JF Kuwa Chama Tishio Cha Siasa?

Jamiiforums Kugeuzwa Chama?

  • Yawezekana

    Votes: 44 71.0%
  • Haiwezekani

    Votes: 19 30.6%

  • Total voters
    62
  • Poll closed .
Shukrani mtoa wazo.Na wazo linaweza kuzaa wazo kulingana na response ya wadau.Kwa sababu lengo ni kuelimisha na kumkomboa mwananchi hata wa kule mwakaleli,basi sisi kama wamoja ndani ya jf tunachoweza kufanya na bila kuathiri majina yetu tunayoyatumia ,na bila kuathiri maana ya jf kama chombo cha kupashana habari kwa watz wote ulimwenguni,lakini habari hizi hizi halimfikii na kumwelimisha mlengwa ambaye ni mwananchi wa chini na ambaye ni mpiga kura,basi tupanue wigo wa jf bila kubadili maana yake kama chombo cha kuelimisha jamii tuanzishe magazeti,radio na tv ambazo waajiriwa wake watatumia majina yao na cv zao kama wafanyakazi wengine,na sisi kila mmoja kwa nia moja tutoe mchango wetu katika magazeti hayo,redio hiyo na tv hizo kama mwananchi wa kawaida bila kutumia jina la humu jf.Elimu hiyo itamfikia mwananchi kote nchini maana at least radio na magazeti yanafika kila kona ya nchi.Na tukiendelea kutumia majina yetu ya jf tuweze kuzisaidia hizi media tutakazozianzisha kwa msaada wa kifedha ambao tutalipa kwenye account ya media .kama ni Rev kishoka kalipa ,atabaki kujulikana kama Rev kishoka na msaada wake utazifia media hizo.
Lakini kuwa na chama cha siasa na kuchagua viongozi humu humu wengine hawako tz!na ni nani atakuwa tayari kuexpose jina lake halisi?
 
Mimi nadhani tufanye uhamasishaji humuhumu JF na kwenye vyombo vingine vya habari.Tuelimishe jamii kama ambavyo imekuwa ikifanyika,JF imefanya mengi kuhusu EPA,Richmond,Rada,Kiwira,Alex Stewart na wizi mwingine uliotokea.Utitiri wa vyama sio sababu bali kuielimisha jamii hasa ya vijijini ili wajue haki zao na jinsi ya kulinda rasilimali za Nchi yao.
 
Ngoja na mimi niweke tofali langu,
JF kwa uzoefu wangu wa SIASA, naomba tuiache hivyo ilivyo. Kama itabadilika basi ni kuwa iwe na TV, Radio, Magazeti, nk. Hatari ya kukigeuza hiki chombo ni hii kwamba, SIASA ni siasa. Hata mie ukinichagua tuseme niwe RAIS wa Tanzania, kesho hamtaamini kuwa ni mimi. Ntafanya hivyo kwa kulazimishwa na au kuvimbiwa madaraka. Ilikuwa hivyo, ipo na itaendelea kuwepo. Ila ukweli ni kuwa ni wazo zuri sana. Nikiwa nchi za watu, kulikuja kutokea wakati CHAMA CHA WAFANYAKAZI na ni maarufu sana duniani, kiliamua kuongeza nguvu (ambition za kiongozi wao kuwa Rais) na wakaamua kuingia kwenye SIASA. Kweli walienda hadi wakachukua nchi. Ulianza ugomvi mkubwa sana na chama kile kikafa. Yule jamaa ikaja kuwekwa wazi deal alizokuwa akifanya wakati huo hadi unasikia kichefuchefu. Ila ndiyo siasa.
Mie ningependelea kama ni kuanzisha chama basi JF iwe na mtoto wake pembeni. Huyu mtoto awe na watu wanaojulikana kwa majina na picha zao. Huko tuanze kuandika katiba, miiko ya viongozi, mambo gani ya kushughulikia, hukumu kwa viongozi wasiotimiza ahadi zao, hukumu kwa viongozi wazembe na ambao hawaendi saidia/kuona matatizo ya wananchi wao. Matumizi ya mali za uma na ufujaji wake. Mipaka ya madaraka kuanzia Rais hadi watendaji wa chini. Nasema hivyo kwa sababu, kila nchi ambayo mtu anaongoza bila mpaka inakuwa ni rahisi sana kuwa Dikteta. Hizi control za usalama wa Taifa, Constitutional Court (Mahakama ya katiba) nk ni muhimu sana kulinda madudu kama haya ya leo kutokea. Kuna katiba ambazo hii mahakama kama ingelikuwepo ingelilazimisha bunge kuzibadili. Ila leo CCM wanahonga wabunge wao na wao wanazibwa mdomo na ma VX. Kama kila kitu kitaandikwa na kuweka masharti magumu kwa viongozi wa hicho chama mara wakiingia madarakani, nafikiri wengi tutakuwa tayari kupunguza mlo wetu ili hiki chama kifanye mabadiliko ya NGUVU ya katiba na kurudisha Azimio la Arusha?/Miiko ya viongozi. Upupu unaofanywa wakati mwingine hii Mahakama ingelisaidia maana ingelitosha sisi JF tunaenda kuishtaki serikali.
Mahakama ya katiba iundwe na Mahakimu waliobobea na hata Maprofesa kama Shivji nk. Hawa wawe wanadumu kwa miaka tuseme 8, na hawawezi kuondolowa madarakani. Wao wenyewe wanachagua Boss wao. Hii itasaidia Rais wa Tz au chama tawala asiwe na nguvu ya kuwaondoa na hivyo kuwatisha. Hii ifanyike kwa Usalama wa Taifa ambao wao nao wawe na bajeti moja na JWTZ ambayo itakuwa ya SIRI. UWT usiwe na kupepelza watu tu ila hata maswala ya uchumi wa nchi. Mashirika mengi yanakufa ili kupisha ubinafsishaji wa bei chee. Hivi badarini kweli ni sehemu inayoweza kuwa inaleta hasara? Ila utashangaa Tanzania inaleta na hivyo wameamua kubinafsisha kwa TICT sijui? Huu ni uhujumu wa uchumi wa nchi na ni kazi ya UWT kudeal na hizi deal zote. Mikata ya Madini na kusamehe mikopo, wizi wa BoT, ununuzi wa RADAR na ndege mbovu, UWT mko wapi?
Samahani mie si mwana Siasa mzuri, ni fundi mchundo. Mnisamehe mpangilio mzuri ila nategemea nimeeleweka kwa hayo machache yaliyoshindiliwa kama MP3. Hayana tu picha, yangelikuwa MP4.
 
Kwani vipi? Mi naona watu wanaendelea kuchangia kama vile hili si swali.

Mwanzisha thread kauliza ingawa kwa mtindo wa kutoa maoni, au ndiye Mwenyekiti wa Chama tarajiwa?
 
Thanks.

Did he also said tunahitaji uongozi Bora? Na unafikiri Chama cha Siasa kazi yake si Kushika uongozi wa nchi?

Suprisingly he also said Kiongozi Bora atatoka CCM . . .

hapo nilipohigghlight ndipo tatizo linapoanzia na ndipo litakapoanzia kwa jamii Forum Political party. kama motive itakuwa ni KUSHIKA UONGOZI, sidhani kama watakaofanikiwa kushka uongozi watawakumbuka wanaotakiwa kuwatumikia. Hivi unajua kuwa kinachotusumbua sasa hivi ni kukosekana kwa uongozi bora, na si chama bora?
tatizo kubwa ni kuwa wanaowania kuongoza hawajui kwua wanachokitaka ni kutawala. Sijaona ni jinsi gani sisi humu JF tunaweza kutoka nje ya box hilo.

Brother (or whoever you are) usidanganyike na maneno mazuri humu, who are contributing here are just human beings, not alliens like you lol
 
Allien,

Shukrani kwa wazo lako hili. Nikuangalize vitu vichache tu:

a. Kama wazo lako liko makini kama linavyosikika basi mpango huo wa kuanzisha chama cha siasa uwe nje ya JF. JF ni lazima iendelee kuwa na kubakia jukwaa huru. Siku JF ikigeuka kuwa chama cha kisiasa siku hiyo hiyo itakoma kuwa JF! Ina maana JF nyingine itahitajika.

b. Kupanga kitu kizito kama Chama cha Kisiasa ambacho kinaweza kuchukua uongozi wa kijiji au Taifa unaweza kuanzia JF lakini usiwe na kuungamanika na JF. Kwa maana ya kwamba usitegemee jamii ya wana JF ambao ni watu tofauti sana katika mitazamo, malengo, na mwitikio wao kuhusu masuala ya nchi.

Siyo wote wanataka au kukusudia kuiondoa CCM madarakani hata ukiwaona wanaikosoa humu. Kama ulivyosema hapo juu kuwa "kwenye msafara wa mamba hata kenge wapo".. miye niongeze hata "mijusi nayo imo!"


c. Swali la tatu ni kwanini iwe Chama cha Siasa? Binafsi mwaka huu naenda hatua ya tatu mbele kwa mujibu wa harakati nilizojipangia mwenyewe kuelekea 2010. Na hatua hiyo haihusishi chama cha siasa lakini kitu ambacho naamini kitakuwa na nguvu zaidi ya kuleta mabadiliko. Ninaamini (kama mtu alivyodokezea hapo juu na kuungwa mkono na Suki) siyo lazima kuwa Chama cha Siasa kuweza kuleta mabadiliko tuyakayo.

d. Katika muda wote ambao nimekuwa mshiriki wa fora mbalimbali nimegundua kitu kimoja, don't count on people. If you think you are called to do something, go and do it! Watu wengine watafuata, wengine watakuangalia waone ukishindwa wakucheke, wengine watasubiri ufanikiwe wajiunge nao, na wengine watakushangaa kwanini umeanzisha kitu fulani!

So, kama unafikiri unataka kuanzisha chama cha siasa; go and do it! Kama unataka ushirika wa watu wachache, wasiliana nao pembeni, toa mwaliko, badilishaneni mawazo n.k!

e. Kama ningekuwa mtu wa kufikiria kuanzisha chama cha siasa; chama hicho naamini kingekuwa tofauti sana. Tofauti kiasi kwamba:

- Kitasababisha vyama vya upinzani vilivyopo viwe obsolete
- Kitakuwa tishio la kweli la CCM
- Kitasimama peke yake kama upinzani halisi
- Kitakuwa tayari kushika madaraka kwani wanachama wake watakuwa ni watu ambao Taifa linaweza kuamini kuiongoza nchi.
- Na kitajenga na kuundwa katika misingi iliyoliunda Taifa hili. Chama kitakachorudi kwenye misingi ya Taifa letu.

n.k n.k

Bahati mbaya, mimi si mwanasiasa so, uwezekano huo haupo kwa sasa.
 
Hapana. JF kuwa Chama cha Siasa ni kupoteza mwelekeo. Na kwa mawazo yangu, sidhani kama njia ya kumkomboa mwananchi ni kupitia Chama cha Siasa. Maendeleo hayawezi kuletwa na wanasiasa. Kwa nchi zetu za kiafrika, wanasiasa ni wapinzani wakubwa wa maendeleo. They are naturally selfish and JF political party won't be an exception. Maendeleo yataletwa na wananchi wenyewe. All they need is education and right information. Information is power. Wananchi ambao wako "informed" sawasawa, hawawezi kumchagua kiongozi asiyefaa. Hawawezi kudanganyika kirahisi. Serikali haiwezi kufanya maamuzi ambayo hawayataki. Itakuwa ni vigumu kwa viongozi kula rushwa. Kumbuka ni wananchi haohao ndio huwezesha njama za viongozi kula rushwa (accountants, bankers, drivers, e.t.c). Tunahitaji pia kuwa wazalendo (We lack patriotism).

