Malipo ya kodi TRA huwa yanakuwaje? Nataka kuagiza mzigo, shida sijui hapa Tz nitaulipia shilingi ngapi!
Si mizigo yote inalipiwa kodi. Kama ukitumia njia ya "Registered Air Mail" mara myingi haulipi kodi kwa items nyingi.
 
Mimi process zote nimezielewa mpaka kufikisha mzogo Tz, shida yangu ni hizo kodi za Tanzania, nimeenda kwenye mtandao wa TRA hawana guidance inayoeleweka kuhusu Mizigo inayotoka nje, ukizingatia Tanzania tuna sifa moja ya "poor customer care", hapa napo pana fursa nzuri. Hii kutumia kwa njia ya posta nayo inaonesha forwarding companies nyingi kama myus hawatumii courier hii kusafirisha mizigo.
 


Safi sana
 
Nahotaji kuagiza JBL FLIP 4 speaker, naombeni muongozo mtandao gani mzuri wa kuagizia
 
Je package yote ina uzito wa KG ngapi??

Kumbuka uzito wa bidhaa ndio hutupatia shipping cost.
Waweza pitia hapa: www.bit.ly/101buy4me kwenye bandiko namba 1 na #2.

Ni vyema kuagiza toka china sababu ya kuwa na option nyingi za kusafirishia.

Karibu
Mzigo unalipiwa kutokana na uzito au pia inazingatiwa na aina ya mzigo unaoimport?
 
Nilijaribu kununu bidhaa nikapewa na track number lkn kuitrack ilikua mtihani,pia nilisahau katika kufatilia mzigo nikajikuta nimekubali kua umefika tayari,bado sijakata tamaa nataka kuagiza kitu kingine cha bei kidogo lkn kabla sijafanya hivi naomba msaada na maelezo mazuri nisije kupoteza pesa tena.

Lkn pia p.o box nililotumia nimetumia la sehemu napofanya kazi,kama hamtojali basi naitaji maelekezo
 
Sasa unataka msaada gani mkuu? Be specific unachotaka kujua maana maelezo yako mzozo kidogo
 
Sasa unataka msaada gani mkuu? Be specific unachotaka kujua maana maelezo yako mzozo kidogo
[/QAsante mkuu,naitaji hatua ya kwanza napoanza kuagiza mzigo mpaka ya mwisho kupokea mzigo ili nijue nilikosea wapi
 
Vitu hua vinafikaga vizuri kabisa wala usiwaze mimi nishaga agiza muffler ya gari ingawa ilikua tofauti na nilivyoona kwenye picha, Spot Lights, saa, mikanda, taa za kuwaka ndani ya gari, radio ya gari,etc ingawa vingine vilichelewa sana
 
Hatua ya kwanza jisajili kwenye mtandao unaotaka kununua bidhaaa,eg AliExpress

Humo utajaza data zako fresh ikiwepo na adress yako bila kukosea postcode ya eneo lako

Hatua ifuatayo,fanya manunuzi ,tumia mpesa mastercard kufanya payments ni rahisi sana..

Subiria mzgo wako huku ukiwa una utrack,ukifka posta nenda na ID yako utapewa furushi lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…