Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo)

Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo)

Kuna watu wananishangaa kwa msimamo wangu wa zero tolerance kuhusiana na uzinifu. Wanauliza sasa Ngabu wewe utaacha wangapi kama huna moyo wa kusamehe kila unapocheatiwa.

Narudia tena. The moment I find out my woman has cheated on me it's over! Kaput. Hata kama mwishowe nitakuja kuacha wanawake milioni moja then so be it. I just don't put up with that kind of B.S..

I value my dignity to the nth degree and getting two-timed is an ultimate insult to me. You cheat on me I dump on the spot and keep on moving.

So to me infidelity is completely and thoroughly unacceptable. It's black and white. No in between.
 
Bishanga unatumia kinywaji gani?... Ngoja nikuitie weita, Bili kwangu

Inabidi watu waache unafiki na kufuchaficha mambo tuyaweke hadharani ili ufumbuzi upatikane...

Kuna watu wana miaka 60+ watoto wao wamemaliza chuo wana kazi lakini mzee anamiliki nyumba ndogo
Hebu niambie hawa nao wataitwa wa mtaani

Ni ndoa ngapi watu wanaishi kama masanamu tu... baba ana chumba chake na mama ana chumba chake hata kwa miaka 10, utasema ni nyumba ndogo? Tuweni wakweli
ahsante ,kinywaji changu mimi ni mateka wima,kwa leo niko Mwanza,tukutane mlango mmoja.
Darlington,kuna mtu aliwahi kujisemeaga humu mmu kuwa maisha ni sinema and we are all actors.
 
Hakuna muujiza wowote unaopatikana kwenye nyumba ndogo..............ni tamaa tu na sredi kama zile za kuwatia moyo kufanya hivo. Wala sidhani kama mwanaume akiamua kuwa na nyumba ndogo kwamba kuna kitu kimepungua/anakikosa kwa mke wake na kosa hilo anapaswa abebeshwe mwanamke la hasha!! Wanaume acheni ubinafsi mjue hata wanawake wana mioyo kama mliokuwa nayo nyie, kumbuka kitendo usichokipenda wewe kufanyiwa kwa nini umfanyie mwenzio???

Ni kweli kabisa tena huko nyumba ndogo unakuta mtu anafokewa na kuamrishwa kama mtoto mdogo hafurukuti kabisa,lakini yupo tu.Akirudi kwa mkewe anajifanya mbogo ili asiulizwe.
 
ahsante ,kinywaji changu mimi ni mateka wima,kwa leo niko Mwanza,tukutane mlango mmoja.
Darlington,kuna mtu aliwahi kujisemeaga humu mmu kuwa maisha ni sinema and we are all actors.

kweli Maisha ni sinema...

Dah, na hicho kinywaji cha kwenye sinema.... Ngoja ni google, sijui hii IBM itakubali
 
Mnatulaumu sisi nyumba ndogo ambao hatuna waume, hamjui kwamba asilimia kubwa ya wake za watu wanatoka nje ya nyumba zao kuja kunyang'anyana na sie tusio na waume? hamshangai walioolewa humu ni wengi ila wanaopinga ni wawili tu? Wengine mbona wako kimya ndio kusema hawana wivu? wanajua wanachokifanya.

Mimi kubishana ndio nimeishia hapa kwani wengi wetu hapa hatuzungumzii maisha halisi tena tunaona aibu hata kwenye keyboard tu ambapo ninaandika na hakuna anaenijua, je huko tunakojulikana.

Kukaa kimya sio kwamba tunasapoti NO .Nilivyo na hasira na nyumba ndogo naweza hata kujikuta napata BAN.Mie binafsi nilipambana nayo mpaka alihama mji.
 
Bishanga
sio kwa vile sijaoa basi siwezi kujua madhara ya nyumba ndogo, kila kitu kipo wazi tu na ukweli kila mtu anauona.

sijui una umri gani,maana wanaume wengine vijeba na hawajaoa,anyway my point is ukishaoa na ukadumu kwenye ndoa yako say for ten years,rudi tena kwenye thread hii uone kama msimamo wako wa leo utakuwa ni ule ule,best wishes
 
Nimeishi maisha mazuri sana na ninaendelea kuishi, nimelelewa vizuri kwenye familia ya kikristo inayomjua Mungu, nimesoma vizuri, nimekua vizuri..., lakini maamuzi ya kuishi maisha ninayopanga mimi ni yangu, sio ya mzazi... Uovu, kila mtu ana tenda ovu lake... mwisho wa siku ni juu yangu na Mungu wangu. Maisha ya zamani yahamfanyi mtu kuamua kufanya anachofanya

Ila bado umegoma kunisimulia nyumba ndogo alifanyaje mpaka ukatelekezwa?

