Jinsi Richmond/Dowans walivyoizunguka TANESCO na Taifa

Jinsi Richmond/Dowans walivyoizunguka TANESCO na Taifa

Thanks kwa sana tu Mkjj.

Natumaini Legal and Human Rights Center kwa kushirikiana na mashirika mengine ya haki za binadamu yanakusanya/yanapewa/yanapokea hizi taarifa na nyingine nyingi ili kusaidia rufaa ya WATANZANIA huko Mahakama Kuu dhidi ya hukumu ya kisanii ya ICC.

Kama ulivyosema, suala la Richmond kuhamishia mkataba wake Dowans bila kupata ridhaa ya kimaandishi kutoka TANESCO ni kinyume cha kifungu 15.12 cha mkataba kati ya Richmond na Tanesco. Nadhani hapa tayari Richmond walikuwa wamekiuka mkataba.

Uozo ni mwingi sana, na unatia hasira sana.

Hizo walizoiba za EPA, Kagoda, Deep Green na nyinginezo haziwatoshi tu hadi waibe na hizi??? Arghhhhh....

This is the beginning of their end.

Tunisia, Egypt, then Tanzania...

Down with the corrupt tyranny!!!
 
Mwanakijiji said:
Sijui kama viapo kwao vina maana tena kwa sababu wale waliokula viapi ndio wametusaliti.

MKJJ,

..wenzako wamekula kiapo kulinda mtandao na maslahi yake.

..wamiliki wa Dowans ni viongozi wakuu wa serikali na CCM.

..kwa msingi huo, hii pesa lazima walipwe tu.
 
Thanks kwa sana tu Mkjj.

Natumaini Legal and Human Rights Center kwa kushirikiana na mashirika mengine ya haki za binadamu yanakusanya/yanapewa/yanapokea hizi taarifa na nyingine nyingi ili kusaidia rufaa ya WATANZANIA huko Mahakama Kuu dhidi ya hukumu ya kisanii ya ICC.

Kama ulivyosema, suala la Richmond kuhamishia mkataba wake Dowans bila kupata ridhaa ya kimaandishi kutoka TANESCO ni kinyume cha kifungu 15.12 cha mkataba kati ya Richmond na Tanesco. Nadhani hapa tayari Richmond walikuwa wamekiuka mkataba.

Uozo ni mwingi sana, na unatia hasira sana.

Hizo walizoiba za EPA, Kagoda, Deep Green na nyinginezo haziwatoshi tu hadi waibe na hizi??? Arghhhhh....

This is the beginning of their end.

Tunisia, Egypt, then Tanzania...

Down with the corrupt tyranny!!!


Kweli.. usisahau kuwa mojawapo ya sababu za supplier kudefault ilikuwa ni 12.1e ya Mkataba yaani kuassign mkataba kwa mtu mwingine bila consent ya Tanesco. Hiki kifungu ni muhimu sana kukishikilia kwani ndicho kilichosababisha Richmond kutafuta njia ya uongo baada ya siku 30 kupita kujaribu kusahihisha makosa yao.
 
MKJJ,

..kuna kitu nime-notice kinajitokeza tena sasa hivi.

..raia mwema wameripoti kwamba taarifa iliyotolewa na Chiligati ni kinyume na majadiliano na msimamo wa kikao cha CCM-CC.

..pia wakati wa mchakato wa mkataba wa Richmond, Lowassa na Msabaha, walikuwa wanafanya maamuzi yanayokwenda kinyume na msimamo wa baraza la mawaziri.

..wakati ule niliuliza ujasiri wa Lowassa na Msabaha kukiuka maamuzi ya baraza la mawaziri ulikuwa unatoka wapi? nani aliyempa Chiligati ruhusa ya kutoa taarifa inayokwenda kinyume na msimamo wa CCM-CC?

..hivi hawa kina Lowassa,Msabaha,na Chiligati hawana msimamizi?
 
jaman ina maana kamati ya mwakyembe ilituficha mambo mengi sana na bado wao(mwakiyembe na sita) wakaacha kututetea wakati wa hii hukumu! Sasa kelele ni za nini kwenye vyombo vya habari kwa,ba kampuni ni za kitapeli alafu hawapeleki evidence concrete kama hizi?!
 
jaman ina maana kamati ya mwakyembe ilituficha mambo mengi sana na bado wao(mwakiyembe na sita) wakaacha kututetea wakati wa hii hukumu! Sasa kelele ni za nini kwenye vyombo vya habari kwa,ba kampuni ni za kitapeli alafu hawapeleki evidence concrete kama hizi?!

Kamati ya Mwakyembe kama ilivyokuwa Tanesco ilikuwa inaangalia ushahidi ulioletwa mbele yake. Watu pekee waliokuwa wanajua kilichokuwa kinaendelea kati ya Dowans na Richmond walikuwa ni hao wawili. Hata Kamati Teule ilipofanya kazi yake haikuwa inajua hili ambalo tumelijulisha sasa; as a matter of fact bila Richmond/Dowans kufanya blunder ya kihistoria huko Marekani tusingejua kabisa. Kina Mwakyembe na Sitta wamejua hili masaa machache kabla ya mkutano wa Wabunge wote wa CCM.
 
well well well!..................sasa tusubiri feedback...............
 
Kama Kikwete ataendelea kuwa rais wa hii nchi basi ndio mtaelewa kwamba watanzania ni mbumbumbu. Mawaziri et al wapo wapo tu kuangalia matumbo yao hakuna uwajibikaji. Misri hivi sasa wanaangalia jeshi lichukue nchi na kumwondoa Mubarak sisi je ni nani wa kumtegemea kumwondoa JK? Hayupo pale kwa niaba ya Watanzania bali kwa niaba ya m a b a s h a wake ambao anawatumikia. Anaendelea kumlinda Mkapa ambaye aliiba na kufanya biashara Ikulu. Anaendelea kumlinda RA ambaye ni partner wake kwenye kampuni ya Dowans, pamoja na Sin bin clair aliyepora kila eneo la madini nchini. Viongozi ambao wana uchungu na hii nchi pamoja na wabunge ni jukumu lao kuona kwamba keki ya taifa hailiwi na mafisadi papa ambao wameingia Ikulu kwa njia ya Wizi.
 
Kwa taarifa hii kwa kweli mafisadi wanakula lakini hivi kwa nini tanesco walisaini huo mkataba naomba nielimishwe ninavyoelewa ni kwamba wataalamu hutoa ushauri wa kitaalamu na
 
Kwa taarifa hii kwa kweli mafisadi wanakula lakini hivi kwa nini tanesco walisaini huo mkataba naomba nielimishwe ninavyoelewa ni kwamba wataalamu hutoa ushauri wa kitaalamu na

Wizara ilitaka wasaini
 
Kama Mwakyembe na Sitta walikuja kulifahamu hili kabla ya kikao cha wabunge wa CCM basi ni good news. nilidhani labda hii issue bado haijafikishwa kwa wawakilishi wa wananchi, na hiyo ingekuwa hatari.
 
Kama Mwakyembe na Sitta walikuja kulifahamu hili kabla ya kikao cha wabunge wa CCM basi ni good news. nilidhani labda hii issue bado haijafikishwa kwa wawakilishi wa wananchi, na hiyo ingekuwa hatari.

GN, hivi unafikiri ni rahisi kwa wabunge wa CCM kwendaa kinyume na Kamati Kuu. KK walikuwa wanategemea wabunge wangeendorse their position... tatizo ni hii taarifa.
 
hii iabidi niipitie kwa umakini! hii ishu inarudishwa bungeni? Na kina hasa? Mwakyembe na Sitta wana uwezo wa kudefile rank?
 
Fragmitation for all this is really bady and Nataka kulia kabisa kwa hili kaka maana sisi Watanzani ni watu wa aina gani
 
Tatizo ni kuwa ukweli husimama wenyewe; hukodoa macho kama simba mwenye njaa; huvuta mwitiko. Huwezi kuupuza ukweli au kuukataa daima kwani ukweli una tabia yake nyingine - hauondoki kwa sababu haukubaliwi. Hubakia kama shahidi asiyelala kujishuhudia wenyewe.
 
Tatizo ni kuwa ukweli husimama wenyewe; hukodoa macho kama simba mwenye njaa; huvuta mwitiko. Huwezi kuupuza ukweli au kuukataa daima kwani ukweli una tabia yake nyingine - hauondoki kwa sababu haukubaliwi. Hubakia kama shahidi asiyelala kujishuhudia wenyewe.

Na kwa watawala ukweli huwa mchungu, wa ghali sana. Kama inavyojidhihirisha sasa kupitia Dowans, na kama ule wa EPA ulivyowakodolea macho. Katika jitihada za kujaribu kuficha ukweli gharama kubwa sana hutumika, bila mafanikio. Ni muda na pesa kiasi gani zimetumika katika kujitahidi kuficha ukweli wa EPA na Dowans, Kiwira, RITES, etc.
 
Did a bit of research and thought I would share. Positions of experts in the area of arbitration.

By far the most important international instrument on arbitration law is the 1958 New York Convention on Recognition and Enforcement of Foreign Arbitral Awards.

