RYZEN 5 Custom built PC

h120

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
2,532
3,316
Habari zenu wana tech,

Narudi tena na tena kwa mara nyingine, lengo kuu likiwa ni kufahamishana kuelimishana na kuhamasishana kwenye nyanja hii muhimu ya Tech, Gadgets & Science Forum.

Kama kawaida huu uzi ni muhimu kwa wale wazee wa Custom built PC kutegemeana na malengo ya muundaji.

Kwa tusiofahamiana unaweza kupitia nyuzi hii ya nyuma yenye maudhui sawa kabisa na hii Wapenzi wa Gaming Pc & Building

Leo narudi na project Ryzen, nilifunga mashine ya intel kipindi hicho cha nyuma nikaja iuza, kwa sasa kulingana na mahitaji binafsi na shughuli zangu nimeamua kufunga kitu mpya ila safari hii nimeamua kwenda na CPU ya AMD zinazojulikana kama Ryzen, CPU hizi zina maboresho makubwa sana na zimeleta ushindani mkubwa sana kwa intel kuanzia perfomance mpaka unafuu wa bei.

Kwenye huu uzi nitaweka gharama zote pamoja na future upgrades ntakazo fanya, kwa sasa sijakamalisha 100% ila zile core components karibu zote zipo kwa hivyo taarifa zingine nitaongeza kulingana na vifaa vitakavyofika.

Baadhi ya tips muhimu ni kitu cha kwanza kabisa unapaswa kuchagua ni processor ni processor ya chaguo lako kisha inafuata MOBO(motherboard) na vingine vitafuata hivyo viwili ni muhimu sana na uchaguzi uatendana na bajeti yako pamoja na matumizi uliyokusudia, usifanye makosa ya kulipia gharama kubwa kwa features usizotumia ni matumizi mabaya ya pesa.

Computer Parts List

1. CPU - Ryzen 5 5600

ryzen 5.png

Description:
Class:
Desktop
Socket: AM4
Clockspeed: 3.5 GHz
Turbo Speed: 4.4 GHz
Cores: 6 Threads: 12
Typical TDP: 65 W
Cache Size: L1: 384 KB, L2: 3.0 MB, L3: 32 MB
Other names: AMD Ryzen 5 5600 6-Core Processor
CPU First Seen on Charts: Q2 2022
CPUmark/$Price: 155.06
Overall Rank: 296
Last Price Change: $139.00 USD (2022-12-02)

Kama zinavyoonekana hizo ndio specs za hii CPU Ryzen 5 5600, kuna version mbili kuna Ryzen 5 5600 na Ryzen 5 5600x, tofauti ya hizi models ni base frequency ya 200Mhz kwa gharama ya 30$ to 40$, sikuona ulazima wa kulipia 40$ kwa tofauti ya 200Mhz hivyo nikaenda na 5600 na si 5600X, kitu kingine muhimu cha kuzingatia ni kwamba hizi CPU mbili 5600 na 5600X hazina intergrated GPU, hivyo unalazimika kuwa na graphics card unapoamua kuunda PC kwa kutumia kati ya hizi cpu mbili, katika series ya 5600 kuna moja yenye Intergrated GPU ambayo ni 5600G ila yenye specs zake zipo chini kidogo ukilinganisha na 5600 na 5600X, kwa taarifa zaidi unaweza google.

Bei ya hii CPU mpaka kunifikia mkononi ni 370,000/=Tsh
Mahali nimenunua Aliexpress

2. Motherboard- GIGABYTE B550M AORUS ELITE

Gigabyte B550M Aorus Elite Motherboard.jpg

  • Supports AMD Ryzen™ 5000 Series/ Ryzen™ 5000 G-Series/ Ryzen™ 4000 G-Series and Ryzen™ 3000 Series Processors
  • Dual Channel ECC/ Non-ECC Unbuffered DDR4, 4 DIMMs
  • 5+3 Phases Pure Digital VRM Solution with Low RDS(on) MOSFETs
  • Ultra Durable™ PCIe 4.0 Ready x16 Slot
  • Dual Ultra-Fast NVMe PCIe 4.0/3.0 M.2 Connectors
  • High Quality Audio Capacitors and Audio Noise Guard for Ultimate Audio Quality
  • Realtek GbE LAN with Bandwidth Management
  • Rear HDMI & DVI Support
  • RGB FUSION 2.0 Supports Addressable LED & RGB LED Strips
  • Smart Fan 5 Features Multiple Temperature Sensors , Hybrid Fan Headers with FAN STOP
  • Q-Flash Plus Update BIOS without Installing the CPU, Memory and Graphics Card
  • Anti-Sulfur Resistors Design

Kwenye MOBO nimeamua kwenda na GIGABYTE kwa uzoefu nimeshatumia board zao sijapata changamoto yoyote hivyo nimeamua kuwatumia tena, key specs zipo hapo juu kwa full specs za board husika unaweza google utaona zote.

