Mwanamama selebu namba 2 wa JF Binti Foxy Faiza amezua gumzo kufuatia kila anapokwenda kuwa na kufuli kwenye mkoba ambalo mwenyewe anadai ana matumizi nalo.
Chanzo chetu ambacho ni rafiki wa mwanama shosti huyo kilichojitambulisha kwa jina moja Rejao kilitonya kuwa, FF amekuwa na tabia ya kutembea na nguo hiyo ya ndani na wakati mwingine kuitumia kujifutia jasho.
Nilishawahi kuishudia ile nguo ya ndani, ina rangi ya maziwa hivi. Siku moja tulikuwa maeneo flani tunapiga stori, mara akaitoa na kujifutia jasho, alisema Rejao
Akasema mbali na kuitumia kwa matumizi hayo, siku moja alipomtembelea nyumbani kwake alishangaa kuitumia nguo ileile kujifutia uso, hivyo kumfanya amfikirie tofauti.
Katika kuweka mambo sawa alitafutwa FF na mahojiano yalikuwa hivi:
Mimi: Unadaiwa kutembea na kufuli lako kwenye mkoba na watu wanalihusisha na mambo ya kishirikina, wewe unalizungumziaje hilo?
FF: Hee! Hayo ni maamuzi yangu bwana, kwani kuna tatizo gani?
MImi: Lakini kwa nini utumie kufuli kujifutia jasho, kwani umeshindwa kununa kitambaa? Huoni kwamba unawafanya watu wakufikirie tofauti?
FF: Wanifikie vyovyote, hayo ni maamuzi yangu.