Mnondwe
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 4,013
- 3,678
Salamu wanajukwaa, leo asubuhi nimebaini jinsi wahudumu wa vituo vya kuuzia mafuta wanavyotuibia wateja.
Nilikuwa kwenye kituo cha mafuta Sinza nimepaki tayari kuwekewa mafuta baada ya kulakiwa kwa bashasha na kuelekezwa pump na wahudumu, kwa mara ya kwanza nilihisi wananiita kimashindano labda kuna bonus kwa mwenye mauzo makubwa.
Nilipaki kwenye pump ya kati katika tatu zilizopo, lakini nikaambiwa niende ya mwanzoni au mwishoni, mimi bado nikawa katika ileile pump ila muhudumu hakutaka kunihudumia pamoja na bashasha za kunilaki mwanzoni.
Akaja mtu ana dumu la lita tano akapewa petrol akaondoka, akaja na mwingine pia akapewa, kwakuwa nilikuwa nawahi nikasogea pump ya mwishoni nikapata huduma nikaondoka huku nikitafakari sana kwanini imekuwa vile.
Baadaya ya kuwaza sana, nimegundua pump zile mbili yaani ya mwanzo na mwisho huwa zitatoa mafuta machache, kwa mfano ukinunua lita tano, basi unapata pungufu na ndiyo maana wanasakizia wenye magari tuende huko kwakuwa hatutayaona.
Pump ya kati itakuwa inatoa ujazo sahihi ndiyo maana huwa wanawauzia wenye vidumu tu. Hili nimeliona pia Kinondoni katika kituo kikongwe sana.
Nawaomba wenye magari tukatae kuhamishwa pump jamani, inaonyesha watu wa vipimo hawajalibaini hili.
Karibuni tupeane uzoefu.