Darlingtone
wewe ni nyumba ndogo so hapa ni lazima tu utatetea yale uyafanyayo ila ukweli unabaki pale pale ninyi JANGA ktk ndoa za watu.

Abt mm kusema kusema nyumba ndogo mfano wewe ambaye hujutii jambo hilo ni kutokana na maisha mliyopitia huko utotoni sikumaanisha kuishi maisha mabaya NO.
May be ww mwenyewe ulikua mtoto wa Nyumba ndogo then ukaja ukawa mtoto wa nyumba kubwa, or mamdogo wako alikua nyumba ndogo ya mtu,or umeishi na ur frnds ni watoto wa nyumba ndogo n.k n.k n.k
so nyumba ndogo kwako imekua jambo la kawaida umeweza hata kuli practice na upo hapa kulitetea.

Abt unaposema nimegoa kukusimulia sijakuelewa hebu funguka vizuri.
 
Dear JF Members....


Wale mnaowakilisha Waume zetu... Wale ambao tunawakilisha nafasi yetu ya Mke halali..... Na wale ambao wanawakilisha nyumba ndogo....


Kwa Waume Zetu..... (Akina Shem ODM, Darling Kaizer (thou u have kwepad), Klorokwin, The Boss, EMT, Mbu, Bishanga, RR and Co)

Nawapongeza kwanza kwa kuunda kikundi cha kuchekelea Nyumba ndogo na jinsi ya Kumaintain... Pia nawapongeza kwa katiba yenu ambayo muongozaji mkubwa na Msimamiaji maandishi ni Teamo.... Then Kubrash chama kuna silent member ambae sasa ni Active kaja with a "Bang" The Boss....

Nimeshangaa saana response yenu katika huu uzi.... Maana ule uzi wa the Boss I got an impression that you guys when infidelliting knew what you did and what you are about... Kwamba however or much you cheat... Kwanza kabisa heshimu Mkeo na familia yako... I said to myself kwamba cheating ni kubwa saana BUT if these Men (hubbys and dads) wana huu msimamo.... Then at least i am proud kua their families are safe.... However I am genuilnely dissapointed na response yenu on the threa enthusiatically kabisa mko kupongeza kazi nzuri za nyumba ndogo na kuwakandamiza wake zenu.... You think we don't know kua you cheat?? OK... Cheating za pishana wengine wanajenga huku wengine wakipanga... BUT still almost all of you cheat!

Narudi kwenye miongozo ya hizo promo zenu.... Hive THE GUIDE TO HAVING NYUMBA NDOGO MMESOMA??? - Ya The Boss???? Maana mliweka ma LIKE kibao na kusupport kua that is the way it should be.... Are you guys serious kwamba ile guide mwaifuata?? Au sie ambae tunakua cheated upon ndo tumeielewa kuliko nyie.... For in brief ile Guide inatoa mwongozo kua never ever give an upper hand to Nyumba ndogo dhidi ya wife... Kwa kutumia tu hichi kipengele cha kwanza... Mmefeli.... Hapo zijaenda ya pili hadi mwisho.... Sijaona alofaulu katika hicho kipengele kilichoandikwa na nyie wenyewe watalaam wa nyumba ndog.... Nawashauri mpitie upya kanuni zenu....

1.Nyumba ndogo LAZIMA iwe na heshima kwa mkeo na wewe mwenyewe,
akileta dharau au kujifanya ana mrusha roho wife,UNAPIGA CHINI FASTA.....
hii ndio kanuni ya kwanza na muhimu na ndio muongozo wa mpango mzima..
kama hutaki mkeo ajue,basi iwe hivyo,na sio vinginevyo,marufuku mashindano kati ya wife
na nyumba ndogo...bora zaidi wasijuane wala kukutana kwenye shughuli zao...


