Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,183
- 1,502
Maria Sarungi, Mwanaharakati na Mwanachama hai wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekuwa akiendesha kampeni za kutukana na kudhalilisha Viongozi/Mamlaka halali kwenye mitandao ya kijamii kwa mgongo wa kudai katiba mpya.
Sio tatizo kudai anachokiamini, tatizo ni namna anavyoendesha hizo harakati zake, zimekuwa ni harakati za kutukana watu, kudhalilisha mamlaka halali na muda mwingine kubeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hakuna ubishi kuwa Mheshimiwa Freeman Aikeli Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema ni Mmoja wa Wanasiasa wa upinzani wenye mafanikio makubwa na historia itamuandika kwa wino wa dhahabu. Mbowe amekuwa wakati wote akikosoa, kushauri au kufanya harakati bila kudhalilisha au kutweza utu na heshima za watu wengine. Hawa wanaojiita wanaharakati wa mitandaoni ni bora wakajifunza na kuiga heshima na hekima ya Mwenyekiti wao.
Tunaweza kutoa dukuduku zetu bila kutukana, kukebehi au kudharau watu wengine na Serikali yetu ikasikiliza na kufanyiia kazi. Maria Sarungi, mamlaka unayoidhalilisha imewekwa na Wananchi. Serikali inafanya mambo mengi ya maendeleo haiwezekani kila siku wewe ni kukosoa tu as if hakuna Shule mpya zinazojengwa, barabara, miradi ya maji, hospital, vituo vya afya, miradi ya Umme, SGR, NHPJ, Elimu bure etc.
Tanzania ni nchi yetu, itajengwa na Watanzania.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan