Jinsi wanausalama wa mtandaoni wanavyowapata watu

Jinsi wanausalama wa mtandaoni wanavyowapata watu

Habari zenu nahisi mko safi sana, je unajua kuwa pamoja na kwamba server ya baadhi ya forums ni vigumu kupata wenye akaunt lakin nawaibia siri, kidogo, pamoja na hiyo kama kukupata hawashughulik sana,

Watu wengi hawajuhi njia hizi hutumika na kumpata muhusika
1. Matangazo ya kazi, hapa watu wanakuwa washasahau kama wamesha comment mambo yasiyo na msingi. Mwana intelijensia mmoja anaweka tangazo la kazi, watu wanazama pm na kujiachia sana kuwa kaka nisaidie kaka nisaidie

2. Kuna wale wanaojiita "MISS FLAN NA MISS FLAN" Vijana wengi kwa mihemko ya mapenzi huzubaishwa na nyuzi wanazoanzisha hawa wanaojifanya wanawake kumbe ni madume kwenye mtandao, na kuwafuata PM kutililika kila kitu
Na kupanga maeneo ya kukutana mara mtu hatokei lengo ameshapata contact yako,

3. Matangazo ya biashara na connection mbalimbali, hizi pia ni njia rahisi kumdaka mtu na wamedakwa wengi mno,

4. Ushauri wa mapenzi na nguvu za kiume , hapa hatari sana watu wanaanzisha nyuzi watu wanaingia kichwa kichwa,

5. Wale wanaodanganya eti " nimepata clip moja ni hatari inamsema mkulu naogopa kuiweka hapa" utasikia watu wanajibu na Ku pm Namba yangu unitumie whatsap bhaaass.

6. Wanaojifanya kuipinga serikali na kuikashfu mtandaon hawakamatwi kama B-K hawa ni wa kutilia mashaka maana wanatengeneza mazingira uone hawako.na serikali na unapanga nao mikakati kumbe hatari sana,

7. Njia Nyingine inayotumiwa na nchi zilizoendelea ni rahisi kujua kwa Kuwa kifaa chochote kinachotumia mawimbi ya kimtandao kina kawaida ya kutuma signal au Taarifa kila sekunde katika chanzo chake Sever machine hivyo kitendo cha wewe kutumia kifaa cha aina hiyo Tayari umejiingizA katika hesabu za mtu Na ni rahisi kudakwa kwa sababu kifaa chako kinasema ulipo.

Ushauri ni kwamba usitoe contact zako hata kama ni dili, maana ni Muhim kujilinda, lakin pia tuwe makini tunavyoanzisha thread au Ku comment tusitukane,

Pia. Tekinologia ilipofikia kila kifaa,unachotumia kuweka line ya Simu, watoa huduma wanajua IMEI Namba.Wanaweza fatilia taarifa zako na print mawasialiano na nambari washirika wako,na kujua mahali.Fake Ids ni kama tinded na pazia .La msingi uwe makini kuzingatia sheria na kuwa tayari kuwajibika kwa unachokiandika.

Muwe na mchana mwema

Britanicca encyclopedia
Hahahhah
No. 5 ndio iliniweka Stakishari.
Nikajaa Pm...wakajaa na mimi
 
Mimi ku comment chochote kitakachonifanya niishie mahakamani siogopi ila am in no mood to anticipate pyu! pyu! pyu!
 
😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀.....Utapishana na gari la mshahara usiogope PM sana!!!
Hahahhah
Mie kiukweli muda mwingine nakuwa fyatu ila saa zingine nakuwa kama mwanamke wa kujenga familia.
Hahhaha
 
Hamna namna

Maana waweza jikuta unapishana na gari la mshahara kama ulivyosema
Si unaangalia mtu alivyokuja hauingii kichwa kichwa mwanangu,akija kirafiki unaenda nae kirafiki akija kidwanzi unaenda nae kidwanzi,akija kimafioso unaenda nae hivyo hivyo kimafioso,ukifata principle hauwezi pishana na gari la mshahara 😀😀😀.
 
Hahahhahhah
Kwakweli.
Ila unadhani mie nilivyokamatwa pale Catalunya unadhani ilikuwaje...mtu alikuja humu Pm, kwanza nimeanza nae jukwaani, tukahamia Pm...kumbe askari.
Nikaingia kwenye 18 zake, nikaenda Stakishari, kumbe nilikuwa natafutwa siku nyingi tangu kazini.
Basi nikala siku zangu 14 selo, nikarudi uraiani.

Humu acha tu niwe bandidu.
Ukiona mpaka nimekutana na mtu niliyemjua pm basi ujue kazi ipo
 
Pole sana!!
 
Back
Top Bottom