Kwa walowakilisha Nyumba Ndogo.... (The so proud and fierce ladies Darling tone and Sarafina plus the pop up ram)

Kuna baadhi ya post mmeniquote ambazo inatakiwa niwajib... BUT then nimegundua kua najirudia kama mnavojirudia.... Kuna sehemu hapo nyuma EMT Kagusia kua wanawake hatupendani... Which is true for we are always in competition... Hivo siwashangai... na wala sioni ajabu kwamba mwajimwaya na mwaona raha kuelezea role yenu katika hizo infidelity... Who wouldn't after all waume zetu hapa wameonesha wako so weak hearted kwenu na wala hawana say.... Wameshindwa hata mmoja (with an exception ya Mtumish ambae nae ha-qualify for he is not married.. na wengine wachache ambao wanachungulia na kuondoka) kututetea na kutusimamia sie wake zao... Kwamb Ok... YES jamani we do cheat... But mambo ya huko yaacheni huko huko na msituletee wake zetu.... Nime observe saana hii.... Darling tone + Sarafina... Msingepata support ya hawa waume zetu i.e ODM, Klorokwini, Bishanga, et al.... labda ni mda mrefu mngekua mmeachia mjadala njia... BUT Lucky you ladies it seems hatuna power over our hubbies hata tu kutusimamia ni time of need.... The good thing about kua nyumba ndogo ni kua you can be a wife in the long turn na kumpiga teke the original wife (ukikuta kila kitu kimeendaliwa with the help ya wife anaepigwa teke) wee inakua hapo kwa ajili ya starehe... Who can blame you?? After all its survival of the fittest... That is why i HATE nyumba ndogo maana familia nyingi saana zinaharibika... Whereas "hit and runs" ni safer... Sometimes they even spice up the marriage... Hivo nawapongezeni.....


To my Fellow Married Women....

I don't know what to say.... Najua Mmeumia na mwaendelea kuumia.... BUT naamini kwamba it is beta we learn to stand up for ourselves... na kutokubali upuuzi wa akina baba ambao wanaamini tu eti sababu you are married na umezaa you can not live even if he is shit and full of bull shit!!! Nashukuru Nyumba Kubwa kwa nguvu yako hapa... Nakushukuru Roulette kwa Counter thread... Nashukuru wale wote walotupa support hata kwa post moja.....


Pamoja Saana

AshaDii...

 
Darlingtone
wewe ni nyumba ndogo so hapa ni lazima tu utatetea yale uyafanyayo ila ukweli unabaki pale pale ninyi JANGA ktk ndoa za watu.

Abt mm kusema kusema nyumba ndogo mfano wewe ambaye hujutii jambo hilo ni kutokana na maisha mliyopitia huko utotoni sikumaanisha kuishi maisha mabaya NO.
May be ww mwenyewe ulikua mtoto wa Nyumba ndogo then ukaja ukawa mtoto wa nyumba kubwa, or mamdogo wako alikua nyumba ndogo ya mtu,or umeishi na ur frnds ni watoto wa nyumba ndogo n.k n.k n.k
so nyumba ndogo kwako imekua jambo la kawaida umeweza hata kuli practice na upo hapa kulitetea.

Abt unaposema nimegoa kukusimulia sijakuelewa hebu funguka vizuri.

Kwa kweli sioni argument yako... Hapo kweny red sina mahusiano nayo kabisa...

Baba yangu ni mume wa mke mmoja na bado wanaishi na mama in their early 80's

Kama wewe ni muathirika wa nyumba ndogo, tueleze...
 
Narudia asilimia kubwa ya wanaume wanacheat; lakini ni asilimia ndogo sana (ambao nawaita mbumbumbu) ndio wana mantain nyumba ndogo.

Nitolee mfano wa baba yangu; alikuwa ni kiwembe sana; lakini alikuwa anajisifu mbele yetu kuwa yeye ni baba mwenye heshima zake na hawezi kulala nje ya nyumba yake wala kuzaa hovyo. Sisi wote ni watoto wa mama mmoja na baba hakuwahi kuzaa nje wala hakuwahi kuhudumia nyumba ndogo japo alikuwa anapiga sana nje (may be alikuwa anatumia protection kwani kwa speed yake angeukwaa; but he is still healthy and alive)

Kwa hiyo wanaume wanaohudumia wanawake nje nawahita malimbukeni; wajanja hawaweki makao.

Nimefanya kazi na wanaume wengi tu lakini ni mmoja so far ndiye najua ana nyumba ndogo; the rest ni wajanja wana hit and run.
. And strange enough mdogo wangu alipata mchumba baba akamwambia hilo si kabila la kuoa wanatabia ya kuhamia kwa wanawake wa nje. Hence to me mwanaume mwenye akili hawezi jisifu eti kuna mwanamke namuhudumia; huku ni obvious anapewa mgao tu huyo mwanamke anaye wa kulala nae jamaa akienda kwa wife.

Sasa nyie wanaume pimeni; ni wale wa kupangishia wanawake nyumba?? Then nyie ni malimbukeni; wajanja hawafanyi hivyo na ni wengi ambao nawaweka kwenye kundi la wajanja.
 
The idea that it's okay for married men and women to sleep with hookers (on a one-night stand basis) but it's not okay to maintain a long term relationship with a paramour is downright preposterous!
 
kweli Maisha ni sinema...

Dah, na hicho kinywaji cha kwenye sinema.... Ngoja ni google, sijui hii IBM itakubali

unywaji wa mateka wima:
rule no 1:kabla hujaanza kunywa miguu ya suruali unaibana na kamba au rubber band kwa chini karibu na unyayo,
rule namba two: hakuna kwenda toilet
rule namba three: once ukinyanyuka breki ya kwanza chooni nyumbani kwako na suruali uifue huko huko! Usicheze na mataptap bana!
 
sijui una umri gani,maana wanaume wengine vijeba na hawajaoa,anyway my point is ukishaona na ukadumu kwenye ndoa yako say for ten years,rudi tena kwenye thread hii uone kama msimamo wako wa leo utakuwa ni ule ule,best wishes

kudumu kwenye ndoa na nyumba ndogo is two diffent thngs mkuu.

Hapa nazungumzia small house na jinsi ya kuziepuka.

Well sijaoa na siwez kuweka % mia kuwa ndoa yangu itadumu hapo ita depend na mwanamke mwenyewe na life inavyokwenda siku hadi siku akitaka kuwa limbukeni i will kick her out siwezi kuvumilia upumbavu anisaliti kwa kugawa nje then nimsamehe kwa kuwa tu nataka ndoa idumu.
Na kwa staili hiyo ndio mana wale wenye nyumba ndogo wanafanya uzinzi wakiamini wake zao watawasamehe kwa kigezo cha ndoa kudumu!

Hata ndoa za nyingine hakuna talaka lakini bado vitabu vinasema Kila mtu awe na mke wake mwenye na wasitengane ISIPOKUA tu kwa UZINZI.

Bishanga labda nikuulize tu je ww uko ready kuibiwa mke wako? I mean mkeo awe na kidumu nje akipangishie chumba kiwe kinamburudisha huko! Utakubali?
 
Kale kabatani kamepotea. Kakirudi ntakugongea.

Mpaka sasa Maisha halisi yanaongoza kwa bao tatu dhidi ya moja la Maisha ya kusadikika

Wafungaji wa Maisha halisi ni Wewe, Darlington na Sarafina1 wakati lile la kufutia machozi la Maisha ya kusadikika limefungwa kwa Penalti na AshaDii shemeji yangu.

Mpira bado unaendelea na dakika zilizobakia ni tatu.

Baada ya kusema hayo, naomba nikusalimu na kukuomba urafiki.

I'm good! Karibu
 
AshaDii shem wangu hapo juu.......

Pole sana. Nimekusoma na nimeziona feelings zako. Kiukweli siyo kwamba tunasupport ila tunaelezea hali halisi ilivyo........ Kwa mfano kwangu mie my wife is everything and she always come first. Sitegemei hata siku moja eti nnayecheat naye anaweza kumpindua! Nina miaka takriban kumi ya ndoa mama watoto wangu hajawahi hata kunihisi kama nimeshawahi kumcheat!

Tuko nyuma yenu wake zetu, we do support you and we love you. Lakini hapa kinakuja kitu ambacho kwa wanaume ni vigumu sana kukikwepa.......naturally mwanaume ni vigumu sana kuridhika kuwa na mwanamke mmoja. Ndiyo hali halisi na ukweli ambao haupingiki. Tunayaona na kuyashuhudia mengi. Thats why sie wakongwe tunawasihi vijana wetu, shetani litakapowaingia wakajikuta wanacheat then wacheat responsibly. Siyo kufanyia sifa na kuleta ubazazi utakaosababisha ndoa zao kuparanganyika.

