Jinsi tunavyoibiwa petrol station

Jinsi tunavyoibiwa petrol station

Kiukweli imenikuta pale mwenge mpakani niliweka mafuta ya elfu 20 kwakawaida huwa najua wapi gauge huwa inafikia. Siku hiyo mshale haukupanda nilipouliza nikaambiwa utapanda badae, nimeenda mpaka home haupandi.

Sasa nikaja kujua sababu huwa nikijaza mafuta 20 kwa routes zangu huwa natumia siku mbili ila siku ile nikaishiwa mafuta siku ya pili kabla sijafikia ata robo ya trip. Nikaamua kuwafuata na bahati nzuri nikamkuta jamaa aliyeniuzia kumpiga mkwara akasema eti pump nilikuwa mbovu, nikwambia nitawaripoti kwa euwra, wakasema labda ilitokea shida.

Watu wa shell ni wapuuzi sana, ni wezi sana.
mwisho wa siku ulirejeshewa kiasi cha petrol ulichoibiwa?
 
Total & Victoria basi wengine usiende
 
Asee mi wamenifilisi basi..
Mwaka wa tano huu ila kuanzia Leo ni dumu kwa kwenda mbele...

Hivi sheli wanakubali ushushe dumu ukiwa na gari hapo hapo?
Kama gari lako la petrol wadanganye ni la diesel, ila ww unahitaji petrol kuna gari la mshikaji nampelekea ngwese ndinga lake limebuma rodini.
 
Mimi gauge yangu Ya mafuta Ni digital, Unayosema Ni kweli kabisa,nimeshawekewa litre 8.6 muhudumu anakomaa kaweka litre 10, nikamwambia Kabla hajaanza kuweka mafuta nilikua na reserve Ya litre 10.2 kwahiyo baadaya Ya Kuongeza mafuta yake ilitakiwa gauge isome 20.2, nikaanza kumpa vitasa vya nguvu,shabashi wanatuibia sana hawa kima.
 
na ukikuta sheli yenye petrol iliyochakachuliwa pamoja na kidumu chako kujaa vizuri lazima gauge ishuke mda mfupi baada ya kutumia, wenye kujua mafuta mazuri pia mtuelekeze pa kuyapata
 
Hii nimeiona mara nyingi sana: Pump unayoshinikiziwa kupark gari huwa mara nyingi inakuwa imetoka kujaza volume ndogo ya mafuta kwenye chombo kingine cha moto, so ukipark hapo wanaanza kufuel kwako bila kuanzia ZERO reading ya meter yao (Mostly utakotakuta either imetoka bajaji or bodaboda) unaishia kulipa 20,000/= kumbe umewekewa mafuta ya 14,000/= hiyo 6000 ni faida kwake.

Pia huwa wanakuchangamkia mwingine anakuongelesha mwingine anaweka pump kwenye gari na kujifanya wamesahau kukuuliza waweke mafuta ya sh. ngapi na wanakwambia wameshaanza kuweka. Tabia hii ipo sana sheli za fulani hapa maeneo ya ubungo.

Huwa nikifika hapo nazima gari nashuka kabisa ndio naanza kuonea nao

Kuelekea sinza ukitokea Shekilango kuna kituo cha Mafuta GBP, Ni muda umepita lakini nilipatwa na mkasa kama unavyoelezea hapa Ndugu, Nilikuwa na Gari Land cruiser VX V8 inatumia Diesel ,Jipya, na nilikuwa natokea Toyota Motors ambako baada ya taratibu zote nilikabidhiwa Gari langu na Nyaraka zikionyesha pia Mafuta yaliongezwa lita50. Na vipimo vya gari vilionyesha mafuta yapo chini ya Nusu tanki,Kwa kuwa nilikuwa nasafiri mchana huo nilipitia nyumbani nikachukua
Nguo chache na mkoba wa safari kwa ajili kazi, Napendelea kutumia mafuta ya BP tangu zamani hivyo nikaona nikiingia pale sinza itakuwa pia ni rahisi kutoka ingawa hakukuwa na foleni sana, Wakati naingia nilipokelewa kwa Bashasha sana na Dada wawili wakiwa na mlinzi mwenye silaha na nikaelekezwa pa kusimama , kwa kuwa mfuniko unafungulia ndani tayari Mhudumu alishaishika pipe ya kuweka mafuta na kuomba nifungue mfuniko..! Pembeni mlinzi nae kaniijia na kuanza kusemesha huku kasogelea mlango kwa karibu sana, kwa kuwa kioo kilikuwa wazi upande wangu na tena nilikuwa na fedha nyingi kidogo ikaniwia vigumu kuteremka kwa hofu ya yule mlinzi maana aliona wakati natenga zile fedha za kununulia mafuta, ghafla Muhudumu akaniuliza niweke lita ngapi? Nikamjibu Jaza kabisa Kichekesho cha Mwaka nikashangaa zimeingia Lita 142.7.. kama kwamba Gari lilikuwa halina mafuta kabisa , Ghafla mlinzi akatoka eneo lile na nikaletewa Risiti ya Madai, Kwa kuwa Nilitambua kuwa umefanyika mchezo mchafu kwa upole nilimwambia yule Muhudumu kilichotokea ingawa alihamaki kidogo lakini Body language yake haikuendana na sentesi zake, Na yule mlinzi alitegemea ubishi maana nilifikiria vitu vingi, Pampu inasoma 142.7 Litres, Ninapokwenda ni muhimu na nikipoteza muda najichelewesha,Nitabisha nini sasa, Nikafikiria hasara zinapata Watu wangapi? Nikamwambia yule Binti Naondoka lakini usitegemee nitarudi kujaza mafuta hapa tena na Rafiki zangu nikawaaambia, Yule Binti hakuwa mchangamfu tena kama mwanzo, Hivyo Niliingizwa mjini kwa kuiamini BRAND kumbe ovyo tu labda wabadilike.
TUWENI MAKINI UNAPOHITAJI KUONGEZA MAFUTA HAKIKISHA PAMPU INAANZA KUSOMA UPYA.
 
Kama gari lako la petrol wadanganye ni la diesel, ila ww unahitaji petrol kuna gari la mshikaji nampelekea ngwese ndinga lake limebuma rodini.
Mrejesho nimeenda na dumu mbili za Lita ishirini pale GBP ya mapambano kila Lita 20 nimeuziwa 370000, maajabu sasa nimeenda kujaza kwenye Gari nimestaajabu sana, kiufupi hawa watu ni wanatupiga

Note: kwenye dumu hujaziwi kwa kutumia mpira unakuta umeshaandaliwa yamefichwa chemba, so mnabadilishana madumu
 
na ukikuta sheli yenye petrol iliyochakachuliwa pamoja na kidumu chako kujaa vizuri lazima gauge ishuke mda mfupi baada ya kutumia, wenye kujua mafuta mazuri pia mtuelekeze pa kuyapata
Mi nimeelekezwa TOTAL pale Mlimani City... nimeanza kujaza pale, baada ya mwezi ntajua tuu
 
IMG-20250713-WA0001.jpg
 
Salamu wanajukwaa, leo asubuhi nimebaini jinsi wahudumu wa vituo vya kuuzia mafuta wanavyotuibia wateja.

Nilikuwa kwenye kituo cha mafuta Sinza nimepaki tayari kuwekewa mafuta baada ya kulakiwa kwa bashasha na kuelekezwa pump na wahudumu, kwa mara ya kwanza nilihisi wananiita kimashindano labda kuna bonus kwa mwenye mauzo makubwa.

Nilipaki kwenye pump ya kati katika tatu zilizopo, lakini nikaambiwa niende ya mwanzoni au mwishoni, mimi bado nikawa katika ileile pump ila muhudumu hakutaka kunihudumia pamoja na bashasha za kunilaki mwanzoni.

Akaja mtu ana dumu la lita tano akapewa petrol akaondoka, akaja na mwingine pia akapewa, kwakuwa nilikuwa nawahi nikasogea pump ya mwishoni nikapata huduma nikaondoka huku nikitafakari sana kwanini imekuwa vile.

Baadaya ya kuwaza sana, nimegundua pump zile mbili yaani ya mwanzo na mwisho huwa zitatoa mafuta machache, kwa mfano ukinunua lita tano, basi unapata pungufu na ndiyo maana wanasakizia wenye magari tuende huko kwakuwa hatutayaona.

Pump ya kati itakuwa inatoa ujazo sahihi ndiyo maana huwa wanawauzia wenye vidumu tu. Hili nimeliona pia Kinondoni katika kituo kikongwe sana.

Nawaomba wenye magari tukatae kuhamishwa pump jamani, inaonyesha watu wa vipimo hawajalibaini hili.

Karibuni tupeane uzoefu.
Thread 'Kasi ya ujenzi ya vituo vya kujazia mafuta ya magari inaendana na ubora, usafi na usalama wa mafuta yenyewe?' Kasi ya ujenzi ya vituo vya kujazia mafuta ya magari inaendana na ubora, usafi na usalama wa mafuta yenyewe?
 
Ongeza bidii kwenye kutafuta hela uache kuchunguza pamp
 
Salamu wanajukwaa, leo asubuhi nimebaini jinsi wahudumu wa vituo vya kuuzia mafuta wanavyotuibia wateja.

Nilikuwa kwenye kituo cha mafuta Sinza nimepaki tayari kuwekewa mafuta baada ya kulakiwa kwa bashasha na kuelekezwa pump na wahudumu, kwa mara ya kwanza nilihisi wananiita kimashindano labda kuna bonus kwa mwenye mauzo makubwa.

Nilipaki kwenye pump ya kati katika tatu zilizopo, lakini nikaambiwa niende ya mwanzoni au mwishoni, mimi bado nikawa katika ileile pump ila muhudumu hakutaka kunihudumia pamoja na bashasha za kunilaki mwanzoni.

Akaja mtu ana dumu la lita tano akapewa petrol akaondoka, akaja na mwingine pia akapewa, kwakuwa nilikuwa nawahi nikasogea pump ya mwishoni nikapata huduma nikaondoka huku nikitafakari sana kwanini imekuwa vile.

Baadaya ya kuwaza sana, nimegundua pump zile mbili yaani ya mwanzo na mwisho huwa zitatoa mafuta machache, kwa mfano ukinunua lita tano, basi unapata pungufu na ndiyo maana wanasakizia wenye magari tuende huko kwakuwa hatutayaona.

Pump ya kati itakuwa inatoa ujazo sahihi ndiyo maana huwa wanawauzia wenye vidumu tu. Hili nimeliona pia Kinondoni katika kituo kikongwe sana.

Nawaomba wenye magari tukatae kuhamishwa pump jamani, inaonyesha watu wa vipimo hawajalibaini hili.

Karibuni tupeane uzoefu.
Ilinikuta hiyo picha ya ndege kibaha sita sahau halafu ilikuwa usiku.
 
Back
Top Bottom