Dotori, ni wazo zuri sana na lilikuwa kichwani mwangu pia.... umeniwahi kutype tu mkuu.. lol.
Kwa kuongezea tu, hizo medani ziendane na hiyo contribution per month, kwa hivi sasa ni $30 recurring, kitu ambacho wengine hatuna na hatutaweza kumudu, mara moja sawa. Ukitaka ku cancel hiyo subscription itakubidi uingie tena kwenye settings za malipo na mihangaiko mingine na usipoangalia utaishia kupata charges za benki tuu kutokana na account kuwa tupu!!
Mimi nashauri kuwepo na $2, $5, $10, $15 na hiyo $30 kwa wenye kuweza kumudu hizo kwa mwezi. Basi hii michango iendane basi na yale Dotori unayasema; ya tin, copper, silver, gold na platinum.
Nyongeza ni kuwa, rangi za majina labda nazo ziendane basi na contribution. Wale wasiotoa- Nyeusi, wale wa $2- Kijani, $3- Navy blue, $5 - Blue, $10 -Purple, $15 - Brown na $30 - Red.
Ni haya tu kwa sasa, ahsanteni.
SteveD.