Jinsi Richmond/Dowans walivyoizunguka TANESCO na Taifa

Jinsi Richmond/Dowans walivyoizunguka TANESCO na Taifa

Mi nilikuwa nadhani ni mizaha pale tunaposema kuwa mawaziri wetu huwa wanasaini mikataba bila kuisoma...nimeyaona live sasa...Richmond walifanya kitendo hicho makusudi wakijua hakuna ambae angeshtukia kitendo hicho...and very positively, as expected, wakubwa wetu wa serikali wanaona ukiukaji huo mkubwa siyo ishu, wamekazania DOWANS walipwe haraka sana...wataalamu wa sheria za mikataba mko wapi? Who are these Rex attorneys na wanatumikia sheria za dunia ipi?...tutapata majibu soon.

Sio hivyo bali ni ubinafsi na tamaa na ile ya kupewa 10%...hakuna wazalendo sasa hivi
 
KWA UTHIBITISHO HUU WA WIZI MGONGONI MWA DOWANS, SERIKALI IJIUZULU MARA MOJA

Kwa mtaji wa taarifa hii KUTHIBITISHA VIONGOZI WETU SERIKALINI kutulazimisha visivyohalali kulipa Dowans na hatimaye hii siri nzito kutufikia walipakodi masikioni basi kwa pamoja Watanzania hatuna lingine tena

Kwa pamoja tunasema Kikwete, Rostam Azizi, Nimrod Mkono, Nazir Karamagi, Balozi Maajar, Ngeleja, Chenge, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madalali wenu wengine wengi zaidi, tunasema MJIUZULU MARAMOJA!!!!

Na nyinyi vyama vya upinzani, asai za kiraia na wanaharakati mbali mbali mkiendelea kunyamazia zaidi HICHI KITHIBITISHO CHA WIZI WA KODI ZETU iliokua iliokua ikilazimishwa na Kikwete na CCM na hatimaye Mungu kutuletea uthibitisho huu, basi watu tutawageukeni na nyinyi na kuonana wabaya hapa!

Kwa taarifa hii Serikali ya CCM ijiuzulu sasa hivi na wala si kusubiri zaidi. Hii na hatarii!!!

Hawawezi kujiuzulu hawa mkuu inabidi tuwatoe tu kwa nguvu ya umma!!
 
big news. wazee wa bagamoyo na sumbawanga si wawachukue misukuke hawa jamaa wa dowans na kuwafanyisha kazi kila siku.......inauma sana.hope tundu lisu atailipua bingeni na kafulila pia,sita nae sijui
 
aaah sasa legality ya hiyo hukumu inatoka wapi? Hv jaman tanesco wana lawyers kweli au wakat wa kutoa utetezi wao walioverluku hvo vifungu yan day afta day nackia mambo mapya kuhsu hyo issue. Nategemea kusikia hata hiyo kesi haikuamuliwa huko icc hilo pia possible

Lawyers wanao ila sema either wameshirikishwa kwenye hilo deal au wameogopa kwa vile ufisadi huu unamhusu JK na swahiba zake! Lakini pia inawezekana hakuna kesi iliyofanyika zaidi ya kucheza na paper work tu. Kama sivyo, kwanini Dowans hawajapeleka hiyo hukumu mahakama kuu na badala yake wanapeleka viambatanisho tu huku wakihaha walipwe haraka haraka?
 
tumewahi fikiria haya....?

yameshafikiriwa na kufafanuliwa kwenye ripoti ya Mwakyembe. Jamani.. labda mrudi nyuma kusoma Ripoti ya Mwakyembe tena kupaa majibu ya masuali yote ya tenda yalivyokuwa na jinsi gani Richmond walipewa Tenda in the first place. Tumeandika hiyo tukiwa tuna presume kuwa watu wanakumbuka na wana access ya ripoti ya Kamati Teule.
 
Mi nilikuwa nadhani ni mizaha pale tunaposema kuwa mawaziri wetu huwa wanasaini mikataba bila kuisoma...nimeyaona live sasa...Richmond walifanya kitendo hicho makusudi wakijua hakuna ambae angeshtukia kitendo hicho...and very positively, as expected, wakubwa wetu wa serikali wanaona ukiukaji huo mkubwa siyo ishu, wamekazania DOWANS walipwe haraka sana...wataalamu wa sheria za mikataba mko wapi? Who are these Rex attorneys na wanatumikia sheria za dunia ipi?...tutapata majibu soon.

Mkuu huwa wanajua hiyo mikataba na implications zake ila sema tu hawajali kwasababu wao wanakuwa wameshachukua chao mapema (CCM). In short, hawana uchungu ni nchi hii kwasababu mwisho wa siku anaye umia ni mwananchi wa kawaida siyo wao (mafisadi).
 
Mzee mwenzangu MM,

Maneno hayo hapo chini ni maneno ya kizalendo yenye fukuto kuu la kuipenda nchi kama uhai wako mwenyewe. Binafsi nashukuru sana kwa uchambuzi wako yakinifu.

Naamini kwa dhati kabisa CCM na vibaraka wake watafagiliwa na mahali pao kutoweka katika ufinyu katika muda mchache ujaokizazi chetu kikiwa na nguvu na ari ya kujenga nchi.


"Kutokana na uzito wa ushahidi ambao tumeupendekeza mbele ya wasomaji na Watanzania wenzetu tunajikuta tunabakia na mapendekezo yafuatayo tu:

  1. Serikali isilipe hata senti moja na iamue kujitoa kwenye Mahakama ya Usuluhishi na badala yake Bunge letu liimarishe sheria zetu za usuluhishi wa kibiashara ili mikataba yote inayohusiana na umma inapotokea matatizo iamuliwe kwa sheria zetu wenyewe.
  2. Mitambo ya Dowans ambayo tayari tumeshalipia zaidi ya gharama yake kuiingiza nchini ikamatwe na kutaifishwa kwa kutumia madaraka ya Rais (Executive Order) au kwa sheria nyingine yoyote ile.
  3. Watendaji wote wa Dowans S.A na Dowans Tanzania Limited ambao walikuwepo wakati Dowans S.A inarithi mkataba wa TANESCO kutoka Richmond kwenye makubaliano ya Disemba 23, 2006 watimuliwe nchini, watangazwe kuwa ni "watu wasiotakiwa" personae non grata. Wapewe si zaidi ya masaa 24.
  4. Rostam Aziz ambaye ndiye amekuwa kinara wa kuitetea Dowans na ambaye mapema mwaka huu (Januari 5, 2011) alikiri kuwa yeye ndiye aliyewashawishi Dowans kuja nchini na ambaye ndiye aliyepewa nguvu ya kisheria (Power of Attorney) kutumika kwa niaba ya Dowans Holdings S.A alikuwa anajua na alipaswa kuwa anajua kuwa Dowans S.A walikuwa tayari wamechukua mkataba wa Richmond na TANESCO. Akiwa ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye aliapa kulinda na kutetea sheria na Katiba ya nchi yetu alipaswa kuonesha uzalendo kwa kuitaarifu TANESCO (shirika la umma) juu ya jambo hilo. Akiwa ni mtu ambaye angenufaika kwa namna moja au nyingine na uwepo wa Dowans nchini (akiwa ni mshirika na rafiki wa mmoja ya wamilikiwa wa Dowans S.A) Rostam hakuliweka na hadi hivi sasa hajaweka Tanzania mbele katika suala hili. CCM inatakiwa imvue uanachama na serikali imshtaki kwa makosa mengi ambayo tungeweza kuyafafanua kutokana na kushiriki kwake.
  5. Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Nazir Karamagi naye ahojiwe na ikibidi ashtakiwe kwa kushiriki kwake kuificha TANESCO ukweli kuwa mkataba wa TANESCO kuhamishiwa kwa Dowans S.A na Richmond. Bw. Karamagi alijua alipaswa kujua kuwa mkataba ulikuwa umekwishahamishiwa kwenda Dowans kutokana makubaliano ya Oktoba 14, 2006. Kwani, ni yeye aliyetoa taarifa kwa TANESCO juu ya nia ya Richmond kuhaulisha mkataba wake kwenda Dowans S.A na alisisitiza kuwa iwe hivyo licha ya mapingamizi ya Shirika hilo la Ugavi.
  6. Mwanasheria Mkuu wa Tanzania awajibishwe kwa kutetea malipo haya ambayo ni wazi ni kinyume cha sheria.
  7. Huduma yote iliyotolewa na majenereta ya Dowans S.A ichukuliwe kuwa ni huduma ya bure kwani Mkataba uliosainiwa Disemba 23, 2006 haukuwa na maana yoyote kisheria kwani Dowans S.A ilikuwa imekwishajifunga kinyume na kifungu cha 15.12 na Mkataba wake na Richmond wa Oktoba 14, 2006. Ukweli huu uko wazi kwani katika kesi yake dhidi ya Richmond huko Houstona Marekani, Kampuni ya Dowans haitaji kabisa mkataba wa Disemba 23, 2006 bali inatambua kuwa iliingia makubaliano na Richmond ya kuchukua mkataba wa TANESCO tarehe 14, Oktoba 2006.
  8. Watanzania wote wenye dhamiri njema wapinge kwa nguvu na namna zote malipo haya ya kidhalimu na kutaka wale wote waliojitokeza kuyatetea wawajibike wao wenyewe au wawajibishwe na vyombo halali. Malipo haya ni kinyume na maadili, ni ya kimabavu na yanadhalilisha utu wa Mtanzania.


