Mkuu Trader, nimejitutumua kuelewa hiyo lugha ya kisheria uliyoandika na ninapenda kuamini kwama nimeelewa sahihi. Nakushukuru kwa utafiti wako na mawazo yako. Hata hivyo najaribu kujitahidi kukubaliana na wewe lakini bado yafuatayo yananitatiza;
1. Ninaposoma bandiko lako inakuwa kama nasikiliza marudio ya kauli za Ngeleja na Werema kwamba kwa mujibu wa sheria ni lazima tulipe hiyo tuzo vinginevyo?
2. Lakini pia ninasikia sauti za akina Mwakembe na Sita kwamba mahali pa kutokea pako wazi, uhalali wa kampuni na mkataba kuhamishwa
3. Pia nasikia sauti za wanaharakati wanasheria kwamba kuna uwezekano kabisa wa kupinga hiyo tuzo na kushinda.
4. Mwisho nasikia sauti za wananchi na wabunge kwamba tusilipe chochote kwani siyo deni ambalo ni kipaumbele katika madeni yote ya ndani na nje.
Kwa hiyo naomba niahirishe kukubaliana na wewe hadi wanasheria wote, viongozi na wananchi watakapozungumza lugha moja, kwamba hiyo hukumu hatutakiwi kisheria kukata rufaa. Nasikitika sana.