Gharama ya hii board mpaka kunifikia mkononi ni 408,000/-Tsh
Mahali nimenunua Aliexpress

3. Power Supply (PSU) - Thermaltake BT 600W Full Modular Bronze psu

bt600.png

Model PS-BTM-0600FNFABC-1
Watts: 600W
RGB fan: No
Maximum output wattage 600W
Colour: Black
Size: width said height said length 150mm(W) x 86mm(H) x 140mm(D)
PFC (Power Factor Correction) Active PFC
PG signal :100-500 msec
Shutdown hold time > 16msec at 70% of full load
Input frequency: 50Hz-60Hz
Input voltage: 100V – 240V~
Operating temperature: 5°C to + 40°C
Operating humidity :20% to 85%, non-condensing
Storage humidity: 10% to 95%, non-condensing
Storage temperature: -40°C to + 55°C
cooling system :12cm Hydraulic bearing fan
effectiveness: Meet 80 PLUS®Bronze at 115Vac input.
Mean time between failures 100,000 hrs minimum
Safety certification CE/CB/TUV/ UL/ FCC/ BSMI
PCI-E 6+2pin 2

Kwa upande wa PSU nimeamua kuchagua thermaltake BT600W full modular, ni power supply nzuri ina reputation kubwa hivyo ni brand inayoaminika na bei zao sio za kutisha, pia ni 80+, hivyo utumiaji wake wa kiwango cha umeme ni mzuri kwa maana ya ufanisi, kwa 600W inatosha kabisa kwa mahitaji yangu, ni muhimu kuchagua PSU kulingana expected load capacity ya components zako, kwangu mimi hii inatosha kabisa.

Gharama ya PSU mpaka kunifikia mkononi ni 290,000/-Tshs
Mahali nimenunua Alibaba

4. Computer Case- MSI PAG SHIELD 100L

A4RES2206150F8QPG50.jpg

Last build nilifanya wengi hawakupendezwa na chaguo la case niliyotumia, hata ilipofika wakati wa kuiuza changamoto kubwa ilikuwa case niliyotumia ilionekana ni ya kawaida sana kwasababu haikua na fancy case, nilitumia Case ya hp 7600 kama sikosei, hivyo ilipunguza thamani kiasi fulani japo uwezo wake wa ndani ulikuwa ni mkubwa ila iliangushwa kwa muonekano wake.

Kwasasa nimeamua kutafuta case nzuri yenye mvuto na mwonekano wa kuvutia hivyo basi yeyote atakaeiona anaweza kuvutiwa kwa nje kabla hata kujua yaliyomo ndani, case hii ni MSI PAG SHIELD ina nafsi ya kutosha, kwa components zote muhimu na vents za kutosha kwa ajili ya cooling iwe water cooling au air cooling.

Gharama ya hii case mpaka kunifikia mkononi ni 280,000/-Tsh
Mahali nimenunua Alibaba

5. RAM-Corsair vengeance LPX (2*8GB)

71EXOwFSf-L.jpg

RAM nimechukua hizi corsair Corsair vengeance LPX DDR4 16GB 3200Mhz, zitatosha kwa matumizi yangu japo nilitaka 32GB ila bajeti yangu sikutaka kuzidi kiwango nilicholipia kwa hizi memory stick.

Gharama nilizotumia ni 270,000/-Tshs
Mahali nimenunua Alibaba

6. Cpu Cooler-PA 120 SE TWIN TOWER COOLING

pe 120.png

Cooler nimeachagua hii iko na ratings nzuri nadhani itanifaa japo ni overkilling kwa hii CPU 😂

Gharama nilizotumia ni 150,000/=Tshs
Mahali niliponunua ni Alibaba

7. SSD- SAMSUNG M.2 SSD 240GB
Ninayo M.2 SSD nitaitumia kama boot drive

8. HDD- seagate 500GB
Hii pia ninayo nitaitumia kwa ajili ya storage

9. GPU (Graphics Card)
Hapa bado sijachukua ila natarijia kuchukua RTX 3060ti au 3070 japo bajeti, yake imechangamka nitaangalia kulingana upepo wa gharma.

Mengine nitaongeza kadri nitakapofikia.
Karibuni kwa mawazo, maswali, ushauri maoni nk.

cc
Chief-Mkwawa

UPDATES
** 06-12-2022**

IMG_20221206_100838.jpg

IMG_20221206_100715.jpg

IMG_20221206_100655.jpg

IMG_20221206_100854.jpg

IMG_20221206_100905.jpg

IMG_20221206_100747.jpg

UPDATES
** 16-12-2022**

IMG_20221216_122225.jpg

IMG_20221216_130007.jpg

IMG_20221216_122234.jpg

IMG_20221216_122425.jpg

IMG_20221216_122716.jpg

IMG_20221216_122720.jpg

IMG_20221216_130014.jpg

IMG_20221216_170354.jpg

IMG_20221216_171843.jpg

IMG_20221216_171933.jpg

IMG_20221216_174950.jpg

IMG_20221216_173516.jpg

IMG_20221216_173521.jpg
 
Attachments

  • IMG_20221216_173527.jpg
    IMG_20221216_173527.jpg
    475.8 KB · Views: 28
  • IMG_20221216_173735.jpg
    IMG_20221216_173735.jpg
    585.3 KB · Views: 28
  • IMG_20221216_174939.jpg
    IMG_20221216_174939.jpg
    1.2 MB · Views: 27
Mchanguo mzuri mkuu.. mimi naomba link kwa kina component hapo.. nisipate shda ya kusearch sana huko AliExpress na Alibaba

Na hzo links kama unatumia affiliated unaweza lipwa commission kwa kila purchase

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu wana tech,

Narudi tena na tena kwa mara nyingine, lengo kuu likiwa ni kufahamishana kuelimishana na kuhamasishana kwenye nyanja hii muhimu ya Tech, Gadgets & Science Forum.

Kama kawaida huu uzi ni muhimu kwa wale wazee wa Custom built PC kutegemeana na malengo ya muundaji.

Kwa tusiofahamiana unaweza kupitia nyuzi hii ya nyuma yenye maudhui sawa kabisa na hii Wapenzi wa Gaming Pc & Building

Leo narudi na project Ryzen, nilifunga mashine ya intel kipindi hicho cha nyuma nikaja iuza, kwa sasa kulingana na mahitaji binafsi na shughuli zangu nimeamua kufunga kitu mpya ila safari hii nimeamua kwenda na CPU ya AMD zinazojulikana kama Ryzen, CPU hizi zina maboresho makubwa sana na zimeleta ushindani mkubwa sana kwa intel kuanzia perfomance mpaka unafuu wa bei.

Kwenye huu uzi nitaweka gharama zote pamoja na future upgrades ntakazo fanya, kwa sasa sijakamalisha 100% ila zile core components karibu zote zipo kwa hivyo taarifa zingine nitaongeza kulingana na vifaa vitakavyofika.

Baadhi ya tips muhimu ni kitu cha kwanza kabisa unapaswa kuchagua ni processor ni processor ya chaguo lako kisha inafuata MOBO(motherboard) na vingine vitafuata hivyo viwili ni muhimu sana na uchaguzi uatendana na bajeti yako pamoja na matumizi uliyokusudia, usifanye makosa ya kulipia gharama kubwa kwa features usizotumia ni matumizi mabaya ya pesa.

Computer Parts List

1. CPU - Ryzen 5 5600

View attachment 2435792

Description:
Class:
Desktop
Socket: AM4
Clockspeed: 3.5 GHz
Turbo Speed: 4.4 GHz
Cores: 6 Threads: 12
Typical TDP: 65 W
Cache Size: L1: 384 KB, L2: 3.0 MB, L3: 32 MB
Other names: AMD Ryzen 5 5600 6-Core Processor
CPU First Seen on Charts: Q2 2022
CPUmark/$Price: 155.06
Overall Rank: 296
Last Price Change: $139.00 USD (2022-12-02)

Kama zinavyoonekana hizo ndio specs za hii CPU Ryzen 5 5600, kuna version mbili kuna Ryzen 5 5600 na Ryzen 5 5600x, tofauti ya hizi models ni base frequency ya 200Mhz kwa gharama ya 30$ to 40$, sikuona ulazima wa kulipia 40$ kwa tofauti ya 200Mhz hivyo nikaenda na 5600 na si 5600X, kitu kingine muhimu cha kuzingatia ni kwamba hizi CPU mbili 5600 na 5600X hazina intergrated GPU, hivyo unalazimika kuwa na graphics card unapoamua kuunda PC kwa kutumia kati ya hizi cpu mbili, katika series ya 5600 kuna moja yenye Intergrated GPU ambayo ni 5600G ila yenye specs zake zipo chini kidogo ukilinganisha na 5600 na 5600X, kwa taarifa zaidi unaweza google.

Bei ya hii CPU mpaka kunifikia mkononi ni 370,000/=Tsh
Mahali nimenunua Aliexpress

2. Motherboard- GIGABYTE B550M AORUS ELITE

View attachment 2435808

  • Supports AMD Ryzen™ 5000 Series/ Ryzen™ 5000 G-Series/ Ryzen™ 4000 G-Series and Ryzen™ 3000 Series Processors
  • Dual Channel ECC/ Non-ECC Unbuffered DDR4, 4 DIMMs
  • 5+3 Phases Pure Digital VRM Solution with Low RDS(on) MOSFETs
  • Ultra Durable™ PCIe 4.0 Ready x16 Slot
  • Dual Ultra-Fast NVMe PCIe 4.0/3.0 M.2 Connectors
  • High Quality Audio Capacitors and Audio Noise Guard for Ultimate Audio Quality
  • Realtek GbE LAN with Bandwidth Management
  • Rear HDMI & DVI Support
  • RGB FUSION 2.0 Supports Addressable LED & RGB LED Strips
  • Smart Fan 5 Features Multiple Temperature Sensors , Hybrid Fan Headers with FAN STOP
  • Q-Flash Plus Update BIOS without Installing the CPU, Memory and Graphics Card
  • Anti-Sulfur Resistors Design

Kwenye MOBO nimeamua kwenda na GIGABYTE kwa uzoefu nimeshatumia board zao sijapata changamoto yoyote hivyo nimeamua kuwatumia tena, key specs zipo hapo juu kwa full specs za board husika unaweza google utaona zote.

Gharama ya hii board mpaka kunifikia mkononi ni 408,000/-Tsh
Mahali nimenunua Aliexpress

3. Power Supply (PSU) - Thermaltake BT 600W Full Modular Bronze psu

View attachment 2435826

Model PS-BTM-0600FNFABC-1
Watts: 600W
RGB fan: No
Maximum output wattage 600W
Colour: Black
Size: width said height said length 150mm(W) x 86mm(H) x 140mm(D)
PFC (Power Factor Correction) Active PFC
PG signal :100-500 msec
Shutdown hold time > 16msec at 70% of full load
Input frequency: 50Hz-60Hz
Input voltage: 100V – 240V~
Operating temperature: 5°C to + 40°C
Operating humidity :20% to 85%, non-condensing
Storage humidity: 10% to 95%, non-condensing
Storage temperature: -40°C to + 55°C
cooling system :12cm Hydraulic bearing fan
effectiveness: Meet 80 PLUS®Bronze at 115Vac input.
Mean time between failures 100,000 hrs minimum
Safety certification CE/CB/TUV/ UL/ FCC/ BSMI
PCI-E 6+2pin 2

Kwa upande wa PSU nimeamua kuchagua thermaltake BT600W full modular, ni power supply nzuri ina reputation kubwa hivyo ni brand inayoaminika na bei zao sio za kutisha, pia ni 80+, hivyo utumiaji wake wa kiwango cha umeme ni mzuri kwa maana ya ufanisi, kwa 600W inatosha kabisa kwa mahitaji yangu, ni muhimu kuchagua PSU kulingana expected load capacity ya components zako, kwangu mimi hii inatosha kabisa.

Gharama ya PSU mpaka kunifikia mkononi ni 290,000/-Tshs
Mahali nimenunua Alibaba

4. Computer Case- MSI PAG SHIELD 100L

View attachment 2435897

Last build nilifanya wengi hawakupendezwa na chaguo la case niliyotumia, hata ilipofika wakati wa kuiuza changamoto kubwa ilikuwa case niliyotumia ilionekana ni ya kawaida sana kwasababu haikua na fancy case, nilitumia Case ya hp 7600 kama sikosei, hivyo ilipunguza thamani kiasi fulani japo uwezo wake wa ndani ulikuwa ni mkubwa ila iliangushwa kwa muonekano wake.