Kutoka kwenye
FIKRA PEVU"
 
yameshafikiriwa na kufafanuliwa kwenye ripoti ya Mwakyembe. Jamani.. labda mrudi nyuma kusoma Ripoti ya Mwakyembe tena kupaa majibu ya masuali yote ya tenda yalivyokuwa na jinsi gani Richmond walipewa Tenda in the first place. Tumeandika hiyo tukiwa tuna presume kuwa watu wanakumbuka na wana access ya ripoti ya Kamati Teule.
Sisi watanzania ni wasahaulifu kweli kweli

Watu tunasahau kwamba tuliishangilia CCM na kuipa kura November 2010 kwa ujira wa Khanga,kofia,shati na Tshirt? Tutakumbuka kweli mambo mazito ya Kikatiba na kisheria ya Ripoti ya Dr MWakyembe??
Tumeshau kwamba Dr Slaa aliahidi kuondoa kodi ya Cemenet na Bati ili hata mwenye MShahara wa 150,000 aote kujenga nyumba?
Watanzania tu wasahaulifu kwelikweli.
Mtanzania Average hana muda wa kupoteza kujua Hali yake Duni inatokana na nini na nini afanye kuanzisha vita ya kweli ya kupinga uhuni wa serikali ya CCM. Mtanzania average anajiuliza" Hivi Richmond wasingepewa Tenda hiyo tenda ningepewa mimi?? Au hizo pesa za kuwalipa ningepata shilingi ngapi?

Nye!
 
yameshafikiriwa na kufafanuliwa kwenye ripoti ya Mwakyembe. Jamani.. labda mrudi nyuma kusoma Ripoti ya Mwakyembe tena kupaa majibu ya masuali yote ya tenda yalivyokuwa na jinsi gani Richmond walipewa Tenda in the first place. Tumeandika hiyo tukiwa tuna presume kuwa watu wanakumbuka na wana access ya ripoti ya Kamati Teule.

Hii ni indication kwamba JF ya sasa si ile ya wakati ule and the new guys are not doing their homework!!!!!!! Sasa unakuta ushabiki ndiyo unatumika kuendesha mjadala na bado kuna members ni wabishi hata kwa yale yaliyokwishasemwa au kuandikwa baada ya kuwa proven.

Mtu anauliza Mwakyembe alikuwa wapi siku zote? Au ooh hawa akina Sitta ni kusema sema tu as if wao ni TAKUKURU, DPP na mahakama. Where is UWT?
 
Mahakama ya Kimataifa inajua yale tu ambayo yanaletwa mbele yake; yaani ushahidi unaoletwa mbele yake. Mahakama haifanyi uchunguzi nje ya ushahidi ulipo pale. Ni jukumu la pande zinazoshtakiana kudisclose information yoyote ambayo ni relevant kwa kesi. Tanesco hawakujua kuwa wakati DG anasaini anaandika barua kuwa Dowans irithishwe mkataba wa Richmond Disemba 21, 2006 wao Dowans na Richmond walikuwa wamekwisharithishana mkataba oktoba 14 na Dowans wameshaanza kutekeleza kwa kulipia mitambo ya Vulcan iliyoingizwa nchini Oktoba mwishoni 2006.

Dowans walitakiwa kuwaambia ICC kuwa mkataba wake na Tanesco ulirithiwa Oktoba 14. Bahati isingeweza kufanya hivyo kwa sababu ingefichua kuwa ilirithi mkataba bila idhini ya Tanesco.

Wow! I hope any good lawyer would do so! you are Journalist by professional, unalisema jambo la kisheria kama mwanasheria!! just common sense! hawakuliona hawa watetezi au hawakulijua, just imagine; unawaza, kuishi, kuota na kusema kuhusu kazi yako...uanasheria kweli uchunguzi na technik ndogo hii hawakuiona??? no something is wrong with our system!
 
Mtu huitaji kuwa lawyer kuona kwamba huu mkataba ni batili in so many angles, kwa kuangalia haraka haraka naona grounds mbili, Kwanza kuna grounds za Fraud, pili kutokana na shinikizo la wizara hii inamaanisha Tanesco on their part walisign mkataba without free Consent..., Hii issue naona sasa sio ya kukataa kulipa tu bali ontop ya kutokulipa inabidi watu wawajibike....., Huu ni wizi wa bila huruma, and this is what we know sijui ni mangapi huwa yanapita bila sisi kujua...
 