Baada ya kusema sayo, mie ODM kwa niaba ya watu wote waliokukwaza tunakuomba utusamehe bure na kukuomba uukubali ukweli huu ambao kwa hakika uko wazi kabisa.
 
kudumu kwenye ndoa na nyumba ndogo is two diffent thngs mkuu.

Hapa nazungumzia small house na jinsi ya kuziepuka.

Well sijaoa na siwez kuweka % mia kuwa ndoa yangu itadumu hapo ita depend na mwanamke mwenyewe na life inavyokwenda siku hadi siku akitaka kuwa limbukeni i will kick her out siwezi kuvumilia upumbavu anisaliti kwa kugawa nje then nimsamehe kwa kuwa tu nataka ndoa idumu.
Na kwa staili hiyo ndio mana wale wenye nyumba ndogo wanafanya uzinzi wakiamini wake zao watawasamehe kwa kigezo cha ndoa kudumu!

Hata ndoa za nyingine hakuna talaka lakini bado vitabu vinasema Kila mtu awe na mke wake mwenye na wasitengane ISIPOKUA tu kwa UZINZI.

Bishanga labda nikuulize tu je ww uko ready kuibiwa mke wako? I mean mkeo awe na kidumu nje akipangishie chumba kiwe kinamburudisha huko! Utakubali?

we hujui kinachoendelea nyuma ya pazia la ndoa, nshasema huko nyuma kuwa wake za watu kibao wanapigwa paipu na waume zao wanajua lakini for some reasons wanaminya.Sitaki kuongea mengi kuhusu visa vya wanawake lakini mtu wangu wa karibu sana ashawahi kuambukizwa kisonono na mkewe na mpaka leo yuko naye.Tatizo kwenye thread hii wachangiaji wengi (kina AshaDii et al) wameegamia kwenye mfumo jike as if wao ni malaika kumbe wapi ni wazambi tu kama sisi.
 
Thread ya The Boss imemsaidia sana rafiki yangu na anasema kwa sasa mambo yake yanakwenda vizuri,kaweza kubadilisha upepo ambao ulikuwa unamuelemea baada ya kumpa notes toka kwa the Boss,tukubaliane tu kuwa kila kitu duniani kina sura mbili na huwezi badili hilo,kuna watu wanaoponda kuhusu kuwa na nyumba ndogo lakini kwa wale walionazo ambao the Boss aliwalenga imewasaidia kuishi kwa amani zaidi bila bughudha.

hizo ni sababu tu nyepesi nyepesi mnazotoa ili kutaka kuhalisha UOVU lakini bado ukweli unabaki pale pale nyumba ndogo ni JANGA kwa ndoa za watu. Ni kuikosea jamii heshima.
sisi wote kama tunataka jamii bora kamwe tusi support nyumba ndogo.
 
Mimi bwana..........Mimi kazi yangu ni kugonga tu! kashuhudie kule.

Hapa kibaruani kuna wadada wawili nadhani watakuwa waimba kwaya au watumishi kanisani kwa jinsi wanavuoonekana nadhifu na wenye heshima. Lakini wanavyotafunwa na madereva, huwezi amini! Ndio, ni wake za watu hawa! Na waume zao wanawaleta kazini na kuwafuata jioni.

Ndo maana ODM nlishajiapizaga.......... Sitakanyaga ofisini kwa wife wala kuhudhuria shughuli yoyote inayoandaliwa na kampuni yao ambayo itahitaji spouses kuhudhuria........... Nani anapendwa kung'ongwa?

Tukutane nyumbani, tumalizane nyumbani.

Baada ya kusema hayo, ODM anarudi kitandani kuiombea Tanzania ishushe angalau bei ya sukari, kama kushusha bei ya petroli haikubaliki kama malaria.

Asprin utanifanya nipaliwe na chakula(i'm eating right now)yaani nimecheka aahhh jamani hizi story za wake za watu wanaoliwa mimi ndio sitaki hata kusimulia ni aibuuuuuuuuuu hiyo ya kushushwa na kufatwa halafu in between mamaaa anaenda kucharika maeneo anarudi saa nane flani hivi daahh nishai kweli. Kwa ufupi nyie midume mnaojifanya mna cheat na kuamini kuwa wake zenu ni wasafi sana na hawafanyi POLENIIIIIII
 
Back
Top Bottom