It's far possible for informed citizens to monitor their government (e.g. EU, Japan, US, e.t.c.). Ni dhahiri kuwa, serikali tulizonazo Afrika ni mbovu kwa sababu ya uwezo mdogo wa wapiga kura; uwezo mdogo (ignorance) wa wanaongozwa. So, JF inaweza kufanya kazi kubwa sana ya kuelimisha wananchi na kuwapatia habari sahihi kwa wakati. Ikumbukwe kuwa, idadi kubwa ya wananchi wanaishi vijijini. Huwezi kunishawishi kuwa JF inawafikia wananchi wa vijijini (Rufiji, Kilwa, Makongorosi, Kwa Mpiga Miti, Sanya Juu, Igunga, Makunduchi, Mwembe Mchomeke e.t.c.) So, safari bado ni ndefu. Kwa kupitia Radio, TV na Magazeti, "impact" itakuwa kubwa zaidi. The thinking that we can do more through politics, by itself, is an indication that we have a long way to go. Ni mawazo tu!
 
Suki, hakuna mafumbo hapa. Fafanua!

Fumbo,mfumbie mjinga....no?
Sidhani hata kidogo,mabadiliko ya kijamii tunayoyatarajia yataletwa na siasa au philistine political leaders we currently have for that matter.Kwa mtazamo wangu,viongozi na wananchi kwa ujumla,tunapoteza muda mwingi kwenye mijadala ya kisiasa-creating a ''poliwood'' of our own while possible reforms still in dreamland.

Back to JF as a political vessel.
Like you said,kwenye msafara wa mamba kenge wamo:To a massively undeniable extent,JF is so far,being portrayed as a pastime for bored,political savvy individuals and knowledgeable,angry religious beings.And although steamy debates between members may signal ubivu wa maarifa among JF political racounters,it is not necessarily an indication of the political stance of the forum as a whole.
 
Last edited:
Mkuu X-Paster;

Sijakuelewa . . . . Unaweza kufafanua usemi wako?

Pole mkuu Allien kwa kukukwaza... I hope ukisoma kuanzia Post #4 mpaka Post #72 Utakuwa ushapata jibu nilikuwa nina maanisha nini...!

Waswahili wanasema Jitihada Haishindi Kudra...!

Kwa kunakiri msemo wako..." kwenye msafara wa Mamba na Kenge wapo... na Mkjj akaongeza na Mijusi wamo..." Nami nakuongezea... Vinyonga nao watakuwemo kwenye msafara...!

Nasisitiza tena.."JF kuna Udini... Hatutakaa tukaelewana..."

Kila la kheri Bro.
 
Jambo la kwanza kufanya ili JF iwe Chama cha Siasa ni Members kuacha kuwa "anonymous". Chama cha siasa ni chama cha watu jasiri. Sio lazima waseme mambo sahihi kila siku. Wawe tayari kukosolewa na kujisahihisha.
JF mkiwa mafichoni kwa kutotaja majina yenu halisi haitawezekana kuunda chama hata cha "civil"!
 
Wakulu;

So far wengi wanaunga mkono wazo hili ingawa kwa mitazamo tofauti. Mhtasari wa Hoja nyingi zilizotolewa ni kama ifuatavyo:

- Kwamba kuna wana JF ambao tayari ni wanachama wa vyama vya siasa

- Kwamba JF tayari inafanya kazi nzuri as a "Watch Dog" ya maovu yote yanayoifanyika nchini

- Kwamba JF iendelee na role yake ya sasa na inaweza kupanua wigo kwa kuanzisha TV, Radio, Magazeti nk.

- Kwamba kwa wale wanaoona kuwa vyama vya sasa na viongozi wao wanapwaya wanafikiri Chama makini Mbadala kinatakiwa kiundwe

- Kuna wanaotaka kuwa tuangalie ni chama gani kilicho serious na kikubali kujiunda upya na kuwachukua wana JF wazuri ambao watataka kuleta mabadiliko ya kweli na wajiunge huko.

- Kuna wanaoona kuwa Chama Kipya Kianzishwe ambacho kitafanya vyama vingine vionekane kama vile havina upinzani wowote wa maana na kuleta maendeleo

- Kwamba Malengo ya Chama hicho yawe ni ya kweli katika vitendo na kilete mabadiliko ya kweli na kukidhi haja za Watanzania

- Kwamba kuna ambao wako tayari kuanza kuyafanyia kazi mawazo haya lakini katika namna ambayo italeta mshikamano badala ya mfarakano.

- Pia kuna wengine ambao wako against mawazo haya na wanaona ni kukosa mwelekeo, ndoto za alinacha na kupoteza muda

- na mengine mengi . . .

Mpaka sasa, Wakulu wafuatao wako tayari kufanyia kazi mawazo haya katika mtazamo chanya:

1. Allien
2. Siao
3. Waberoya
4. BM21
5. Mlalahoi
6. Recta
7. Rodelite
8. Gembe
9. Susuviri
10. Mwita Maranya
11. Calnde
12. Kamuzu
13. MwakyJ
14. Baba Lao
15. Mwamaroroi
16. Sikonge

Kumekucha . . . . . Tuendelee kusemezana Wakulu tutafika tu . . .

Meanwhile, tunaomba wale Wanachama wenye vyama vyao vya siasa, kama wanahoja za kutushawishi tujiunge nao kwa mantiki ya michango iliyotolewa humu na kujisafisha na kujiunda upya . . . basi watoe hoja zao . . . .

Vinginevyo tukifika Idadi ya 200, basi tutaanza mikakati ya vitendo ya nini cha kufanya maana utakuwa ni mtaji tosha wa kuanzisha chama Serious.

Mimi si Mwanasiasa lakini napenda kuona wazo hili linafanya kazi na kuona Uongozi makini unachaguliwa.
 
- Haya sasa wakuu turudi back to the real ishus maana taifa liko njia panda, vijana wetu wamepasi hawana sekondari za kwenda form one, that is wasup! I mean mpaka leo bado sijaamini!
 
Kweli nimeamini Tanzania kila mtu anataka kukimbilia kwenye siasa...hivi kuna nini uko kwenye siasa?
 
- Haya sasa wakuu turudi back to the real ishus maana taifa liko njia panda, vijana wetu wamepasi hawana sekondari za kwenda form one, that is wasup! I mean mpaka leo bado sijaamini!

Du! Kweli wewe ni FMES . . . .

Si ungeanzisha tu Thread yake Mkuu?

Sasa hujaamini nini wakati Serikali inasema imejenga Sekondari kila kata? Kama ulipata nafasi ya Kumsikia Rais wa Msumbiji wakati wa Sullivan Summit akieongelea nini wanafanya . . . . We need to learn from them . . .

Wewe unashangaa matatizo ya Sekondari . . . Ajira je? Afya? nk Na unafikiri solution yake ni nini?

Tuyaache hayo, una maoni gani kuhusu mada ya Thread hii?
 
Kweli nimeamini Tanzania kila mtu anataka kukimbilia kwenye siasa...hivi kuna nini uko kwenye siasa?

LOL . . . Unanikumbusha ya Mwalimu . . . Kuna biashara gani pale Ikulu?

Mkulu, Wanasiasa wa kweli hawana wanalotafuta bali ni Uchungu tu wa kuwaletea watu wao na nchi maendeleo. Je kwa sasa ni Wanasiasa wangapi wa namna hiyo? Unawafahamu?
 
Nina pledge dollar 1000, za kuchapishia katiba na ilani ya uchaguzi watakazoandaa MKJJ na Rev.Kishoka.

Kama hayo machapisho yataandikwa kwa lugha za Kiswahili, Pundit na Nyani Ngabu tunawaomba msaidiane na waandishi ili ziende kwenye lugha ya dunia, I mean kiinglish!

Shy, Yo-yo, Yeboyebo, tunaomba nembo ya chama hiki.

Jmushi, Invisible, Maxcence na FMES, tunaomba muwe idara ya intelijinsia, hakikisheni katika member wa JF; EL, RA, BWM, Chenge,n.k hawaexist, la kama wamo wakubali tuwatume kazi yeyote! hasa za usafi wa ofisi yetu ambayo makao yake makuu yako Kigoma mjini! BMW atakuwa akishusha na kupandisha bendera ya chama kila siku asubuhi na jioni!

Nziku , Mkandara na MIMI waweka hazina
Kwanza tuanze kuunda kamati .......

Please propose jamani watu wengi sana humu na kila mtu anafaa!

waberoya

Wasi wasi wangu unaanzia hapoooo
 
LOL . . . Unanikumbusha ya Mwalimu . . . Kuna biashara gani pale Ikulu?

Mkulu, Wanasiasa wa kweli hawana wanalotafuta bali ni Uchungu tu wa kuwaletea watu wao na nchi maendeleo. Je kwa sasa ni Wanasiasa wangapi wa namna hiyo? Unawafahamu?

Kumbe wakuu pia mna kauchu ka madaraka; mnataka siasa pia; kuwasaidia watu wa TZ mpaka muanzishe chama cha siasa? hamuwezi kuwasaidia waTZ mkiwa nje ya siasa mkawa na mission zingine kama ilivyo JF kwa sasa (ingawa naona mnataka kuihamisha kwenye ajenda ya msingi) na chanzo chake tutakijua si muda; sidhani kama ni swala la kuunga mkono; vyama tayari vipo; vinahitaji kupewa mawazo au kuendelezwa ili kukdhi haja ambayo hata nyie mtaanzisha chama mtaenda kukuta otherwise mtu mwenye malengo ya kuanzisha chama anaweza kuanza kijiwe chake fresh aendelee lakini sidhani kama ni sahihi kutumia mgongo wa JF. Yangu ndio hayo; hamjanishawishi
 
Kumbe wakuu pia mna kauchu ka madaraka; mnataka siasa pia; kuwasaidia watu wa TZ mpaka muanzishe chama cha siasa? hamuwezi kuwasaidia waTZ mkiwa nje ya siasa mkawa na mission zingine kama ilivyo JF kwa sasa (ingawa naona mnataka kuihamisha kwenye ajenda ya msingi) na chanzo chake tutakijua si muda; sidhani kama ni swala la kuunga mkono; vyama tayari vipo; vinahitaji kupewa mawazo au kuendelezwa ili kukdhi haja ambayo hata nyie mtaanzisha chama mtaenda kukuta otherwise mtu mwenye malengo ya kuanzisha chama anaweza kuanza kijiwe chake fresh aendelee lakini sidhani kama ni sahihi kutumia mgongo wa JF. Yangu ndio hayo; hamjanishawishi

Ni kweli kabisa mkuu. Kama watu wanadhani chama cha siasa ndicho chenye siri ya ukomboziw a watanzania, vipo vingi tu, ni suala la kuchagua kipi kitumike, na si kuwa na wazo la kuanzisha kipya. Mnaweza kuchagua hata 'kilichokufakufa' na kukigeuza kuelekea malengo mnayoyataka.
Lakini linapozungumziwa suala la vyama vya siasa, ni lazima tufanye reference kwa hivi vilivyopo na hapo ndipo mashaka yanapoibuka wka sababu vilivyopo havijafanya vile vinavyoeleza kwenye katiba na ilani zao. Sijui hicho kipya kitawezaje kujipambanua tofauti ha hali iliyopo sasa.
Pia, vyama vya siasa vimeshajibainisha kuwa ni suala la ualaji zaidi kuliko kutetea maslahi ya watanzania, kuanzia chama tawala mpaka vya upizani. Kwa nini tunalenga kuwaumiza zaidiw atanzania kwa jina la kuwakomboa?
 
Upinzani wa kweli utatokea ndani ya chama tawala na wala si kuwa na vyama vingi kama utitili hapa Tanzania. Ama ni bora kujiunga na vyama vilivyopo then kuviimarisha pale mnapoona pana kasoro.

KWANINI UINGIA GHARAMA ZA KUANZA KUJENGA MSINGI WA NYUMBA WAKATI MSINGI ULISHAJENGWA, KAZI SASA NI KUPANDISHA NYUMBA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom