Jinsi Richmond/Dowans walivyoizunguka TANESCO NA TAIFA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Richmond/Dowans walivyoizunguka TANESCO NA TAIFA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 26, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  UJASIRI WA UFISADI

  Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development wa tarehe 23 Juni, 2006 wa kuingiza majenereta ya umeme kufuatia upungufu wa nishati hiyo uliokuwa umekithiri nchini mwaka 2006 ulihamishiwa kwa kampuni ya Dowans Holdings S.A tarehe 14 Oktoba, 2006 mwezi mmoja kabla bila ya kuihusisha TANESCO kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa kifungu 15.12 cha mkataba huo.

  Kifungu hicho cha Mkataba kilikuwa kinaruhusu mkataba huo uliokuwa na thamani ya dola milioni 172.5 kuahulishwa kwenda kwenye kampuni nyingine baada ya makubaliano ya pande hizo mbili tena kwa maandishi.

  Sehemu ya kifungu hicho cha mkataba huo ambao FP inao kinasema wazi kuwa "Neither party may assign this agreement or grant any security interest, charge, lien, or other encumbrance in this Agreement other than by mutual agreement between the parties in writing". Kwa maneno mengine, mkataba ulikataza pande zote mbili (TANESCO na RDC) kuhaulisha jukumu lolote au jambo lolote linalohusiana na mkataba huo kwenda kwa kampuni au chombo kingine pasipo makubaliano ya maandishi kati ya pande hizo mbili.

  Hivyo kitendo chochote kwa upande wa TANESCO au Richmond kuhamisha mkataba au majukumu yake kwenda kwa chombo kingine bila ridhaa ya kimaandishi ya mwenzake ilikuwa ni uvunjaji wa mkataba huo. Hata hivyo, katika taarifa ambazo Kamati Teule iliyoundwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchunguza Richmond ilipatiwa chini ya kiapo kampuni ya Richmond ilihamisha mkataba wake kwa Dowans Holding S.A tarehe 23 Disemba, 2006.

  Mlolongo wa matukio kwa mujibu wa ripoti ya Kamati teule hadi kufikia RDC kuhamisha unaonesha kuwa Shirika la Ugavi wa Umeme la Tanzania lilifichwa ukweli wa kilichokuwa kinaendelea kwani haikujua kuwa wakati wote inafikiria ugumu wa kuhamisha mkataba huo kwenda Dowans kampuni ya Richmond tayari ilikuwa imeshauhamisha mkataba huo.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyosomwa kwa kile kilichodaiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa kuwa ni "kwa mbwembe" inaonesha kuwa TANESCO waliandikia RDC barua tarehe 27 Oktoba, 2006 ya tahadhari kuwa RDC ilikuwa inaonesha kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba (default notice) iliyotaka majibu kufuatia mapungufu kadhaa ambayo TANESCO waliyaona. Ripoti hiyo inasema kuwa kwa mujibu wa TANESCO mapungufu hayo yalikuwa ni pamoja na "kushindwa kwa kampuni hiyo kusafirisha angalau mtambo wa kwanza wa wastani wa unit 22 kW kuja Tanzania; kushindwa kwa kampuni hiyo kutoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya utekelezaji wa mradi; uwepo wa kampuni hiyo Marekani kihalali; uwezo wa kampuni hiyo kitaalamu na kifedha kuweza kutekeleza Mkataba huo wa umeme wa dharura katika muda muafaka."

  Lengo la taarifa hiyo ilikuwa ni kutaka majibu kutoka RDC ya kwanini TANESCO isione kuwa Richmond wameshindwa kazi na hivyo kuvunja mkataba. Barua hiyo ya tahadhari haikujibiwa. Kwa mujibu wa Ripoti ya Mwakyembe shirika la TANESCO likaandika barua nyingine za tarehe 17 na 23 Novemba, 2006 "kuikumbusha (Richmond) kuhusu hoja zake za awali (za barua ya Oktoba 27, 2006) ambazo hazikujibiwa na kudai maelezo kuhusu taarifa za kwamba kampuni hiyo haikuwa na mahusiano na Pratt & Whitney iliyotegemewa sana kubeba sehemu kubwa ya majukumu ya mradi."

  Hata hivyo barua zote hizo tatu hazikujibiwa wala hoja zilizoibuliwa na TANESCO kupewa majibu yenye ushawishi wa ukweli na mvuto wa kiakili. Na siku hiyo ya Novemba 23, 2006 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO alijieleza kwa Waziri juu ya tatizo lililokuwa linaonekana kuhusu uwezo wa Richmond. Tarehe 28 Novemba, 2006 yaani siku tano baada ya barua ya Mkurugenzi wa TANESCO Waziri wa Nishati Bw. Nazir Karamagi alimpigia simu aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Balozi Fulgence Kazaura kumtaarifu kuwa kampuni ya Richmond ilikuwa inakusudia kuhaulisha mkataba wake kwenda kampuni "nyingine" na hivyo alitaka kujua kama mkataba uliruhusu uwezekano huo.