Kwasasa nimeamua kutafuta case nzuri yenye mvuto na mwonekano wa kuvutia hivyo basi yeyote atakaeiona anaweza kuvutiwa kwa nje kabla hata kujua yaliyomo ndani, case hii ni MSI PAG SHIELD ina nafsi ya kutosha, kwa components zote muhimu na vents za kutosha kwa ajili ya cooling iwe water cooling au air cooling.

Gharama ya hii case mpaka kunifikia mkononi ni 280,000/-Tsh
Mahali nimenunua Alibaba

5. RAM-Corsair vengeance LPX (2*8GB)

View attachment 2435898

RAM nimechukua hizi corsair Corsair vengeance LPX DDR4 16GB 3200Mhz, zitatosha kwa matumizi yangu japo nilitaka 32GB ila bajeti yangu sikutaka kuzidi kiwango nilicholipia kwa hizi memory stick.

Gharama nilizotumia ni 270,000/-Tshs
Mahali nimenunua Alibaba

6. Cpu Cooler-PA 120 SE TWIN TOWER COOLING

View attachment 2435905

Cooler nimeachagua hii iko na ratings nzuri nadhani itanifaa japo ni overkilling kwa hii CPU 😂

Gharama nilizotumia ni 150,000/=Tshs
Mahali niliponunua ni Alibaba

7. SSD- SAMSUNG M.2 SSD 240GB
Ninayo M.2 SSD nitaitumia kama boot drive

8. HDD- seagate 500GB
Hii pia ninayo nitaitumia kwa ajili ya storage

9. GPU (Graphics Card)
Hapa bado sijachukua ila natarijia kuchukua RTX 3060ti au 3070 japo bajeti, yake imechangamka nitaangalia kulingana upepo wa gharma.

Mengine nitaongeza kadri nitakapofikia.
Karibuni kwa mawazo, maswali, ushauri maoni nk.

cc
Chief-Mkwawa
Machine nzuri sana mkuu, hata upgrade path yake nzuri utakaa nayo mda mrefu.

Vitu vyepesi kwanini huchukui USA?
 
Kuna vingine hapo gharama imekua juu, kutokana courrier, mfano RAM hizo fedex kanipiga piga kidogo.

Pia nimefatilia parts nyingi za electronics zinatoka ASIA, changamoto ni tunanunua kwa watu wa kati, leo ukitaka kuuza tuseme motherboard za ASUS au MSI huwezi kupata sehemu yoyote kwa bei nzuri zaidi ya china.
 
Mkuu vitu vya PC china ni Expensive. Kwa Asia Malyasia bei chini, pia Usa bei zipo chini.

Vitu vya bei rahisi China ni ununue kwa kampuni ya Kichina kama Xiaomi ama Huawei.

Mfano hizo ram ni chini ya $60 kwa US, mobo ni $100 etc

Nimecheki Malyasia hio Mobo ni $85
 
Kwenye Ram hapo nikweli hii gharama imekua juu kwasababu ya usafiri,

Kuhusu MOBO sijui ni used unaongelea au mpya,

Ila kwa uzoefu wangu gharama za ku import kutoka US hazina tofauti sana na za huko ASIA, nimewahi kununua Graphics card 2 tofauti kutoka US, na CAMEO 3 plotter gharama za usafiri na kodi ya TRA hazikuleta unafuu kivile, na items zinazotoka hizo region mara zote nilionana na jamaa wa cutoms TRA, vinginevyo labda kama mtu atatumia freight forwarders ambao pia nao wana gharama kiasi fulani.
 
Yes unatumia freight forwarder, Aramex to be specific. $27 kwa kilo moja. Kuna jamaa wa door to door wa $25 ila sijawahi watumia.

Trick hapa ni kununua kwa seller mmoja, mfano Amazon then vinawekwa package moja, kama vitu ni vyepesi unaweza unganisha viwili ama vitatu kwa fee moja ya usafirishaji, Cpu, ram, ssd ni vitu vyepesi sana.
 
Hii ni nzuri kwa mtu anaeamua kununua vyote kwa pamoja, binafsi nimekua nachukua kimoja kimoja, kulingana na mfuko unavyoruhusu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom