JF imefunguliwa(?) Naipata bila VPN

JF imefunguliwa(?) Naipata bila VPN

Haijafunguliwa, nadhani wamejisahau tu. Baada ya muda mfupi lazima utumie VPN tena kuingia.

Matusi humu ni machache, kisichotakiwa na serekali ni ukweli.

Jukwaa hili halikufungwa kwa sababu ya matusi, bali ni kwa kuongea ukweli usioipendeza Serikali.
 
Sijajua kama wamefungua na sitoi mguu kwenye accelerator
1771783249954.png


Waliokuwa wanashindwa ku access JF kipindi imefungiwa nawaona masnitch au watu primitive wasiojua wapo katika kizazi gani.
 
Haijafunguliwa, nadhani wamejisahau tu. Baada ya muda mfupi lazima utumie VPN tena kuingia. Matusi humu ni machache, kisichotakiwa na serekali ni ukweli. Jukwaa hili halikufingwa kwa sababu ya matusi, bali ni kwa kuongea ukweli usioipendeza serekali.

Matusi yapo. Na ukweli upo.
Kusema matusi hayapo ni kuongea uongo.

Kuhusu sababu za kufungiwa unaweza kuwa sahihi
 
Hamjambo wote!

1. Turudi kwenye majukwaa, vilinge na vijiwe vyetu.

2. Matusi tupunguze maana kuacha kabisa kuna watu najua hawataweza.

3. Uzushi, bullying, kejeli, kuvuana nguo tuache.

4. Ukosoaji uendelee sambamba na suluhu kwa Kila ukosoaji.
Haina maana kukosoa bila kutoa suluhu kwa kile unachokosoa.

5. Kupongeza kusizidi hasa kwa kile kikosi kazi cha uchawa. Kwa sababu uchawa ukizidi wengine uvumilivu huwa Mdogo hujikuta wanatukana.

6. Mada za elimu, kuonya, burudani, kupiga soga, kuchombeza, fursa, n.k. ziendelee.

7. Tuwape Uhuru vijana wetu wadogo wale wenyw umri wa kujadili ngono, uchakataji, mapenzi kufanya hivyo bila kuwa kejeli kwani huo ni umri wao.
Lakini pia wapo watu wazima wachache ambao kwao hiyo ni starehe na hobby.

8. Mabishano na uchokozi wa hapa na pale ni muhimu kuchangamsha kijiwe lakini usizidi.
Sisi wengine hatuwezi ishi sehemu tulivu bila kuona hekaheka, uchokozi,

9. Mada tata zianzishwe, zile ambazo wengine hasa watu wengi huogopa kujadili. Ndio maana ya kutumia anonymous.

10. Spana ziendelee kama kawaida bila kumuangalia mtu usoni. Dadeki!

11. Kumekucha

Kazi ianze.
Ingekuwa imerudi bila VPN ingekuwa na matangazo boss.
 
JF haikufungiwa sababu ya matusi , bali kuanika ufisadi katika mgodi wa makaa ya mawe , tuweke rekodi sawa.

Matusi yapo kila mahali, huwezi zuia matusi mahali penye mikusanyiko maana tunakutana watu wa aina tofauti, kuanzia makuzi hata exposure.
 
Back
Top Bottom