  Ripoti ya Mwakyembe inasema kuwa "Tarehe hiyo hiyo 28 Novemba 2006 uongozi wa TANESCO ulimshauri Mwenyekiti wa Bodi kama ifuatavyo:- (i) Mkataba kati ya Richmond Development Company LLC na TANESCO hauruhusu kukabidhi majukumu ya Mkataba kwa Kampuni nyingine isipokuwa kwa maafikiano ya pande mbili za Mkataba (Kifungu 15.12)." Tarehe 4 Disemba, 2006 (chini ya siku kumi tangu Karamagi adokeze nia ya Richmond kuhamisha mkataba) TANESCO walipokea barua kutoka Richmond ambayo ilionesha kuwa kampuni hiyo ilitaka "kutumia haki yake chini ya Kifungu 15.12 cha Mkataba ili kuhamisha majukumu yake yote ndani ya Mkataba huo kwenda kwa DOWANS Holdings, S.A. Aidha, Richmond Development Company LLC ilieleza kwamba tarehe ambayo TANESCO itaridhia mapendekezo hayo iwe ndiyo tarehe rasmi ya kuhamisha mafao na majukumu yote kwa DOWANS Holdings, S.A na kwamba DOWANS Holdings, S.A itawasilisha vielelezo vya utambulisho wake kwa TANESCO"

  Hata hivyo, barua hiyo ambayo TANESCO waliipokea Disemba 4, inaonesha kuwa iliandikwa Novemba 9, karibu mwezi mmoja kabla. Siku moja kabla ya kupokea barua ya Dowans kutaka kuhamishia mkataba wake kwa Dowans yaani tarehe 8 Disemba, 2009 TANESCO ilikuwa imeiandikia Benki ya Citibank isaidie kufanya uchunguzi wa kujua kampuni ambayo Richmond ilikuwa inataka kuhamishia mkataba wake ilikuwa ni kampuni gani na yenye uwezo gani kwani "la "kwani japokuwa masharti ya Mkataba yanaruhusu Mkataba kuhamishwa, TANESCO ingependa kufahamu hasa ni nani anayehamishiwa Mkataba huo"

  Kamati Teule haikufanikiwa kupata majibu ya Citibank ila iliambiwa kulikuwa na shinikizo toka Wizarani "kuwa viongozi wa Wizara kama kawaida yao waliishinikiza TANESCO kukubaliana na ombi la Richmond Development Company LLC la kuhamisha mkataba." Ni kutokana na hilo tarehe 21 Disemba, 2006 TANESCO ikaiandikia kampuni ya Richmond kukubali uhaulishaji wa mkataba huo kwenda kwa Dowans kwa barua yenye SEC. 388/12/206 ambapo pamoja na mambo mengine ilitaka "ipate hati ya uthibitisho kutoka Dowans Holdings, S.A ya kuridhia uwajibikaji kamilifu katika kutekeleza Mkataba wa tarehe 23 Juni, 2006, kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC."

  Hivyo tarehe 23 Disemba 2006 Mkataba ukaingiwa kati ya TANESCO na Dowans S.A ambao ulikuwa ni kuhamishia mkataba kati ya TANESCO na Richmond kwenda kwa Dowans Holdings S.A.

  Kwa mujibu wa ripoti ya Kamati Teule kusainiwa kwa mkataba huo kati ya TANESCO na Dowans Holding S.A kulileta mambo matatu muhimu ; kwanza, "Tarehe 23 Disemba 2006 ndiyo siku rasmi ambayo Richmond Development Company LLC imekabidhi rasmi majukumu yake ya utekelezaji wa Mkataba kati yake na TANESCO kwa Dowans Holdings S.A"; Pili, "Dowans Holdings, S.A itatekeleza majukumu ya Mkataba uliotiwa saini kati ya TANESCO na Richmond Development Company tarehe 23 Juni, 2006 kwa masharti yote kama yalivyo katika Mkataba"; na tatu, "Malipo halisi na madeni ndani ya Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC, sasa yatakwenda kwa Dowans Holdings, S.A kuanzia tarehe 23 Disemba, 2006."

  Hata hivyo kulikuwa na tatizo; Richmond Development Corporation LTD ilikuwa tayari imeshahamisha mkataba wake na TANESCO kwenda kwa Dowans miezi karibu miwili nyuma. Yaani, RDC iliingia mkataba na Dowans Holdings S.A tarehe 14 Oktoba, 2006 bila ya kushirikisha, kutaarifu au kwa namna yoyote ile kupata maridhiano ya kimaandishi toka kwa TANESCO kinyume cha kipengele cha 15.12 tulichokiona hapo juu.

  Hii ina maana kuwa mazungumzo yote yaliyofuatia hadi TANESCO kukubali kuwa Richmond ihamishe mkataba kwenda kwa Dowans SA katika barua ya Disemba 21, 2006 yalikuwa ni kanyaboya, au danganya toto kwani wakati TANESCO inaingia ikiamini (in good faith) kuwa Richmond ilikuwa bado haijahaulisha mkataba kwa Dowans, Dowans iliingia ikijua kuwa tayari imekwisha fanya hivyo.

  Kampuni ya Richmond ilihamisha mkataba wake kwenda Dowans tarehe 14 Oktoba, 2006 ikikabidhi majukumu yake yote iliyokuwa imekubaliana na TANESCO kwenda kwenye kampuni hiyo inayodaiwa kuwa ni ya Costa Rica. Mkataba huo uliingiwa kabla tu ya mitambo ya kwanza kusafirishwa kwa ndege kupelekwa Tanzania. Siku hiyo hiyo wakati Richmond inahamisha mkataba wake wa Juni 23, 2006 na TANESCO kwenda Dowans Holdings S.A ilihamisha vile vile mkataba wake wa Septemba 25, 2006 kati yake na Vulcan (Vulcan Advanced Mobile Powers Systems, LLC na Vulcan Power Group, LLC) wa ununuzi wa mitambo toka kampuni hiyo kwenda kampuni ya Dowans Holdings S.A.

  Ni muhimu kutaja kuhamishwa kwa mkataba wa Richmond na Vulcan kwenda Dowans S.A kwa sababu mara baada ya mkataba huo kuhamishwa kwa Dowans S.A kampuni hiyo ililipa Vulcan dola milioni 7.5 na ikanunua mtambo wa kwanza wa gesi ambao uliingizwa nchini mwishoni mwa 2006 na kupokelewa kwa shangwe. Wakati baadhi ya magazeti yaliripoti kuwa "mitamo ya Richmond yawasili" ukweli ni kuwa mitambo hiyo ilikuwa ni ya kampuni ya Dowans Holdings S.A ambayo ndiyo ilinunua na kugharimia kuingizwa kwake nchini.

  Hili hata hivyo linaleta matatizo makubwa mawili ya kisheria ambayo yote yanahusiana na malipo ya shilingi bilioni 94 ambayo kampuni ya Dowans S.A inatarajiwa kulipwa siku chache zijazo kufuatia hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (International Court of Arbitration). Tatizo la kwanza ni kuwa wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Nazir Karamagi alipozungumza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Balozi Fulgence Kazaura Novemba 28, 2006 kuulizia kama mkataba wa Richmond unaruhusu kuhamishwa kwenda kampuni nyingine, kampuni ya Richmond ilikuwa tayari imekwisha hamisha mkataba huo kisheria kwenda Dowans Holdings S.A.

  Hii ina maana kuwa yote yaliyofuatia hapo hadi baadaye TANESCO kukubali kuhamisha mkataba kwenda Dowans kwa barua yake ya Disemba 21, 2006 yalikuwa ni mazingaombwe tu ya kujaribu kutimiza matakwa ya kifungu cha 15.12 cha mkataba wa Richmond na TANESCO kama tulivyoona hapo juu. Ilikuwa ni muhimu kwa Richmond kutimiza kifungu hicho kwa sababu vinginevyo mkataba kati yake ya Dowans usingekuwa halali kwani ungekuwa umehaulishwa kinyume cha makubaliano.

  Hili linatuleta kwenye kuelewa kwanini jitihada zote za TANESCO kuitaarifu Richmond kuwa ilikuwa inaelekewa kushindwa kutekeleza mkataba hazikuzaa matunda. Inafafanua kuwa kwanini barua za Oktoba 27, Novemba 17, 23 na 29 kwenda kwa Richmond hazikujibiwa na badala yake maelekezo ya Waziri Karamagi (Novemba 28, 2006) kwa Kazaura kuwa "Richmond Development Company LLC walikuwa wanataka kuhamisha majukumu yao yaliyobaki katika Mkataba wa uletaji mitambo na uzalishaji umeme wa dharura kwa kampuni nyingine." Majibu yaliyotolewa siku ile ile kwenda kwa Waziri kuwa " Kifungu cha 15.12 cha Mkataba huo hakiruhusu kukabidhi majukumu ya Mkataba kwa Kampuni nyingine isipokuwa kwa maafikiano ya pande mbili za Mkataba." Hili lilithibitisha tatizo ambalo Richmond waliligundua baada ya kuingia mkataba na Dowans Oktoba 14, 2006 bila kuwashirikisha TANESCO. Hivyo, mpango wa "kuwashirikisha TANESCO" ukaingizwa na hatimaye TANESCO wakakubali na "mkataba" ukahamishwa "rasmi" kwenda Dowans Disemba 23, 2006 kama Ripoti ya Mwakyembe ilivyoonesha. Hii ina maana Richmond ilivunja mkataba na TANESCO pale ilipoamua kuhamisha mkataba wake huo kwenda kwa Dowans Oktoba 14, 2006 bila ya ridhaa, ushauri, makubaliano ya kimaandishi kati yake na TANESCO kama kipengele cha 15.12 cha Mkataba kilivyotaka.

  Richmond ilijua kuwa imefungwa na kipengele kingine ambacho kiliweka wazi kuwa endapo ingehamisha mkataba huo bila ya kuihusisha TANESCO basi itakuwa imejiingiza matatani. Kipengele hicho ni cha 12.1e ambacho ni sehemu ya mambo ambayo yatafanya Richmond kuwa imeelekea kushindwa kutekeleza mkataba. Hivyo, Richmond ilikuwa haina jinsi nyingine kwa sababu isingeweza kuiambia TANESCO kuwa tayari imeingia mkataba na Dowans kwani itakuwa ni sababu tosha kwa TANESCO kuvunja na isingeweza kuvunja tena na mkataba na Dowans S.A kwani tayari Dowans walishaingia gharama za kununua majenereta toka Vulcan. Njia rahisi ilikuwa kuanzisha mazingaombwe ya "kuhaulisha mkataba kwenda kampuni nyingine".

  Hili hata hivyo linatuingiza kwenye tatizo kubwa la pili ambalo linahusiana moja kwa moja na malipo ya Bilioni 94 kwenda Dowans S.A siku chache zijazo. Kesi iliyoamuriwa na ICC-ICA ilizingatia kati ya mambo mengi uhalisia na uhalali wa mkataba wa Dowans. Sehemu kubwa ya hukumu hiyo ilishughulikia ukweli kuwa mkataba uliokuwa umeingiwa na TANESCO na Dowans wa Disemba 23, 2006 ulikuwa ni halali. Katika hukumu hiyo kilichoangaliwa ni makubaliano ya kuhamisha mkataba kutoka kwa Richmond kwenda Dowans Holdings S.A kama yalivyoanzishwa na mawasiliano ya simu kati ya Waziri Nazir Karamagi (akiwa Calgary, Canada) kwenda kwa aliyekuwa mwenyekiti wa bodi Balozi Kazaura Novemba 28, 2006.

  Kuna mambo ambayo tuna uhakika nayo na ambayo ni msingi wa hatimaye kukataa kuwalipa Dowans S.A na Dowans Tanzania Limited tuzo iliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC). Mambo yafuatayo ni ya kuzingatia.

  1. Wakati Karamagi anawasiliana na Kazaura kuulizia kama mkataba wa Richmond/TANESCO unaruhusu kuhamishika alikuwa tayari na taarifa kuwa Richmond walikuwa tayari wameshahamisha mkataba kwenda Dowans, SA Oktoba 14,2006 (mwezi mmoja na nusu kabla)
  2. Majibu ya TANESCO siku ile ile kwenda kwa Kazaura ikitaja uwepo wa kifungu cha 15.12 kwenye mkataba kinachozuia kuhaulisha mkataba bila ya ridhaa ya maandishi toka kwa TANESCO inatuonesha kuwa TANESCO walikuwa hawajui kuwa Richmond walikuwa tayari wamehamisha mkataba wao kwenda Dowans Holdings S.A Oktoba 14, 2006
  3. TANESCO wakiwa wamepewa jina la kampuni iliyokusudiwa kuhamishiwa mkataba ya Dowans S.A wanawasiliana na wawakilishi wa kampuni hiyo ili kupata taarifa za uwezo na uhalisia wa kampuni hiyo kuweza kuchukua mkataba. Na wanawaandikia barua Citibank ili iwasadie kufanya uchunguzi wa uhalisia na uwezo wa kampuni hiyo. Barua hiyo inaandikwa Novemba 8, 2006. Barua hiyo aidha haijibiwi au hakuna ushahidi wa kuwepo kwa majibu yake.
  4. Novemba 9, 2006 kampuni ya Richmond wanawaandikia barua rasmi TANESCO kuwajulisha nia yao ya kutaka kuhamisha mkataba kwenda kampuni nyingine wakitumia haki yao ya kifungu cha 15.12 cha Mkataba. Hii ndiyo barua ambayo inawafikia TANESCO Disemba 4, 2006. Hapa kuna jambo la kutafakari kidogo. Kwanini barua iliyoandikwa Novemba 9, 2006 iwafikie TANESCO Disemba 4, 2006? Yawezekana iliandikwa baada ya kugundua kuwa mkataba umeshahamishwa kwa Dowans S.A Oktoba 14, 2006 lakini TANESCO hawakuwa na taarifa hivyo walihitaji kutengeneza mazingira ya taarifa?
  5. Pendekezo la nne hapo juu linaonekana lina ukweli kwa sababu ni tarehe 28 Novemba, 2006 ndipo Karamagi anaulizia kama mkataba unaruhusu kuhamishika; na anapoambiwa kuwa haiwezekani isipokuwa kwa ridhaa ya pande zote mbili chini ya kifungu 15.12 ndipo siku sita baadaye (Disemba 4, 2006) barua iliyoandikwa Novemba 9, 2006 inafika TANESCO ikiwa na nia ya ya kuhamisha mkataba chini ya haki za 15.12. Barua hiyo ya Richmond ilisema kuwa kampuni iliyokusudiwa ilikuwa ni Dowans S.A na kuwa kampuni hiyo mpya itajitambulisha yenyewe kwa TANESCO.
  6. Novemba 14, 2006 Dowans S.A inawaandikia TANESCO ikijitambulisha kuwa ndiyo kampuni ambayo imekusudiwa kurithi mkataba wa Richmond na TANESCO. Wakati Dowans S.A inaandika barua hii tayari ilikuwa imeshaingia mkataba na Richmond Oktoba 14, 2006. Lilikuwa jukumu la Richmond na Dowans S.A kuitaarifu TANESCO kuwa mkataba umekwishachukuliwa. Hilo hata hivyo lingekuwa kinyume na kifungu cha 15.12. Dowans iliandika barua kana kwamba ilikuwa haijachukua mkataba huo bado na hivyo kudanganya ili kupata faida ya aina fulani kinyume na sheria yetu ya Mikataba ya 2002. Kuna mambo ambayo TANESCO ingeweza kujua kuhusu kampuni ya Dowans lakini suala la kuwa ilikuwa tayari imekwishaingia mkataba lilikuwa ni suala la kujulishwa na Richmond au Dowans wenyewe. Ni sawasawa na mtu ambaye kwa muda wote wa uchumba na hatimaye siku ya harusi anafunga ndoa akiamini kuwa anayefunga naye ndoa hakuwa tayari amefunga ndoa na mtu mwingine ambayo ilikuwa bado halali kisheria. Ndoa inaweza kufungwa lakini endapo ikaja kujulikana kuwa yule mwingine alificha ukweli kuwa tayari alikuwa katika ndoa halali basi ile ndoa ya pili inafutiliwa mbali (annulled) kwani haikuwahi kuwepo.
  7. Barua ya Dowans ya Disemba 8, 2006 inaondoa shaka kabisa kuwa Dowans waliwaficha TANESCO ukweli kuwa tayari kampuni ya Costa Rica ilikuwa tayari imekwisha funga "ndoa" na Richmond kuchukua mkataba wake na TANESCO bila ridhaa ya kimaandishi na TANESCO. Barua hii kwa mujibu wa hukumu ya ICC (kifungu cha 517) iliomba kibali cha kuhamisha mkataba na kutoa taarifa mbalimbali kuhusu kampuni hiyo na kampuni ya Portek Group.
  Ni kutokana na mabo hayo hapo juu ndipo tunaona makosa makubwa ya hukumu ya ICC. Hukumu hiyo kifungu cha 518 ambacho kinatupilia hoja ya "kutokuwa wa kweli" iliyotolewa na TANESCO dhidi ya Dowans inadai kuwa yote yaliyosemwa kwenye barua hayo yalikuwa ni kweli (factual). Hukumu hiyo inasema kuwa "based on the evidenced presented before the Tribunal, all these (yale yaliyodaiwa kwenye barua ya Disemba 8, 2006) representations were proven to be factual – what the letter of 8 December purpoted to present was actually in the dossier accompanying the letter. This is substantiated by the fact that the Tribunal was presented with evidence that DHSA and RDVECO requested the consent of TANESCO to the assignment (of the contract)"

  Hukumu hiyo ikadai katika kifungu cha 519 kuwa "based on the evidence adduced before the Tribunal these representations presented in the dossier of 8 December 2006 were statements of fact, were true". Yaani, " kulingana na ushahidi uliotolewa katika mahakama yaliyosemwa katika barua ya Disemba 8, 2006 yalikuwa ni madai ya uhakika, yalikuwa kweli".

  Ni kutokana na msimamo huo wa mahakama hiyo hoja kuwa Dowans haikuwa mkweli wakati inataka kuchukua mkataba wa Richmond ilitupiliwa mbali katika kifungu cha 524. Baada ya kutupilia mbali hoja hiyo kwa makosa mahakama hiyo ikaangalia kile ilichoamininishwa kuwa ndio makubaliano ya kuhamisha mkataba toka Richmond kwenda Dowans.

  Katika kifungu cha 533 cha hukumu hiyo inaoneshwa kuwa kulikuwa na makubaliano ya kuhamishia mkataba kati ya TANESCO na Richmond kwenda Dowans kwa barua iliyoandikwa Disemba 21, 2006 (kama tulivyoona hapo juu). Na hili lilikuwa kweli kwani ni tarehe 23 Disemba, 2006 mkataba huo ukapelekwa kwa Dowans. Na hata uamuzi wa baadaye wa TANESCO kukubali mkataba uhamishiwe toka Dowans S.A kwenda Dowans Tanzania Limited ulitegemea uhalali wa kitendo cha Disemba 21 na 23, 2006.
  Hili linaturudisha kwenye hoja ya msingi kabisa ambayo inatufanya tuulize maswali yafuatayo:

  1. Kama Richmond ilikuwa tayari imeshahamisha mkataba wake na TANESCO kwenda Dowans S.A Oktoba 14, 2006 ni kitu gani kilikuwa kinafanyika kwa majadiliano ya kuanzia Novemba 9 hadi TANESCO kukubali kuhamishwa mkataba Disemba 21, 2006?
  2. Richmond ilipowasiliana na TANESCO kueleza nia yake ya kutaka kuhamisha mkataba kwenda Dowans wakati tayari ilikuwa tayari imeshauhamisha mkataba huo kisheria kwanini haikuweka wazi jambo hilo kwa TANESCO kama kifungu cha 15.12 kinavyotaka?
  3. Kampuni ya Dowans S.A ililipia na kuingiza mitambo ya kuzalishia umeme mwishoni mwa Oktoba 2006 baada ya kufanya hivyo ikiamini inatekeleza makubaliano yake na Richmond ya Oktoba 14, 2006 yaliyohusisha kurithi mkataba wa TANESCO na ule wa Vulcan. Kwa maneno mengine, Dowans ilianza kutekeleza mkataba wake na Richmond ikiamini ilikuwa inatekeleza mkataba wa TANESCO. Kwanini, Dowans haikuiambia TANESCO kuwa imechukua mkataba kutoka Richmond na badala yake kutenda kana kwamba ilikuwa haijapata mkataba huo bado?
  4. TANESCO isingeweza kujua kwa namna yoyote ile kuwa Richmond imeshaingia mkataba na Dowans Oktoba 14, 2006 isipokuwa kwa kuambiwa na Richmond yenyewe na Dowans S.A. Ni kwa sababu hiyo uongozi wa TANESCO ulijitahidi kuzuia mkataba kuhamishwa lakini wakajikuta "wanasukumizwa" na Wizara na hatimaye kukubali. Ukweli ni kuwa TANESCO hawakuwa na njia nje ya hapo kwani mkataba tayari ulikuwa umeshahamishwa.
  Kutokana na haya yote ambayo tunayo sasa hivi na tunayajua kwa uhakika ni kitu gani kinahalalisha kuwalipa kampuni ya Dowans S.A? Kwa vile tayari wamekwishalipwa zaidi ya bilioni 100 hadi hivi sasa na bado majenereta ni yao na kuna dalili kuwa wanapanga kuyakodisha tena kwetu kupitia kampuni nyingine ni wazi kuwa ni viongozi gani wenye dhamira safi katika Tanzania wanaoweza kuhalalisha malipo ya bilioni 94 zaidi? Mkataba wenyewe wa miaka miwili ulikuwa ni wa bilioni 172.5 (japo majenereta yenyewe kuyanunua moja kwa moja ilikuwa chini ya bilioni 60) na tukilipa bilioni 94 kama ilivyoamuriwa na serikali ni wazi kuwa kampuni ya Dowans S.A na washirika wake watakuwa wamekomba zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa majenereta ya bilioni 60! Hiki ni kilele cha ufisadi, ni kutamalaki kwa uzembe na kutukuzwa kwa kutokuwajibika.

  Kutokana na uzito wa ushahidi ambao tumeupendekeza mbele ya wasomaji na Watanzania wenzetu tunajikuta tunabakia na mapendekezo yafuatayo tu:

  1. Serikali isilipe hata senti moja na iamue kujitoa kwenye Mahakama ya Usuluhishi na badala yake Bunge letu liimarishe sheria zetu za usuluhishi wa kibiashara ili mikataba yote inayohusiana na umma inapotokea matatizo iamuliwe kwa sheria zetu wenyewe.
  2. Mitambo ya Dowans ambayo tayari tumeshalipia zaidi ya gharama yake kuiingiza nchini ikamatwe na kutaifishwa kwa kutumia madaraka ya Rais (Executive Order) au kwa sheria nyingine yoyote ile.
  3. Watendaji wote wa Dowans S.A na Dowans Tanzania Limited ambao walikuwepo wakati Dowans S.A inarithi mkataba wa TANESCO kutoka Richmond kwenye makubaliano ya Disemba 23, 2006 watimuliwe nchini, watangazwe kuwa ni "watu wasiotakiwa" personae non grata. Wapewe si zaidi ya masaa 24.
  4. Rostam Aziz ambaye ndiye amekuwa kinara wa kuitetea Dowans na ambaye mapema mwaka huu (Januari 5, 2011) alikiri kuwa yeye ndiye aliyewashawishi Dowans kuja nchini na ambaye ndiye aliyepewa nguvu ya kisheria (Power of Attorney) kutumika kwa niaba ya Dowans Holdings S.A alikuwa anajua na alipaswa kuwa anajua kuwa Dowans S.A walikuwa tayari wamechukua mkataba wa Richmond na TANESCO. Akiwa ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye aliapa kulinda na kutetea sheria na Katiba ya nchi yetu alipaswa kuonesha uzalendo kwa kuitaarifu TANESCO (shirika la umma) juu ya jambo hilo. Akiwa ni mtu ambaye angenufaika kwa namna moja au nyingine na uwepo wa Dowans nchini (akiwa ni mshirika na rafiki wa mmoja ya wamilikiwa wa Dowans S.A) Rostam hakuliweka na hadi hivi sasa hajaweka Tanzania mbele katika suala hili. CCM inatakiwa imvue uanachama na serikali imshtaki kwa makosa mengi ambayo tungeweza kuyafafanua kutokana na kushiriki kwake.
  5. Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Nazir Karamagi naye ahojiwe na ikibidi ashtakiwe kwa kushiriki kwake kuificha TANESCO ukweli kuwa mkataba wa TANESCO kuhamishiwa kwa Dowans S.A na Richmond. Bw. Karamagi alijua alipaswa kujua kuwa mkataba ulikuwa umekwishahamishiwa kwenda Dowans kutokana makubaliano ya Oktoba 14, 2006. Kwani, ni yeye aliyetoa taarifa kwa TANESCO juu ya nia ya Richmond kuhaulisha mkataba wake kwenda Dowans S.A na alisisitiza kuwa iwe hivyo licha ya mapingamizi ya Shirika hilo la Ugavi.
  6. Mwanasheria Mkuu wa Tanzania awajibishwe kwa kutetea malipo haya ambayo ni wazi ni kinyume cha sheria.
  7. Huduma yote iliyotolewa na majenereta ya Dowans S.A ichukuliwe kuwa ni huduma ya bure kwani Mkataba uliosainiwa Disemba 23, 2006 haukuwa na maana yoyote kisheria kwani Dowans S.A ilikuwa imekwishajifunga kinyume na kifungu cha 15.12 na Mkataba wake na Richmond wa Oktoba 14, 2006. Ukweli huu uko wazi kwani katika kesi yake dhidi ya Richmond huko Houstona Marekani, Kampuni ya Dowans haitaji kabisa mkataba wa Disemba 23, 2006 bali inatambua kuwa iliingia makubaliano na Richmond ya kuchukua mkataba wa TANESCO tarehe 14, Oktoba 2006.
  8. Watanzania wote wenye dhamiri njema wapinge kwa nguvu na namna zote malipo haya ya kidhalimu na kutaka wale wote waliojitokeza kuyatetea wawajibike wao wenyewe au wawajibishwe na vyombo halali. Malipo haya ni kinyume na maadili, ni ya kimabavu na yanadhalilisha utu wa Mtanzania.

  SWALI PEKEE AMBALO LINAWEZA KUVUNJA HOJA HII WAULIZWE DOWANS S.A na watetezi wa malipo haya haramu ni hili - Ni lini Dowans Holdings S.A. walirithishwa mkataba wa Richmond/Tanesco?


  Kutoka kwenye FIKRA PEVU

  NB:

  NOTISI KWA WAHARIRI:

  Kunukuu habari hii au sehemu yake: "Kwa mujibu wa tovuti mpya ya Fikra Pevu inayomilikiwa na mtandao maarufu wa JamiiForums.com"...

  Nimeongeza Ripoti ya Mwakyembe pamoja na Mkataba wa Richmond/Tanesco maana naona watu wanarudia rudia vitu ambavyo tulivimaliza kuzungumzia miaka mitatu iliyopita.
   

  Attached Files:

 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Time. Time will tell.

  Soon and very soon when the Parliament begins!

  Never before Tanzanians will see fire in the parliament like what they will see in the forthcoming session.

  And guess what from both within and outside CCM. Everybody is tired now.

  Dowans; Katiba Mpya; Mauaji ya Arusha etc are just few to mention.
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  aaah sasa legality ya hiyo hukumu inatoka wapi? Hv jaman tanesco wana lawyers kweli au wakat wa kutoa utetezi wao walioverluku hvo vifungu yan day afta day nackia mambo mapya kuhsu hyo issue. Nategemea kusikia hata hiyo kesi haikuamuliwa huko icc hilo pia possible
   
 4. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  jamani uzalendo kwa watz uko likizo au ulishapigwa ridandas ? Haiwezekani lawyers wa kitz wakasimamie kesi km hii hlf isemekane tanesco wamebwagwa lzm nao wameahidiwa kupata mgao.
  Shame upon them!!!!!!?
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Inategemea kama hao lawyers "wanapata fursa yao kwa wakati muafaka" kufanya kazi yao.
   
 6. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  MM,
  Kama mabadailiko kutoka Richmond kwenda Dowans hayakuwa legal, ina maana kuna possibility ya Tanesco kuikana Dowans? Halafu wengi wetu tumekuwa tukisikia kuwa Richmond ilikuwa ni kampuni hewa kwa maana kwamba ilikuwa mifukoni mwa watu wajanja. Sasa inakuwaje kampuni hewa ihamishie umiliki wake kwa Dowans? Hivi hiyo mahakama ya kimataifa haikuyaona hayo au it was non of their business? Je, hivi kuna uwezekano mahakama ya kimataifa nayo ikawa inapokea rushwa??
   
 7. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Thanks M M Mwanakijiji for useful post.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Mahakama ya Kimataifa inajua yale tu ambayo yanaletwa mbele yake; yaani ushahidi unaoletwa mbele yake. Mahakama haifanyi uchunguzi nje ya ushahidi ulipo pale. Ni jukumu la pande zinazoshtakiana kudisclose information yoyote ambayo ni relevant kwa kesi. Tanesco hawakujua kuwa wakati DG anasaini anaandika barua kuwa Dowans irithishwe mkataba wa Richmond Disemba 21, 2006 wao Dowans na Richmond walikuwa wamekwisharithishana mkataba oktoba 14 na Dowans wameshaanza kutekeleza kwa kulipia mitambo ya Vulcan iliyoingizwa nchini Oktoba mwishoni 2006.

  Dowans walitakiwa kuwaambia ICC kuwa mkataba wake na Tanesco ulirithiwa Oktoba 14. Bahati isingeweza kufanya hivyo kwa sababu ingefichua kuwa ilirithi mkataba bila idhini ya Tanesco.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  MM
  Asante kwa taarifa.Hii issue ya Dowans hii kuna mtu itamuandama hadi kaburini kama wataendelea kuidharau au kuifanyia mzaha. Enough is enough! Tuanze kuogopa kidogo watanzania
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  The most weirdest thing katika huu mjadala wa RICHMOND ambao naona watu wana kila document ni kuwa husikii majina ya:

  1. Tender process ilivyokuwa

  2. TENDER VALUATION ilivyofanywa

  3. Katika Valuation team hakuna anaytajwa

  4. Final report ya Valuation team

  5. Mapendekezo yaliyopelkwa kwa DG wa TANESCO

  6. Majina ya wanasheria wa TANESCO walioridhia haya

  7. Majina ya waliokuwa consulted kule WIZARA YA NNISHATI

  8. Majina ya waliohusika kule WIZARA YA SHERIA


  9. Ushauri wao kwenye hili jambo

  10.Role ya PRIVATE law firms kuishauri TANESCO

  11. Mchanganuo ulivyofanywa mpaka kuwateua hawa private lawfirms na sababu...PPA ilifuatwa na je PPRA waliridhia?

  12.Majina ya hao wahusika from the private law firm

  13. Walilipwa Kiasi gani per hour?

  14. Comments za DG wa TANESCO zilikuwa zipi?

  15. Wanasheria wizara ya NISHATI walikuwa akina nani na walimpa ushauri gani waziri?


  16. Wahusika wa PPRA ambao walikuwa consulted na comments zao

  naona kila kukicha tunajadili maamuzi ya kesi na hao wanao likisha hizi documents mbona hawaleti full mzigo includi hayo majina?

  Unles JF is not as influential as it used to back in the day when people used to trust it with leaked docs...Kulikoni au kitumbua kishaingia mchanga?


  Au kama wanavyosema wanywamwezi kuwa the GAME HAS BEEN RIGGED!!

  Unless kuwepo public inquiry into this fiasco
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  We can't be fooled 4 ever, one day yes!
   
 12. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,473
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  Kwanza kwenye hii kesi tanzania iliwakilishwa na nani? Tumjue ili tujue uelewa wake kwenye masuala ya sheria, na ikiwezekana awajibishwe kwa kukiuka maadili ya kazi kwa kujua au kutojua
   
 13. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hapa kuna problem! sisi tunapata hizi nyeti kila kukicha thanks kwa MM Mwanakijiji and co, lakini sadly mwananchi wa kawaida mwenye shida ya ku access net hajui kinachoendelea, There is a need for JF kuanzisha gazeti au Radio ya kuwaelimisha wadanganyika who needs this urgent outreach help!hawa ni wananchi ambao akili zimegandamana na wanahitaji msaada mkubwa sana wa kuwa empower! remember there is no room kwa udini!. Tunahitaji strategies za ziada kwa kuwaelimisha ndugu zetu wa vijijini.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KWA UTHIBITISHO HUU WA WIZI MGONGONI MWA DOWANS, SERIKALI IJIUZULU MARA MOJA

  Kwa mtaji wa taarifa hii KUTHIBITISHA VIONGOZI WETU SERIKALINI kutulazimisha visivyohalali kulipa Dowans na hatimaye hii siri nzito kutufikia walipakodi masikioni basi kwa pamoja Watanzania hatuna lingine tena

  Kwa pamoja tunasema Kikwete, Rostam Azizi, Nimrod Mkono, Nazir Karamagi, Balozi Maajar, Ngeleja, Chenge, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madalali wenu wengine wengi zaidi, tunasema MJIUZULU MARAMOJA!!!!

  Na nyinyi vyama vya upinzani, asai za kiraia na wanaharakati mbali mbali mkiendelea kunyamazia zaidi HICHI KITHIBITISHO CHA WIZI WA KODI ZETU iliokua iliokua ikilazimishwa na Kikwete na CCM na hatimaye Mungu kutuletea uthibitisho huu, basi watu tutawageukeni na nyinyi na kuonana wabaya hapa!

  Kwa taarifa hii Serikali ya CCM ijiuzulu sasa hivi na wala si kusubiri zaidi. Hii na hatarii!!!
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  you cant be serious
   
 16. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  MM,
  Utaniwia radhi kwa kuuliza tena na labda tena na tena. Nadhani ni jambo la kawaida na linalokubalika kwamba endapo mahakama imetoa uamuzi ambao wewe huridhiki nao, unaweza ku-appeal ili haki itendeke. Sasa nimewasikia Mzee Sitta na Dr. Mwakyembe wakieleza bayana kuwa Richmond na mrithi wake Dowans ni makampuni ya kitapeli. Binafsi siwezi kupuuza kauli za viongozi hao kwa sababu nina hakika wakati ule wa sakata la Richmond walipata fursa ya kujua mengi kuhusu utapeli huo kuliko hata walichokiandika na kusomwa bungeni. In other words, ninamchukulia Dr. Mwakyembe as a reliable source of data kuhusu utapeli wa hayo makampuni.

  Sasa ninachojiuliza, ni je, kama kweli viongozi wetu ni wazalendo, walishindwaje kutumia fursa ya ku-appeal na kupeleka ushahidi mbele ya mahakama unaoonyesha kuwa dowans ni kampuni ya kitapeli tu. Ni kitu gani kimezuia Mwanasheria wetu asichukue hatua hiyo? Je, kipengele ulichogusia kwamba kumbe urithishanaji kati ya Richmond na Dowans ulifanywa kabla hata ya kufikia maridhiano kati ya Tanesco na Richmond, hakiwezi kuwa ni sababu tosha ya kuonesha utapeli wa Dowans? Je, tukiamua kama nchi kutolipa Dowans tutapata madhara gani ambayo wananchi wetu wa kawaida yatawaathiri zaidi ikilinganishwa na madhara watakayopata endapo serikali itajikamua na kulipa mabilioni hayo?
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mi nilikuwa nadhani ni mizaha pale tunaposema kuwa mawaziri wetu huwa wanasaini mikataba bila kuisoma...nimeyaona live sasa...Richmond walifanya kitendo hicho makusudi wakijua hakuna ambae angeshtukia kitendo hicho...and very positively, as expected, wakubwa wetu wa serikali wanaona ukiukaji huo mkubwa siyo ishu, wamekazania DOWANS walipwe haraka sana...wataalamu wa sheria za mikataba mko wapi? Who are these Rex attorneys na wanatumikia sheria za dunia ipi?...tutapata majibu soon.
   
 18. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  tumewahi fikiria haya....?
   
 19. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Thanx MM

  Nachukia ufisadi kwelikweli. Hivi kijana Ngeleja Mganga anafikiri nini kuhusu hili?

  Ana umri mdogo, madhambi haya ni makubwa na yatakaa karne nyingi bila kufutika ataficha wapi uso wake hapo baadaye?

   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  aahgrrrrrrrr!, nadhani mwanasheria mkuu huko aliko akiipata hii tumbo halitakaa sawa. Lakini anywayz ujasiri wa kifisadi huwapofusha kabisa hao watawala wetu.
   
Loading...