Takwimu zinaonyesha: Fursa sasa ya kuwa na chama makini cha siasa cha upinzani.

Panzi Mchanga

Senior Member
Jul 31, 2015
127
133
Sina upande ila mapenda vyama vinavyoleta changamoto za maendeleo na "kusimama na nchi"

Takwimu zianonyesha wananchi wasiokuwa na mafungamano na chama chochote inaongezeka, karibu 10%. Na uchambuzi wa ndani unaonyesha hawa wanatoka CHADEMA kwa kuwa na 17% (2017) ya wanachi wenye manhusiano nacho (kutoka 32% ya mwaka 2015). Kwa CCM imeongezeka kutoka 58% (2015 hadi 63 %( 2017).

Hawa 10% wanaashirikia kitu muhimu sana-FURSA yaweza kuwepo. Najaribu kutafakari kwa nini fursa wakati huu na watoa fursa ni chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA? (angalia data hapo juu)

Yawezekana hawa wameshindwa kusimama na nchi wakiwa upinzani. Pengine wameshindwa kwa sababu ya sera zao; na kutofuata utaratibu wa chama-kila mmoja anaweza kusema kwa niaba ya chama. Mambo nyeti ya nchi hayajadiliwi au kuna kukosa upeo wakati wa kuyajadili.

Sitapenda kurejea mambo mengi hapa, ila tu nigusie hili la kuawaambia wakenya waliopiga kura upinzani kuwa watakoma

Chama hiki kinawambia wakenya zaidi ya asilimia 44% (six million plus) waliopiga kura kuwa watakoma. Tena wa nchi nyingine. Haya maneno yanasemekana yanatoka kwa watu mashuhuri katika chama. Ni sawa na CCM wawaambie watanzania 39% waliopigia kura mshika bendera ya uraisi kwa jukwaa la UKAWA 2015 watakoma! (napenda kuwa mahususi zaidi kwa kusema hawa ni viongozi ndani ya CHADEMA, na siyo watu wote walioipigia kura kambi ya upinzani-kwa sababu siyo dhambi kufanya hivyo). Nawafahamu watu wengi mashuhuri waliopiga kura upinzani ila wamebadilika sasa. Hii inadhihirisha na approval rating ya CHADEMA ya 17% (from 32% in 2015). Na hawa wanajikusanya kwenye kundi la walioka tamaa-hawataki chama (ingawa kwa CCM imeongezeka kutoka 58% hadi 63%). Kuna kama 10% wamepigwa na butwaa kwa haya mambo yanayoendelea ya kusema wakenya watakoma na mengineyo na kuacha mambo ya msingi ya nchi.

Nawashauri CHADEMA waachane na mambo ya kibinafsi ya watu. Wasimame na nchi. Kwa mfano kuna maonevu mengi tu yatokanayo na utekelezaji wa sheria usiofuata taratibu. Watu wengi wanadhulumiwa; watu wengi hawajui haki zao. Haya mambo yangefanywa bila ya kuwa na mihemko ya kisiasa naimani wananchi wangewaelewa. Mwangalie Kagame mliyemwita dikteta. Kagonga zaidi ya 95% (kura za ndani na diaspora). Kule wanachi wanamwelewa. Shida ni sisi CHADEMA.

Raisi wa awamu ya tano alipokuwa anagombea urasi alikuwa na popularity ya only 5%. Lowasa 26% (kabla ya kuhama). Ila wananchi walimpa kura-walimwelewa. Mapungufu yapo hasa kwa watendaji wake. Wapo watendaji ambao sera za sasa hawazipendi kwa maslahi yao binafsi (au kwa kushawishiwa na wanasiasa au watu chonganishi ndani na nje ya nchi) na kutaka kuwakomoa wananchi. Kwa mfano, hata haya ya wakuu wa mikoa na halmashauri wanavyo futa hati za viwanja haipendezi. Wangekaa wakakubaliana development program timeline inayokuwa monitored kila baada ya mwaka.Kule Geita kuna mwenye shamba amechimbachimba akapata dhahabu (kumbuka ule wimbo wa almasi) kwenye shamba lake. Kijiji kimechachamaa kinataka kumnyanganya kwa kupitia mikono ya wanasiasa!

Kuna mambo mengi ya kuafanya ndani ya nchi badala ya ku-focus kuleta madhara kwa nchi ambao wanaoumia ni wananchi wa kawaida

Natamani kungekuwa na chama siasa cha kuwatetea wachache (minority). Ukiweza kudhihirisha (demostrate) kwa minority kuwa unaweza; majority watejenga uaminifu. Hata matajiri hawakuanza na faida kubwa. Ila sioni kwa CHADEMA ya sasa walioenda kimataifa zaidi kuharibu uhusiano wa nchi na nchi, kuleta uchonganishi wa kidini, kikabila na kutaka nchi inyimwe misaada kana kwamba anaeadhirika ni Raisi.

Afrika mashariki ina wanachama sita (6). Bado sijasikia chama kingine cha upinzani kutoka katika hizi nchi kikiwaambia wakenya mtakoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom