Haya ndio ya makundi ya watu wa JF na tabia zao

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,138
22,507
JF imejaa watu wa kila aina na ndio hawa hawa tunaishi nao mtaani, wengine pia ni ma diaspora, viongozi nk.

Haya ndio makundi ya J na karibu kila mtu yupo kundi tajwa na tabia zake kama ifuatavyo.

1: Wapenda siasa
Hapa wapo watu ambao wao utawakuta kwenye jukwaa la siasa tu, maisha yao na uwepo wao jf wameamua kuutumia kujadili siasa safi na structure zake.. Huwa sio watu wa mbwembwe nyingi.
Pascal Mayalla anasimama hapa

2: Wapinga serikali
Hawa kila kitu kinachofanyika kuhusu serikali lazima wapinge kwa nguvu zote..Pasipo na aababu ya msingi, wao furaha yao ipo hapo, na huamua kumalizia stress zao hapo. Yaani akinyimwa hata kifanyio na mkewe atailaumu serikali, akilala njaa lawama kwa serikali, akidaiwa kodi lawama kwa serikali. Siku hizi wamehamia kwa diamond Sadala.
BAK , imhotep , Wangari Maathai , Behaviourist Afande Tanzania, Sky Eclat wanachukua namba hapa


3: Wavuruga Mada (vimbelembele)
Hawa kazi yao ni kuvuruga mada za wengine, kwani hupenda kuingiza kitu tofauti na mada yenyewe ili mradi tu wafurahishe nafsi zao mfano, utakuta mtu anaongelea ajali iliyotokea maeneo ya salasala. Lakini mtu anakuja kujibu "eeh shoga mbona kule kwa jana sijakuona?", halafu mwenzie anajibu " shemeji yako aliniweka kwapani shoga eeh nipe ubuyu send off ya felista"
Wangari Maathai , Madame B ,
Wanawakilisha

Au utaskia "mie madini nayaheshimu sana,nilizamia chato kutafuta! Lakini kiuhalisia hajawahi hata kukanyaga huko mgodini..
Mada inahusu mtu aliyezamia bondeni akielezea mkasa wake, wao watakuja kati kati na Kuanza ngendembwe zao " yaani wanawake tunaweza pia kuna Dada alikuwa anauza ndala za kimasai mgodini saivi ana duka kubwa ni broker"

"nilizamia ludewa Nilikuwa nakula wali mkavu ili nisave hela" ama utawaskia "jana shoga shemejio kanibana wakati mie simba anacheza!"..

4: Wajuaji (much know)
Hawa watu wa kundi hili ndio wamejaa wengi sana, yupo radhi aka google fasta na kuja kuendelea na arguments mpka kuchee!
Watu hawa wanajua siasa, soka, mapenzi, ujambazi, umalaya, utafutaji, technology, uchawi, wanyama, muziki, style zote za kusasambuana.. Huwezi kubishana nao ukawashinda watu hawa.
Mshana Jr , Kiranga , joseph1989 , Chige Wangari Maathai japo huyu hajui google.

Utawaskia mara kadhaa "ash wewe sauzi nimekaa sana, huwezi kupata warembo wa kishua sana sana utawapata malaya"
Au "harmonize amekengeuka kesho Yake itakuwa ngumu sana" kana kwamba yeye ni Mungu mpaji wa vyote..

5: Wasioguswa (untouchable)
Hawa ndio wanaomiliki jf! Kwa lugha nyingine ni kuwa wana ushawishi mkubwa na wamejitengenezea Image ya kuaminika! Kiasi kwamba akisema haya ni makalio wakati ni kichwa kuna kondoo wanaamini. Na ole wako ubishe uone utakavyoshukiwa na kondoo kama mwewe!
Mshana Jr ,yupo hapa

"una stress" , tafuta hela" hayo ni maneno utaambiwa na kondoo wao. Akikugusa wewe ni sawa ila ukimgusa yeye utaambiwa "wapuuzi dawa yao ni kuwapuuza"
"punguza uchawi"

6: Matapeli
Hawa ni kundi la Wale ambao siku zote huwa wanakuja kulia lia shida na kuombwa kusaidiwa na mara nyingi huwa ni msaada wa kifedha tu! "nimekata tamaa ya maisha nataka kujiua" ni baadhi tu ya maneno utayaskia kama hayo. Nilipata ajali nimebaki shingo tu! Nashindia maandazi na maji ya kandoro.. Kwaherini wana jf hamtoniona tena" then ana log out (hapa sitaki umbea)

7: Malaya waliokubuhu
Ndio ni malaya! Ni malaya! Hana jamvini mara nyingi kila mtu analinda legacy yake hadharani. Waswahili hawakukosea kusema hakuna mkate mgumu Mbele ya chai. Wapo watabe wengi wamejipatia matunda humu kwa bei sawa na bure au bure kabisa na wala huwezi jua. Japo ni maamuzi ya watu hao wawili mimi sitaki umbea. Mara nyingi public hujifanya kujiheshimu sana na kukemea uzinzi karihu wote, sasa hizi geti zinazojaa sijui huwa zinajaza mbuzi bandani ama? Uzi wa kuliwa kimasikhara ni shahidi yangu

8: Washauri wazuri
Hawa ni watu ambao akikupa ushauri unaweza dhani huyo ni malaika anakaa mbinguni. Yaani anakupa A to Z na unaelewa wazi tatizo lako liko wapi. Sad news ni kwamba hatujui maisha yao background hawa adviser kama wanatekeleza haya wanayoshauri, kuna mmoja alikuwa ni bingwa wa ushauri kuhusu mahusiano lakini cha ajabu. Binti yake wahuni walimjaza mimba aka jazwa ujazwe au both team to score
Chief-Mkwawa yupo hapa

9: Watu wa masikhara na mizaha
Hapa ndio wapo wengi sana kiss kwamba mtu akiwa mgeni basi anaweza dhani wamejaa watu hao tajwa tu..
Wanaweza leta mizaha hata kwenye mambo muhimu
Ushimen ,Asprin , Extrovert na wenzao.

10: Wazee wa kufake life (kujifaragua, kujishongondoa)
Hawa ndio wapo asilimia 98 humu. Maana kila mtu atakwambia ana gari, tena ni kali sio passo wala vitz sijui vinini.
Lakini sasa sijui hizi vitz tunazoziona mtaani ni bata wanaendesha? Hata akiweka mada lazima katikati achomekee, " mwaka jana nilipoenda Dubai kisha nikapitia paris nilikuta weusi wengi sana wana maisha magumu" Au mie juzi nilipokula kitimoto kilo 5 ilinipa kichefu chefu sijui watu mnakula vipi?" Ama "jack Daniel ile ya laki 6 ndio nzuri hivi vya 20k ladha yake huwa inanichefua..

Lakini ukija kumuona live huyo aliyeenda paris utakuta kavaa kiatu kinacheka kwa huzuni, ndevu na shati lake utadhani limetoka kuliwa na ng'ombe! Na huyo wa jack Daniel utamkuta kavaa Dela la buku 6 na akitoka basi ujue anaenda kunywa K vant aka kifutio ili asahau shida haraka. Mwengine atakwambia juzi nilikuwa congo kukutana na mtoto wa koffi olomide, ni Best angu sana" wakati kiuhasilia utakuta anakaa bonyokwa na kamfata Best ake kwa mpalange.

Mwengine atakwambia" nilifanya tour last year December kwa Range Rover discovery yangu, aiseeh it was good adventure"
Kumbe jamaa mwenyewe kabanana ndani ya ki passo na ukute ni mnene Kama tembo..
Wangari Maathai , Anawakilisha wengine wotee

11: Wasimbe (hawajaoa wala kuolewa)
Hapa wako wengi sana asilimia 89 wapo wapo tu, ni watu wazima kabisa lakini kuoa/ kuolewa wanaona kama watakufa leo mke arithi mali, mali zenyewe ukute ni kijiko na kuku wawili wenye ugonjwa wa mdonde.

Wapo pia wenye maisha mazuri humu lakini hawa na ndoa ni sawa na swala na simba! Kazi yao kuviziana na kunyanduana kisha wanashika 50 zao, mtu kishapata kipara cha uzee na kichwa chenyewe kilivyo kama sofuria la jela lakini hataki kuoa

12: Spana mkononi
Hawa jamaa kukuta wamepigwa ban ni kawaida sawa na kunywa maji, yaani ni kama mbwai iwe mbwai hawaogopi kukupa za uso, uwe umezingua wewe au yeye haijalishi spana ipo mkononi any time.
GENTAMYCINE ,Mkaruka
Wyatt Mathewson

Kama umetajwa mara nyingi basi uje unipige


Kama mtanipiga mawe haina noma.
NB: naona watu tajwa baadhi wameniwakia sana hasa kundi lile namba 10,
Ingawa mimi nimeleta ukweli wenyewe pasipo kumshambulia mtu binafsi,
Watu wa kundi namba 10 wengine wameniita punga, wengine wamesema sina kazi, wengine wamesema nakariri sana,
Hii ni ishara kwamba ubongo wangu unafanya kazi extra kuliko hao namba 10 wanojishongondoa vitu ambavyo hawana, hivyo kama mna shida msisite kuniambia Sisi wote ni ndugu nitawasaidia hata pesa ya mafuta kwenye passo zenu...(group 10)

After all hii mada hapa haijakaa kumshambulia mtu bali ni mzaha kama alivyosema Watu8 .
Hivyo watu wa group namba 10 mtulie tu nimeshawatumbua kama wenzenu walivyotulia,
Mnataka niwape kazi yangu ili mnidangie sio? Hamnipati kama kutumbuliwa nimewashawatumbua japo inawauma kwa ndani ndani, lakini mbona wenzenu hawajamaind? Ni nyie tu?
Tusisahau niko hapa karibu mwaka wa 4... Na wala sijakosea,
Niuweni tu 😀😀😀
nalog out...
 
Jf imejaa watu wa kila aina na ndio hawa hawa tunaishi nao mtaani, wengine pia ni ma diaspora, viongozi nk..

Haya ndio makundi ya jf na karibu kila mtu yupo kundi tajwa na tabia zake kama ifuatavyo.

1:Wapenda siasa..
Hapa wapo watu ambao wao utawakuta kwenye jukwaa la siasa tu, maisha yao na uwepo wao jf wameamua kuutumia kujadili siasa safi na structure zake.. Huwa sio watu wa mbwembwe nyingi..

2: wapinga serikali.
Hawa kila kitu kinachofanyika kuhusu serikali lazima wapinge kwa nguvu zote..Pasipo na aababu ya msingi, wao furaha yao ipo hapo, na huamua kumalizia stress zao hapo.

3: Wavuruga Mada (vimbelembele)
Hawa kazi yao ni kuvuruga mada za wengine, kwani hupenda kuingiza kitu tofauti na mada yenyewe ili mradi tu wafurahishe nafsi zao mfano, utakuta mtu anaongelea ajali iliyotokea maeneo ya salasala.
Lakini mtu anakuja kujibu "eeh shoga mbona kule kwa jana sijakuona?", halafu mwenzie anajibu " shemeji yako aliniweka kwapani shoga eeh nipe ubuyu send off ya felista"
Au utaskia "mie madini nayaheshimu sana,nilizamia chato kutafuta! Lakini kiuhalisia hajawahi hata kukanyaga huko mgodini..

4: Wajuaji (much know)
Hawa watu wa kundi hili ndio wamejaa wengi sana, yupo radhi aka google fasta na kuja kuendelea na arguments mpka kuchee!
Watu hawa wanajua siasa, soka, mapenzi, ujambazi, umalaya, utafutaji, technology, uchawi, wanyama, muziki, style zote za kusasambuana.. Huwezi kubishana nao ukawashinda watu hawa.

5: Wasioguswa (untouchable)
Hawa ndio wanaomiliki jf! Kwa lugha nyingine ni kuwa wana ushawishi mkubwa na wamejitengenezea Image ya kuaminika! Kiasi kwamba akisema haya ni makalio wakati ni kichwa kuna kondoo wanaamini.
Na ole wako ubishe uone utakavyoshukiwa na kondoo kama mwewe..!
"una stress" , tafuta hela" hayo ni maneno utaambiwa na kondoo wao.

6: matapeli..
Hawa ni kundi la Wale ambao siku zote huwa wanakuja kulia lia shida na kuombwa kusaidiwa na mara nyingi huwa ni msaada wa kifedha tu..!
"nimekata tamaa ya maisha nataka kujiua" ni baadhi tu ya maneno utayaskia kama hayo.

7: Malaya waliokubuhu...
Ndio ni malaya! Ni malaya!
Hana jamvini mara nyingi kila mtu analinda legacy yake hadharani.
Waswahili hawakukosea kusema hakuna mkate mgumu Mbele ya chai.
Wapo watabe wengi wamejipatia matunda humu kwa bei sawa na bure au bure kabisa na wala huwezi jua.. Japo ni maamuzi ya watu hao wawili mimi sitaki umbea...

8: Washauri wazuri..
Hawa ni watu ambao akikupa ushauri unaweza dhani huyo ni malaika anakaa mbinguni..!
Yaani anakupa A to Z na unaelewa wazi tatizo lako liko wapi...
Sad news ni kwamba hatujui maisha yao background hawa adviser kama wanatekeleza haya wanayoshauri...

9: Watu wa masikhara na mizaha.
Hapa ndio wapo wengi sana kiss kwamba mtu akiwa mgeni basi anaweza dhani wamejaa watu hao tajwa tu..
Wanaweza leta mizaha hata kwenye mambo muhimu

10: wazee wa kufake life (kujifaragua,kujishongondoa)
Hawa ndio wapo asilimia 98 humu
Maana kila mtu atakwambia ana gari, tena ni kali sio passo wala vitz sijui vinini.!
Lakini sasa sijui hizi vitz tunazoziona mtaani ni bata wanaendesha?
Hata akiweka mada lazima katikati achomekee, " mwaka jana nilipoenda Dubai kisha nikapitia paris nilikuta weusi wengi sana wana maisha magumu"
Au mie juzi nilipokula kitimoto kilo 5 ilinipa kichefu chefu sijui watu mnakula vipi?"
Ama "jack Daniel ile ya laki 6 ndio nzuri hivi vya 20k ladha yake huwa inanichefua..

Lakini ukija kumuona live huyo aliyeenda paris utakuta kavaa kiatu kinacheka kwa huzuni, ndevu na shati lake utadhani limetoka kuliwa na ng'ombe!
Na huyo wa jack Daniel utamkuta kavaa Dela la buku 6 na akitoka basi ujue anaenda kunywa K vant aka kifutio ili asahau shida haraka...

Kama mtanipiga mawe haina noma
Nimecheka sana mkuu.
 
Back
Top Bottom