Ndugu wadau na mods katika siku za hivi karibuni na kipindi kilichopita wadau mbalimbali humu,wamekuwa wakiuliza sana juu ya vigezo vinavyotumika kurank jf members,majibu yamekuwa yakitolewa,wapo wanaoridhika labda wapo pia wasioridhika.Sio mbaya sisi sote ni wa moja,mie mwenzenu katika kufikiria sana,nimeonelea nipendekeza hivi: Pamoja na mfumo tulionao sasa wa rank za member.junior member,senior member na senior jf expert member nk.tureform mfumo huu au kuuongezea nyama kidogo,kwa vigezo vilivyopo sasa.Ndio kuna wale ambao labda kwa namna moja au nyingine wanaiwezesha jf kifedha na hivyo kuendelea kuwa hewani,hilo halibishiki kwa kuwa kila mtu anafahamu kuhost tovuti hii lazima tulipia tena vijipesa vingi tu.Hawa wenzetu tuwape status maalumu ya heshima labda "kama senior honorary member" au meritocrat member nk,ili mradi tu tuoneshe tunavyoappreciate michango yao na kwamba mtu yeyote akitaka kuingia katika kundi hilo la heshima,basi afuate vigezo hivyo nasi tutampa tuzo hiyo ya kuitwa hivyo.
Pili,kuna wadau wenzetu humu ni wachangiaji wazuri sana,hoja zao huwa zinaconvince sana na kwa kweli huleta maendeleo chanya.Watu hawa pia uanzishwe mfumo wa kuwatambua na kuwapongeza au kuwatunza,na hii ni kwa admins kutafuta utaratibu ambao sisi wanachama kila baada ya kipindi fulani tutapiga kura au kupendekeza mwanachama wau wanachama tunaofikiri wapewe hiyo eshima kwa mchango wao wa kifikra humu ndani,hii yaweza kuwa wakapatikana kwa thread (yaani kutokana na kuchangia sana katika thread fulani au general) kwa wale watakaotokeza mara nyingi basi tunawachangua walau watu 25 wanapewa hadhi fulani, labda "prior member au senior associate member au hata huo usinia expert member" watu kweli waoneshe expertism fulani katika mada husika au mada fulani fulani.
Na kwa wanaobakia mfano junior member,member,senior member hapa uendelee kutumika utaratibu wa kawaida aidha ni wa credit au number of posts mtu alizoziweka ama kuchangia.wadau mtanisaidia zaidi kuboresha hili wazo.
Angalisho.Hata hivyo wale wanaopewa honorarium kwa kwa kuthamini michango yao kifedha hiyo hadhi yao iwe "ceremonial tu" yaani sijui wataalamu wa kiswahili ceremonial kwa kiswahili ni nini?yaani wasiwe na nguvu ya maamuzi kuwazidi wengine,maamuzi mengo yashiriishe wadau na hawa bwana wasidominate mawazo ya wengine.Labda kwa namna moja ama nyingine watu wengi tunaweza kuwaridhisha kwa mtindo huu.Nadhani kuna mtu aliuliza ina maana mimi nikilipa hela let say 10,000 nitatoka kwenye ujunior member hadi senior au expert member? ili kuondoa mkanganyiko kama huu tuweke merit.
Mnaonaje wakuu,hebu tuchangiane mawazo,hili nimelifikiria haraka haraka tu ili kuboresha mfumo,nikalipost hapa kabla halijanitoka.Mnakaribishwa kukosoa,kuboresha au kutoa mwelekeo chanya mwingine.