• Generally speaking, by their nature, arbitration proceedings tend not to be subject to appeal, in the ordinary sense of the word.
• However, in most countries, the court maintains a supervisory role to set aside awards in extreme cases, such as fraud or in the case of some serious legal irregularity on the part of the tribunal. (can misrepresentation be argued to constitute fraud – i.e under the concept of fraudulent misrepresentation – such that the assignment carried out without TANESCO's knowledge and approval be claimed as such?) Or better to claim contract uberrimae fidei which is a contract of ‘utmost good faith'. Similarly to fiduciary relationships, the parties are required to make known all material facts influencing a contract. As such, had TANESCO been notified of the assignment having been executed prior to their consent, they could, at their option have terminated the agreements.)
• Only domestic arbitral awards (i.e. those where the seat of arbitration is located in the same state as the court seised) are subject to set aside procedure.

In the recognition and enforcement of arbitral awards, the arbitral process is reliant upon national systems of law. This is the classic example of what Lord Mustill meant when he referred to the relationship between the national courts and arbitration being like a relay race. The arbitral tribunal, whilst having sufficient powers to make the award, has no coercive powers to force a reluctant party to comply with the award. This is where the national court system takes up the baton.

Before considering recognition and enforcement in detail, it is worth just mentioning the limited scope of the ability to challenge an award by way of appeal in the seat of arbitration. In considering whether or not it is possible to challenge an arbitral award, it is necessary to look at the applicable Rules of Arbitration, as well as the law of the seat of arbitration. Each state has its own concept of the level of control it wishes to exercise over the arbitral process, and this can vary (as well as distinguish between domestic and international arbitration). If the seat of the arbitration is London, the appeal is to the Commercial Court of the Queen's Bench Division of the High Court of Justice; if it is in France, it is to the Cour D'Appel, Paris; and if in Switzerland, it is to the Swiss Federal Tribunal.

Challenges to awards by way of an appeal are difficult to make; and, purposefully so, as the decisions of arbitrators are meant to be final and binding. Having said that, in the case of Shell Egypt West Manzala GmbH & Anor v Dana Gas Egypt Ltd {2009}the English High Court held that the UNICTRAL Rules that provide for "final, conclusive and binding" does not exclude the possibility of appeal on a point of law.

This is because the legal system recognises that the parties have decided that they are to be bound by the decision of the arbitrators as an alternative to the national court. The law, therefore, gives effect to the intention of the parties and enforces the award just as it would a national court judgment. The House of Lords decision in Lesotho Highlands Development Authority v Impregilo SpA and other clarifies the basis on which arbitral awards may be challenged in the English courts and affirms the underlying policy of the English Arbitration Act 1996, which is to reduce court intervention in the arbitration process to a minimum.

Hilo jopo la mawakili preparing to take on this matter have their work cut out. Issue as raised by Mhe Mwanakijiji regarding the assignment pre- TANESCO approval is the obvious start point. Kwa kweli sioni point nyingine. Issues nyingine zote zimekuwa dealt with na the arbitration.
 
Trader, aisee asante sana nimekusoma vizuri kweli. Na ninaweza kuwa:

a. Kusema kuwa mkataba unasema hakuna "appea" haina maana kuwa it is absolutely impossible to appeal kama ambavyo wanasiasa wamekuwa wakizungumzia hili.

b. Kukiwa na point nzuri ambayo inahusiana moja kwa moja na matokeo ya hukumu inawezekana kusue. Kwa hiyo naamini kubwa linalohitajika ni kuonesha precedence ya kesi ambazo zilikuwa zimeshatolewa hukumu katika arbitration lakini zikakatiwa rufaa.

THanks.
 
Mkuu Trader, nimejitutumua kuelewa hiyo lugha ya kisheria uliyoandika na ninapenda kuamini kwama nimeelewa sahihi. Nakushukuru kwa utafiti wako na mawazo yako. Hata hivyo najaribu kujitahidi kukubaliana na wewe lakini bado yafuatayo yananitatiza;

1. Ninaposoma bandiko lako inakuwa kama nasikiliza marudio ya kauli za Ngeleja na Werema kwamba kwa mujibu wa sheria ni lazima tulipe hiyo tuzo vinginevyo?

2. Lakini pia ninasikia sauti za akina Mwakembe na Sita kwamba mahali pa kutokea pako wazi, uhalali wa kampuni na mkataba kuhamishwa

3. Pia nasikia sauti za wanaharakati wanasheria kwamba kuna uwezekano kabisa wa kupinga hiyo tuzo na kushinda.

4. Mwisho nasikia sauti za wananchi na wabunge kwamba tusilipe chochote kwani siyo deni ambalo ni kipaumbele katika madeni yote ya ndani na nje.

Kwa hiyo naomba niahirishe kukubaliana na wewe hadi wanasheria wote, viongozi na wananchi watakapozungumza lugha moja, kwamba hiyo hukumu hatutakiwi kisheria kukata rufaa. Nasikitika sana.
 
Back
Top Bottom