Jiko la gesi kuwaka moto

Jiko la gesi kuwaka moto

Hizo njiti hapo ulikuwa unawashia au..manake hayo majiko no automatic ignition hayahitaji kuwashwa kwa njiti.
Hili jiko ni automatic kuna muda huwa linasumbua kuwaka hivyo natumia kiberiti.
 
Mlaji unapaswa kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika ikiwemo TBS , na kiuhalisia unapaswa upewe fidia hii ni kutokana na kumlimda mlaji.

Nenda peleka ushahidi wako TBS watakupatia utaratibu
Nani atanipatia fidia ni muuzaji au TBS?
 
Wadau kama brand hii hapo chini vipi, haizingui?
Na kuhusu service linafanyiwaje?
 

Attachments

  • IMG_20180122_220143.jpg
    IMG_20180122_220143.jpg
    125 KB · Views: 118
Najiuliza hicho kioo cha nini? Kinaongeza nini kwenye ufanisi wa jiko? Kingekuwa kioo cha maana hilo jiko lisingeuzwa 80,000!
Kioo kinarahisisha kusafisha. Unaweza tumia ile dawa ya kufutia vioo kuondoa mafuta na mabaki ya chakula kwa urahisi. Lakini pia ni kwaajiri ya kupunguza risk ya kutu maana jiko likiwa linalowa muda wote linakuwa lina weka unyevunyevu na kutengeneza kutu.
 
Heri yako wewe limeka 2 months,kuna jirani yangu kalishusha tu kweny bajaji.Kafunga mtambo,kuwasha akaweka sufuria la maji kuzindua jiko.Kilichofuatia ni vioo kuruka ruka juu na jiko likiishia hapo.Bila ajizi akalipakia na kurudi dukani,nachokumbuka mwenye duka alielewa kwa haraka sana.
Na tahadhali pia kwa wale tunaopenda kuamini sana hay auto hakikisha unazima huku kwenye mtungi na si kufunga jiko peke yake.Kuna baadhi utahishi umelifunga na bado linatoa gesi hasa yakiwa yamekaa muda kidogo.Tuelekeze hata watu wetu katika kuzima hayo majiko.Pole ndugu kwa hasara hiyo.
But uzuri wa gesi ikiwa inavuja utasikia harufu yake katika chumba cha jiko imetapakaa. Ni ngumu gesi kuwa inavuja halafu usijue
 
Kioo kinarahisisha kusafisha. Unaweza tumia ile dawa ya kufutia vioo kuondoa mafuta na mabaki ya chakula kwa urahisi. Lakini pia ni kwaajiri ya kupunguza risk ya kutu maana jiko likiwa linalowa muda wote linakuwa lina weka unyevunyevu na kutengeneza kutu.
Quality aluminium au stainless steel inasafishika kirahisi tu. Sijaona shida yoyote kusafisha jiko la bati tena jeupe.
Wangeweka quality glass inayovumilia joto la jiko, ng'ombe hawezi kuelemewa na nundu yake.
 
But uzuri wa gesi ikiwa inavuja utasikia harufu yake katika chumba cha jiko imetapakaa. Ni ngumu gesi kuwa inavuja halafu usijue
Ni kweli, tuna kaa na watu tofauti hapa duniani.Ni vyema kuelemisha watu,wewe umejua wengine hawajui amini katika hivyo.Kuna watu hawawezi tofautisha harufu na pia harufu mpaka mtu aihisi inategemea na utashi wake kwa huo muda.
Kuna mtu aliwaha acha jiko wazi na harufu kama unavyosema ikatapakaa.Aliyekuja kushtuka ni mtu mweninge tena alikimbilia jikoni baada ya kuhisi kuna mtu anataka kuwasha jiko.Alipoulizwa akasema"Mimi nilijua sijui harufu ya nini huko kumbe gas"
 
Pole sana, unaweza unguliwa na nyumba bila kujua
 
Ni haya majiko mapya yaliyotoka hivi karibuni mkuu.
Majiko ya gesi yaliyokuja vizuri ni zile Nikai za mwanzo za Japan

Nitanunuaje jiko la gesi eti lina kioo chembamba kabisa juu...wakati mara nyingine unaweka sufuria nzito na kubwa.

Hii michina feki itamaliza watu.

 
Kuna kitu kama mafuta yalikuwepo juu ya hicho kioo ndiyo ambayo nayo yaliwaka Au ulifanya Usafi na kitu ambacho kiliharibu uimara wa Kioo.............!!!
 
Hicho kioo kinakaa wapi na kazi yake nini?
Kile kioo kiko pale juu karibu na plates ila imecover sehemu kubwa, na ni urembo tu hakina kazi nyingine.

Sasahivi wachina wameleta hayo majiko ni mengi kweli na kuna namna ya kuadjust aina ya moto unaoutaka kwa chini kabisa...low, high, green au yellow colour.

Imagine jiko la plate 2 pamoja na mtungi wa gesi ule mkubwa vyote vinauzwa laki na 70 tu.
 
Majiko ya gesi yaliyokuja vizuri ni zile Nikai za mwanzo za Japan

Nitanunuaje jiko la gesi eti lina kioo chembamba kabisa juu...wakati mara nyingine unaweka sufuria nzito na kubwa.

Hii michina feki itamaliza watu.


Ninalo la Nikai aiseee ni mashineee
Haya majiko yenye majinaa yasioeleweka mengi mabovu
 
Back
Top Bottom