Jifunzeni Siasa za Freeman Mbowe; Anachofanya Maria Sarungi ni ukosefu wa heshima kwa Mamlaka halali

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Maria Sarungi, Mwanaharakati na Mwanachama hai wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekuwa akiendesha kampeni za kutukana na kudhalilisha Viongozi/Mamlaka halali kwenye mitandao ya kijamii kwa mgongo wa kudai katiba mpya.

Sio tatizo kudai anachokiamini, tatizo ni namna anavyoendesha hizo harakati zake, zimekuwa ni harakati za kutukana watu, kudhalilisha mamlaka halali na muda mwingine kubeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hakuna ubishi kuwa Mheshimiwa Freeman Aikeli Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema ni Mmoja wa Wanasiasa wa upinzani wenye mafanikio makubwa na historia itamuandika kwa wino wa dhahabu. Mbowe amekuwa wakati wote akikosoa, kushauri au kufanya harakati bila kudhalilisha au kutweza utu na heshima za watu wengine. Hawa wanaojiita wanaharakati wa mitandaoni ni bora wakajifunza na kuiga heshima na hekima ya Mwenyekiti wao.

Tunaweza kutoa dukuduku zetu bila kutukana, kukebehi au kudharau watu wengine na Serikali yetu ikasikiliza na kufanyiia kazi. Maria Sarungi, mamlaka unayoidhalilisha imewekwa na Wananchi. Serikali inafanya mambo mengi ya maendeleo haiwezekani kila siku wewe ni kukosoa tu as if hakuna Shule mpya zinazojengwa, barabara, miradi ya maji, hospital, vituo vya afya, miradi ya Umme, SGR, NHPJ, Elimu bure etc.

Tanzania ni nchi yetu, itajengwa na Watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
 
images (5).jpeg

Kazi nzuri inayofanywa na Maria Sarungi iendelee.
 
Maria Sarungi Tsehai amekuwa na msimamo thabiti wa kusimama upande ambao yeye anaona ni wa haki. Hasiti kuwatetea wale ambao anaona hawatendewi haki.

Hasiti kupingana na mamlaka pale anapoona inakosea. Anatoa uwanja kwa watu wote (bila kujali chama chao) kutoa mawazo yao kwa wazi kuhusu muelekeo wa nchi yao. Huko kwenye kutoa pongezi wako wengi, wala hahitajiki.

Ninachoshangaa ni huku kumpigia debe na kumgeuza statesman mtu ambae ni hivi karibuni tu tuliambiwa kuwa alikuwa gaidi. Au ndio mambo ya divide and rule?

Amandla...
 
Maria Sarungi Tsehai amekuwa na msimamo thabiti wa kusimama upande ambao yeye anaona ni wa haki. Hasiti kuwatetea wale ambao anaona hawatendewi haki. Hasiti kupingana na mamlaka pale anapoona inakosea. Anatoa uwanja wa watu wote (bila kujali chama chao) kutoa mawazo yao kwa wazi kuhusu muelekeo wa nchi yao. Huko kwenye kutoa pongezi wako wengi, wala hahitajiki. Ninachoshangaa ni huku kumpigia debe na kumgeuza statesman mtu ambae ni hivi karibuni tu tuliambiwa kuwa alikuwa gaidi. Au ndio mambo ya divide and rule?

Amandla...
Hakuna shida na msimamo wake au namna anavyotetea hayo anayoa amini, Tanzania ni Nchi huru yenye, inayofuata utawala wa Sheria. Tatizo ni namna anavyo adress hayo mawazo yake, sio lazima utweze mamlaka au udhalilishe watu wengine kutetea kile unachokiaminiu.
 
Hakuna shida na msimamo wake au namna anavyotetea hayo anayoa amini, Tanzania ni Nchi huru yenye, inayofuata utawala wa Sheria. Tatizo ni namna anavyo adress hayo mawazo yake, sio lazima utweze mamlaka au udhalilishe watu wengine kutetea kile unachokiaminiu
Sasa ukianza kumtaka akukosoe kwa namna unayotaka wewe si ndio mwanzo wa kumfunga mdomo? Kuna tatizo gani mtu kuwa passionate kwenye kile anachoamini?

Amandla...
 
Maria Sarungi, Mwanaharakati na Mwanachama hai wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekuwa akiendesha kampeni za kutukana na kudhalilisha Viongozi/Mamlaka halali kwenye mitandao ya kijamii kwa mgongo wa kudai katiba mpya.

Sio tatizo kudai anachokiamini, tatizo ni namna anavyoendesha hizo harakati zake, zimekuwa ni harakati za kutukana watu, kudhalilisha mamlaka halali na muda mwingine kubeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hakuna ubishi kuwa Mheshimiwa Freeman Aikeli Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema ni Mmoja wa Wanasiasa wa upinzani wenye mafanikio makubwa na historia itamuandika kwa wino wa dhahabu. Mbowe amekuwa wakati wote akikosoa, kushauri au kufanya harakati bila kudhalilisha au kutweza utu na heshima za watu wengine. Hawa wanaojiita wanaharakati wa mitandaoni ni bora wakajifunza na kuiga heshima na hekima ya Mwenyekiti wao.

Tunaweza kutoa dukuduku zetu bila kutukana, kukebehi au kudharau watu wengine na Serikali yetu ikasikiliza na kufanyiia kazi. Maria Sarungi, mamlaka unayoidhalilisha imewekwa na Wananchi. Serikali inafanya mambo mengi ya maendeleo haiwezekani kila siku wewe ni kukosoa tu as if hakuna Shule mpya zinazojengwa, barabara, miradi ya maji, hospital, vituo vya afya, miradi ya Umme, SGR, NHPJ, Elimu bure etc...

Tanzania ni nchi yetu, itajengwa na Watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Haieleweki kama unampongeza Mbowe au unamlaumu Maria , haijulikani pia kama unalia au unalalamika .

Bali tukuambie hivi , Chadema ni kama kikosi kabambe cha soka , kuna viungo wakabaji , kuna washambuliaji na kuna wengine wagawa pasi , ukiona Maria anatukana nenda Mahakamani
 
Sijawai kumuamini huyo Maria na mwenzake Fatuma, hawa wamekulia kwenye malezi ya faida za wazazi wao kuwa viongozi nchi hii sidhani kama huwa wapo serious saana na hizo harakati zao zaidi ya kuweka kiini macho tuu kwa walala hoi.
 
Haieleweki kama unampongeza Mbowe au unamlaumu Maria , haijulikani pia kama unalia au unalalamika .

Bali tukuambie hivi , Chadema ni kama kikosi kabambe cha soka , kuna viungo wakabaji , kuna washambuliaji na kuna wengine wagawa pasi , ukiona Maria anatukana nenda Mahakamani
We endelea kukunja ngumi huwezi elewa chochote, Chadema ilishafutika kwenye ramani Erythrocyte
 
Back
Top Bottom