Jinsi nilivyotongoza jini bila kujua

Jinsi nilivyotongoza jini bila kujua

Leo saa 3 usiku natuma muendelezo wadau nipo job now na simu inasumbua chaji nataka niiweke chaji mda huu
 
INAENDELEA
********************************************
Basi swali langu la mimi kumuuliza Asha kuhusu kumjua mariam lilimshtua sana unajua kwanini mtaani kwangu nilikuwa nasifika kama kijana mpole na wengi walikuwa hawajawahi kuniona na demu hata asha ni mwanamke flani alietokeaga kunionyesha dalili za kunipenda sema nikawa kama najifanya simuelewi,

Asha akacheka na wewe ushaanza mambo hayo inaonekana huyo mariamu kakukamata eeeh?

Then akaniambia mimi nawahi nyumbani si unajua bibi angu uwa anapenda wajukuu zake tuwe mda wote nyumbani akanipiga begani na mkono wake huku akicheka na kuondoka kwa mwendo wa madaha mtoto ana figa kweli ila mapepe[emoji1] nilijisemea moyoni na kuanza safari ya kurudi kwangu

********************************************
Siku hiyo ikawa imepita kimya kikitawala kati yangu na mpenzi wangu mariamu tulikuwa ni lazima haipiti siku bila kutumiana sms wala kupigiana simu nilishangaa ukimya wake lakini sikujali chochote basi asubuhi nimeamka saa moja nataka niende kutafuta kazi kuna kazi jamaa angu side aliniambia ya kuuza chipsi ni mda mrfu aliniambia bosi wake anatafuta mfanyakazi mwingine hivyo akaona kutokana na uaminifu wangu bora anipe ilo dili japo nilililitupaga kapuni ila unajua mda mwingine ukiwa hauna kazi unakumbuka kazi za nyuma ulizowahi kupewa[emoji1][emoji1]

Sasa nikachukua simu yangu ili niangalie kama mpenzi wangu mariamu amenitumia hata sms yoyote, sikuamini nilipokutana amenitumia sms zaidi yakumi za kulalamika juu yangu sms zake alikuwa akilalamika kitu kilichonishangaza ni kuwa anadai eti namchunguza sana na simuamini kwanini simuamini ingawa yeye ananipenda hapendi kuona namchunguza sms ya mwisho alisema kuwa leo nakuja jioni naomba uwepo",

Sms zake zilinishangaza amejuaje kama namchunguza nikawaza hau asha kamwambia nini lakini asha si alisema hamjui mariamu sasa huyu demu kajuaje? Nilipigwa na butwaa japo nikaona labda ni mambo ya kawaida basi nikamcheki side na kumtaarifu kuwa nakuja ofisini kwake nimekubali kufanya kazi basi baada ya dk 30 nikawa nimefika kwa side nikamkuta anamenya viazi basi akanipa tano na stori za hapa na pale zikawa zinaendelea mimi na side ni washkaji sana tunaopendana sana na unajua hakuna kitu kizuri kama kufanya kazi na mtu unaeendana nae basi rasmi nikawa nimeanza kazi ya kuuza chipsi na side basi nilipiga kazi hadi majira ya saa tisa na nusu nikamwambia side oyaah kama nataka niende ghetto mara moja kuna mgeni aliniambia saa kumi anakuja side akacheka sana akaniuliza shemeji nini nikamjibu ndio akasema poa nenda ila fanya mpango kesho uwahi mapema mimi nitapiga kazi leo hadi saa4 ntafunga,

Basi nikaanza kuondoka kwenda gheto kwangu ile nakaribia ghetto mariamu akanitumia sms beiib mimi ndio nipo uwanjani pale nimekaribia kwako nikasema looh ikanibidi niongeze mwendo niwahi ghetto chafu maana nilikuwa nimepaacha vibaya mashuka sijatandika na ukiangalia mtoto ndio amekaribia[emoji1]

Basi nilipoingia tu ghetto sijakaa kama dk 2 nikaanza kusikia marashi makali harufu nzuri nikasema kimoyoni looh mtoto ameshafika huyo ile sijakaa sawa mtoto akagonga mlango hodi x3

Ikabidi nimfungulie sikuamini mtoto siku hiyo alikuwa amependeza sana sana alikuwa ananukia vizuri mnoo unajua sometime unaweza ukawa na demu mkal hadi ukawa unajiuliza ulimpataje pataje[emoji1]

Basi nikamshika kiuno mtoto akaingia ndani ila neno lake la kwanza mmmh beiib mbona gheto pachafu mimi sipendagi kupakuta hivi leo nataka nikufanyie usafi pakae sawa basi mtoto akaanza kufanya usafi pale ghetoni mimi nilikuwa tu nimetulia kitandani kiukweli nilikuwa nawaza vitu vingi kitu kilichokuwa kinanipa mashaka ni kwann mariamu aliniambia kuwa namchunguza simuamini amejuaje?
Itandelea wakuu hii ni simulizi ya kweli juu ya maisha yangu niliyowahi kuyapitia mwaka miaka mitano iliyopita kwa kuanza mahusiano na jini bila kujua atimae nikapata madhara makubwa ikiwemo upungufu wa nguvu za kiume pamoja na kufukuzwa kazini kisa tu ugomvi wangu ambao ulizuka mimi na mariamu sehemu ya tatu inayokuja yapo mengi katika simulizi hii nawaombeni mzidi kuifuatilia kwani mtajifunza mambo mengi nitaendeleea baadae saa tano wakuu mniwie radhi[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]


MUENDELEZO BOFYA HAPA
 
Huyu mariamu jini bila shaka anasoma uzi huu kazi unayo mbona
Nilishaachanaga nae alisharudigi ujinini mkuu ni mambo mengi nilipitia ili niachane nae nilizunguka kwa waganga wa kila aina na makanisani maana aliniapaga hawezi ondoka kwangu any way nisimalize utamu wa hii simulizi
 
Story za itaendelea haijawahi kuwa na mwisho

Ukifika mwisho unitag mkuu coz nipo ktk experience ya kutafuta jini wa kudate nae coz hawa wanawake wa kawaida tunaelekea kushindwana

Nataka nipate changamoto mpya
 
woyiii

alikaa kimya dakika tatu ndio akakupa namba, bila shaka ni sekunde 180 mmepigwa bumbu wazi😂
 
Back
Top Bottom