Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Tujikumbushe . . . .
Nyerere alikuwa Mwanachama wa TAA
Baada ya TAA kuonekana haina meno ya kutosha, wakaibadilisha TAA kuwa TANU
Akaacha kazi ili kuiimarisha TANU.
I am assuming the messgae is clear!
mkuu,
binafsi sina tatizo na wazo la kuanzisha chama cha siasa.
tatizo langu liko kwenye namna ya kukianzisha, kuchagua viongozi,kukiendesha(vikao,mikutano n.k) huku tukiwa hatufahamiani.Kwa mfano nitawezaje kumchagua Rev.Kishoka wakati simfahamu?Je tukisema kwamba wagombea watume resume zao kwa ajili ya maombi ya uongozi wa chama, tutajuaje kuwa Rev.Kishoka ndiye Simon Petro?(kwamfano, sio jina lake halisi).
Na kwa nature ya shughuli za kisiasa inahitajika chama kiweze kuwepo kwenye uwanja wa mapambano, kutangaza sera na mikakati majukwaani na kwingineko, na watakao kuwa mstari wa mbele ni viongozi, je wale mlioko ugaibuni mtashiriki vipi katika harakati hizo, maana ni muhimu mkawepo live jukwaani kuliko kunadi sera kwenye mtandao kwakuwa ukweli ni kuwa wananchi wanaohitaji kukombolewa wengi hawawezi kukaa mbele ya screen kama sisi hapa.Sina nia ya kumbagua mtu yeyote ila najaribu kuangalia ushiriki wa wote katika kujenga chama imara na kikacholeta matumaini ya kweli kwa wananchi wa Tanzania.
naomba kuwasilisha.