SoC02 Jinsi Serikali inavyoweza kutumia miradi mipya ya kibunifu kuingiza mapato zaidi kuliko kutegemea tozo na kodi zaidi

Stories of Change - 2022 Competition

Bobby12

New Member
Aug 29, 2022
4
7
Tozo

Tozo ni ushuru au kodi ambayo wananchi wanatozwa na serikali. Pia hii ni aina moja wapo ya chanzo cha mapato kwa serikali za sasa hasa zile za ulimwengu wa tatu ambayo pia huchangia maendeleo ya miradi mbalimbali ya serikali kama kujenga hospitali, barabara, shule, mishara na marupurupu pia hutumika kuendesha taasisi za serikali kama polisi, jeshi n.k.

Mapato yasiyotokana na kodi ni muhimu sana lakini mara nyingi vyanzo vya haya mapato havitumiki ambovyo ni muhimu zaidi kwa sasa katika nchi za African kutokana la wimbi la umaskini maendeleo duni, kupanda kwa madeni ya nje, bajeti za nchi kutojitosheleza, rushwa na changamoto nyingine. kwa makaridio inaonekana Africa itahitaji fedha nyingi ili kuibalidilisha kufikia ile ajenda ya umoja wa mataifa ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na ile ya mwaka 2063.

Unahitajika ufanisi, uwezo na jitihada za kuwa mbunifu kufikiria, kuongeza na kupanuo wigo ukusanyaji wa mapato yasiyotokana na kodi mfano bostwana ukusanyaji wa mapato yake nje ya kodi ni asilimia 16 huku Tanzania ni asimilia 2.

Bostwana ina shika asimilia 50 ya mirahaba ya almasi kwenye migodi yake ya orpa, lethakane na Damtshaa pia inashika asilimia 94 ya mirahaba ya madini ya kopa kwenye mgodi wake wa BCL, inaskikilia pia asilimia 50 ya mirahaba ya madini ya magadi na chumvi katika mgodi wake wa botash, migodi mengine ya madini ina mirahaba ya asimilia 10 Hadi 15 japo mingine haina kabisa lakini kwa kushika hizo asilimia inaipa serikali fedha nyingi za moja kwa moja mbali na ulipaji wa kodi.

Mfano ukiangalia nchi nyingi zilizo endelea hazikutegemea tozo hazikuangalia wananchi kama chanzo cha mapato bali hiyo kwao ilikuwa sehemu ndogo nchi kama urusi imewekeza kwenye Maliasili zake gesi, makaa na mafuta na serikali moja kwa moja ndo inauwekezaji pale mfano kampuni lake la Gazprom kupitia huu mradi serikali imekuwa ikipata fedha nyingi pia wanazalisha umeme na makaa ya mawe wanauza nje yanaiingizia serikali fedha nyingi za moja kwa moja bila kutugemea sana vyanzo vya kodi ukiangalia nchi nyingi zilizoendelea kama Dubai pia walikaa chini na wataalamu wa jiolojia mwaka 1994 wakaambiwa ifikapo 2016 mafuta yatakuwa yameisha lakini sultan Bin Sulayem alikuwa kiongozi wa hiyo kamati ya mipango ya milinia ya taifa alisema "nilijua baada ya ile ripoti ya wanajiolojia mafuta yataisha kwahiyo tukafikiria tukaona tuna machaguzi mawili ama kufanya kitu ili kutafuta njia nyingine kuokoa maisha ya watu wa Dubai au kukaa na kusubiri misaada"

Baada ya hapo Dubai ndio ikawaalika wataalamu kuangalia jografia yake kisha kuona wana fukwe na jua ndo vyanzo pekee vinavyoweza kuwapatia mapato ndio wataalamu kutoka nchi mbali mbali za ulaya walio waajiri wakasema kitu pekee ni kutumia hiyo bahari na, jangwa kufanya Dubai kuwa sehemu nzuri na muhimu kwa ajili ya utalii ndo maana wakaanza kujenga hoteli za kitali za fahari kubwa, visiwa vya kujengwa na binadamu kwa kutumia miundo mbalimbali kama vile ramani ya dunia, visiwa vyenye mfano wa mtende maana kwao ndo mti unaopatikana sehemu za jangwa, soko lenye maduka makubwa zaidi dunia ambayo ina kila kitu ndani inayowavutia watalii wengi zaidi duniani, pia walifanya bandari yao kuwa bandari huru (free port) kitu kilichovitia mataifa mengi ya ulaya kupitisha bidhaa zao hadi leo kupitia bandari ya Dubai japo sasa wameanza kutonza kiasi kidogo cha ushuru hii walijua kodi watapata maana biashara itafanyika sana ndani ya nchi yao na serikali itapata kodi.

Ukiangalia kwa upande wetu sisi Tanzania kwenye upande wa mirahaba ya madini ya metaliki, gemstones kama vile tanzanite rubi n.k pamoja na almasi ni asilimia 6 uranium ni asilimia 5 chumvi na madini ya viwandani ni asilimia 3 ukiangalia hiyo mirahaba na ya Bostwana bado tupo chini na ndo maana sekta ya madini inachangia asilimia 10 ya pato la taifa ila ukiangalia nchi kama libya kipindi cha muammar gaddafi asilimia 75 ya pato la nchi huku Algeria gesi inachangia asimilia 25 na mafuta asimilia 19 ya pato la taifa kwa mafuta na gesi tu walitoa sera ya kuwalipa watu wasio na ajira.

Hapa kwetu Tanzania tuna maliasili kuacha madini kuna hifadhi kubwa ya gesi ambayo bado haijachimbwa kuna makaa ya mawe kutokana na hali ya uchumi kupanda kwa bei za nishati ilikuwa ni wakati sahihi kwa serikali hata kama haitawekeza kwa asimilia 100 basi iingie ubia na makampuni iwezekeze angalau asilimia 35 Hadi 50 hii itasaidia kukua kwa pato la taifa moja kwa moja.

Nchi nyingi Africa vyanzo vya mapato visivyotokana na kodi ambavyo tuna tegemea zaidi ni mikopo kutoka nje ifike wakati tufanye kama Dubai kutafuta wataalamu hata kuwaajiri kwa muda waje watufanyie utafiti wa vyanzo mbadala wa kupata mapato mbali na kodi na mikopo maana tumeona mfano mzuri wa Algeria, Libya ya Gaddafi, bostwana, urusi na Dubai walivyotumia vyanzo mbadala mbali na kodi kukuza pato lao mfano hizi nchi zingetegemea kodi tu kutoka kwa wananchi na tozo zingebaki kupewa misaada kama sultan Bin Sulayem wa Dubai alivyosema.

Pia kushindwa kukusanya kwa ufanisi mapato yasiyotokana na kodi kama ya kwenye taasisi za serikali, mashirika mengine pamoja na mikoa katika kuchangia pato lao serikalini unakuta kutokana na rushwa na usimamizi usio thabiti serikali inapoteza mapato mengi inakuwa vigumu kijiendesha badala yake inageukia tozo na mikopo kutoka nje sasa iwapo uongozi ukiwa dhabiti kwamba kila mtu akisimama kwenye nafasi yake na wakuu wa mikoa wakiwa wabunifu kubuni miradi kulingana na jiografia ya mikoa yao itakuza pato na mikoa pamoja na taifa hata hii tozo isingukuwa na nafasi.

Kwa hiyo ninashauri viongozi na watunga sera wawe wabunifu, wapanue wigo wao wakutafuta vyanzo vya mapato kupitia rasilimali yaani maliasili zilizopo katika taifa kuliko kufikiria tu kwa watu. sisi tunavitu vingi kama vile mbuga za wanyama, madini, gesi, makaa ya mawe kinachohitajika tu ni kuunda mifumo upya kutazama upya sera za uwekezaji na mirahaba ya maliasili zetu maana ukiangalia pia serikali ya Dubai ina miliki karibu sheli zote za mafuta kitu kinacholiingizia taifa fedha nyingi moja kwa moja hivi ni vitu tunavyotakiwa kujifunza kwahiyo kwa kuhitimisha tukiangalia ustawihi wa mataifa hayo mengi ni kutokana na uongozi dhabiti, pamoja na ubunifu wa kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ndo umezifikisha hizo nchi zilipofika wala sio kodi kubwa wala tozo.
 
Back
Top Bottom