Mwanakijiji hivi "watu wa siri kali" au serikali ya JK mwenyewe hawakutafuti kweli. siamini vichwa vyote vilivyondani ya serikaliya JK hakuna ambaye hajawi kuyaona haya au kumshtua mkuu.

The good thing is JK is killing CCM silently. Thanks to Dowans.
 
aaah sasa legality ya hiyo hukumu inatoka wapi? Hv jaman tanesco wana lawyers kweli au wakat wa kutoa utetezi wao walioverluku hvo vifungu yan day afta day nackia mambo mapya kuhsu hyo issue. Nategemea kusikia hata hiyo kesi haikuamuliwa huko icc hilo pia possible
Walishaahidiwa mshiko wa nguvu sana na lawyer mwenzao ambaye billionaire sana.
 
Mwanakijiji hivi "watu wa siri kali" au serikali ya JK mwenyewe hawakutafuti kweli. siamini vichwa vyote vilivyondani ya serikaliya JK hakuna ambaye hajawi kuyaona haya au kumshtua mkuu.

The good thing is JK is killing CCM silently. Thanks to Dowans.

hahaha sidhani kama wakinitafuta na kunipata pingu zitatosha... Kazi watakuwa nayo wale tutakaowaachia haya kama watagwaya na kutetemeka mbele zao au nao watashika mwenge umulikao wa fikra pevu za mabadiliko mikononi mwao!
 
Hawa jamaa (CCM) wanajua kila kitu katika hiii saga......hata wao hawajui wanataka nini??? wana tamaa ya hiyo pesa na hapohapo wanaogopa wananchi.....wanapima jinsi walivyopiga pesa ya EPA kiulaini na sasa wanashangaa ngoma imekua ngumu kupiga hii ya Dowans...

Haingii akilini UVCCM wanapinga malipo hayo then wankuja CC (Ambao ndiyo walafi koz most of them ndo walipiga EPA) wanabariki malipo hayo ambayo Werema alisema hayaepukiki. Then wanakaa wabunge wote wa CCM wakiwemo wale wa CC waliobariki wanakuja na story ingine kuwa YAWEZEKANA TUSILIPE au watatusaidia tulipe KIDOGO (MKONO ndo alisema haya)

So ukiangalia kwa undani huwezi jua wao wenyewe wanataka nini.....WANAUJUA ukweli na wanamjua mwenye MALI anaetakiwa kulipwa ni nani....thus why kuna beneficiaries waanaosupport haya Malipo Hasa Waziri husika....BOss wao analijua hili (RAIS) waziri mkuu analijua hili ila cha kushangaza hawalitolei TAMKO kwa kivuli cha kufuata sheria SWALI: SHERIA IPO KTK DOWANS TU?????

They have to know sisi wananchi tumechoka na wizi wao so they have to act smart on this SAGA kuepusha nchi isiingie kwenye machafuko....Janja yao ya kusema TZ kuna udini ili tusijadili mambo ya msingi IMEGONGA mwamba
 
hahaha sidhani kama wakinitafuta na kunipata pingu zitatosha... Kazi watakuwa nayo wale tutakaowaachia haya kama watagwaya na kutetemeka mbele zao au nao watashika mwenge umulikao wa fikra pevu za mabadiliko mikononi mwao!

SURE...U r RIGHT.....In fact Nimeipenda signature Yako...Am 100% behind it....
 
mzee mwanakijiji your the greatest thinker, thanks. kwa kweli imefika wakati sasa wananchi tuamke
tudai haki zetu wanyonge
 
Hapo ndipo ninapojiuliza kazi ya usalama wa Taifa nini? Haiingii akilini UWT ambao tunajua wapo wengi, wapo kila idara, hata kwenye Taasis binafsi walikuwa hawajui hili. Taasis hii ambayo inasemekana bajeti yake ni kubwa kama wizara fulani:


  • inafanyaje kazi zake? Iweje kamati Teule ya Bunge ioneshe ufanisi mkubwa kwa muda mfupi huku wao wapo fulltime.
  • Ufanisi wake unapimwaje? au kazi yao ni kutoa taarifa zinazohusu maandamano tu?
  • Au hawana ujuzi na ubunifu wa kutosha kuweza kugundua mambo ambayo hayana maslahi kwa Taifa?
  • Kwa nini isivunjwe na kutafuta utaratibu mwingine?
  • Au kama taarifa wanatoa, lakini hazifanyiwi kazi kwa nini wasijiuzuru badala ya kuwa wanafiki?
 
Back
Top Bottom