutrack mtu wakampata,
1. Wanatumia attached adverts kwenye forums husika, yaan mfano unakuta umetumia jina fake lakin katika forum iliyopo kuna tanzagazo la biashara Fulani, ukiligusa tu umekula waya, maana wale wanakuwa na MS-DOS PROXY zilizokuwa injected katika website au application zao, ambazo zinawezesha anayetrack kupata IP address and location,
2. Kwakuwa forums hizi siyo peer to peer network ambayo watu huepeana IP address, hivyo wanaotrack wanakuwa easy kujua IP address zako haza kwa wale walio install application (mfano application ya jf kwenye simu yako) wakati wa kuinstall kwenye playstore ulilogini kwa email add
Yako ambayo ni valid hivyo anonymity's inakuwa easy kujua kwamba huyu yuko sehem Fulani na anatumia aina Fulani ya device,
Walio salama Mara Nyingi ni wale ambao hawa install apps za forums kwenye simu wanaenda kwenye browser moja kwa Moja, japo napo wanapajua kutrack
3. Kulogin kwenye simu yako kwenye account mbali mbali ambazo ziko kwa application alafu ukalogin na forum ambayo umeficha jina hiyo Inakuwa imekumaliza siku Nyingi
4. DNS PROXY, hii ni hatari mnoo hizi zimetumika kutrack email address zote valid ambazo watu wanafungulia accounts katika forum's mbali mbali
Hata kama ni vigumu kutrack server ya forum wanatumia hii kujua email addresses zilizofunguliwa Tanzania ni za kina Nani na wanamiliki akaunti zipi ndani ya forums mbali mbali, hii inatumia muda kidogo pamo a na uzembe wa watanzania wanaweza waajiriwa wasiiweze ila nimeona imetrack watu 24 katika forums mbali mbali,
Wito wangu mi huwa situmii email address valid katika forums hata ukifoji address inafungua hata bila kuwa active, maana hapa ni hatari mno,ukitaka kuhakikisha create account yeyote kwenye forum yeyote kwa kutumia email ya kubuni tu, hata ukiandika mwendokasi@gmail.com inakubali , situmiagi email valid, maana hata wakati wa kufanya registration, registration details zote zinatumwa kwa server za trackers, kuanzia jina la mwenye email address na location na amejiunga forum ipi anatumia jina gani,
6. Mods kuuza mechi, yan inaweza kuwa imekuwa ngumu kukupata mod akiamua umekwisha, maana mod wakimjua ni nani alafu wakampata mkwanja wa kutosha hata kama umetumia email fake, maana modes wanauwezo wa kujua kila mmiliki wa account kwa njia hizi,
Logini daily ina access wapi,
Password aliyotumia wao wna uwezo wa kuijua, na udhaifu wa watu kwenye forums mbali mbali huwa wanatumia password Ile Ile kwenye account tofauti tofauti ndani ya forum husika, na katika account Moja wapo anakuwa katoa taarifa sahihi, hivyo mods hata hapa wanaweza kutrack nani mwenys account flani,
7. Kupokea messeji au call kwenye line ambayo umejiunga kifurushi na unaitumia ku browse wakati umelogin kwenye forum yeyote hiyo inatuma direct taarifa husika kupitia e-server detection
Maana inatuma uko wapi mnala unasoma wapi na umelogin kwa akaunt ipi, jamani tuko uchi
Ila nawataadharisha atadakwa mmoja mmoja Mchochezi, maana habari ninayopata nakuwa makin na Mimi,
Ila kwa wanaoishi nje, na wanaotumia Wi-Fi bila kuhusisha line yeyote hao wana uafadhari kidogo,
8. Njia Nyingine ni several messages within forum, yaan zile ni PM mtu akikiu PM Mara 10 unareply hasa hawa huwa wametumwa ni kama mtu anaweza kuifanya mfanya biashara au mdada mkali mkachati, through chatting za PM zinatengeneza mazingira (peer to peer network Ina kuwa easy kuwa created na kusaka IP addresses) msiwaamini sana madada hao,
Tuwe makini orodha ipo nawaambia usibishe nimeona na sitataja, na sitakuja kuitaja kamwe, na kuna forums zitafungiwa soon,
Usinibishie hata kama unaona nimeandika pumba lakin zitilie maanani ukizingatia hayo ni vema hutapoteza ila utagain,
Huu uzi moderators wau pin [emoji625] hapo juu, kuna watu wanatiririkaga humu mwisho wanapotea kama upepo, itawasaidiaTekinologia ilipofikia kila kifaa,unachotumia kuweka line ya Simu, watoa huduma wanajua IMEI Namba.Wanaweza fatilia taarifa zako na print mawasialiano na nambari washirika wako,na kujua mahali.Fake Ids ni kama tinded na pazia .La msingi uwe makini kuzingatia sheria na kuwa tayari kuwajibika kwa unachokiandika.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mh
HakikaNoma sana!
Kwa wanaotumia fake identity na kuamini kuwa wako salama asilimia 100% ni kujidanganya...fake identity inaweza kuwa fumbo kwa sie walei wa mambo ya tekinolojia ila kwa wataalamu kujua taarifa zako ni sawa na kunywa maji ya vuguvugu. (Sitishi ila ndio uhalisia)Habari zenu nahisi mko safi sana, je unajua kuwa pamoja na kwamba server ya baadhi ya forums ni vigumu kupata wenye akaunt lakin nawaibia siri, kidogo, pamoja na hiyo kama kukupata hawashughulik sana,
Watu wengi hawajuhi njia hizi hutumika na kumpata muhusika
1. Matangazo ya kazi, hapa watu wanakuwa washasahau kama wamesha comment mambo yasiyo na msingi. Mwana intelijensia mmoja anaweka tangazo la kazi, watu wanazama pm na kujiachia sana kuwa kaka nisaidie kaka nisaidie
2. Kuna wale wanaojiita "MISS FLAN NA MISS FLAN" Vijana wengi kwa mihemko ya mapenzi huzubaishwa na nyuzi wanazoanzisha hawa wanaojifanya wanawake kumbe ni madume kwenye mtandao, na kuwafuata PM kutililika kila kitu
Na kupanga maeneo ya kukutana mara mtu hatokei lengo ameshapata contact yako,
3. Matangazo ya biashara na connection mbalimbali, hizi pia ni njia rahisi kumdaka mtu na wamedakwa wengi mno,
4. Ushauri wa mapenzi na nguvu za kiume , hapa hatari sana watu wanaanzisha nyuzi watu wanaingia kichwa kichwa,
5. Wale wanaodanganya eti " nimepata clip moja ni hatari inamsema mkulu naogopa kuiweka hapa" utasikia watu wanajibu na Ku pm Namba yangu unitumie whatsap bhaaass.
6. Wanaojifanya kuipinga serikali na kuikashfu mtandaon hawakamatwi kama B-K hawa ni wa kutilia mashaka maana wanatengeneza mazingira uone hawako.na serikali na unapanga nao mikakati kumbe hatari sana,
7. Njia Nyingine inayotumiwa na nchi zilizoendelea ni rahisi kujua kwa Kuwa kifaa chochote kinachotumia mawimbi ya kimtandao kina kawaida ya kutuma signal au Taarifa kila sekunde katika chanzo chake Sever machine hivyo kitendo cha wewe kutumia kifaa cha aina hiyo Tayari umejiingizA katika hesabu za mtu Na ni rahisi kudakwa kwa sababu kifaa chako kinasema ulipo.
Ushauri ni kwamba usitoe contact zako hata kama ni dili, maana ni Muhim kujilinda, lakin pia tuwe makini tunavyoanzisha thread au Ku comment tusitukane,
Pia. Tekinologia ilipofikia kila kifaa,unachotumia kuweka line ya Simu, watoa huduma wanajua IMEI Namba.Wanaweza fatilia taarifa zako na print mawasialiano na nambari washirika wako,na kujua mahali.Fake Ids ni kama tinded na pazia .La msingi uwe makini kuzingatia sheria na kuwa tayari kuwajibika kwa unachokiandika.
Muwe na mchana mwema
Britanicca encyclopedia