JF challenge ya "NO REFORMS, NO ELECTION": Target replies 3K

JF challenge ya "NO REFORMS, NO ELECTION": Target replies 3K

Wewe Msigwa tangu lini ku-comment #NoReformsNoElection imekuwa jinai? Tupe kifungu cha sheria kinachounga mkono, otherwise ni porojo tu. Nyie si mmetafuta wasanii wa ku-comment “Oktoba mnatikiana” ili kuzima #NoReformsNoElection. Sasa mbona sisi hatujasema nyie mnaotikiana tutawatafuta? Si kila mtu afanye anachokiamini, mnaotikiana muendelee kuimba tiki zenu na tunaosema #NoReformsNoElection tuendelee na msimamo wetu. Au pamoja na kutumia wasanii kampeni yenu imefeli ndo mnaamua kutoa vitisho?

Wananchi hatuko tayari kushiriki uchaguzi ambao utaacha ndugu zetu vilema na wengine wafariki. Hivi wewe Msigwa, yule Aquilina aliyepigwa risasi wakati wa uchaguzi mdogo wa Kinondoni angekuwa mwanao ungethubutu kutoa hivi vitisho? Au kwa sababu wanao wanaishi vizuri, hufikirii watoto wa wengine? Hivi unajua Aquilina alikuwa mtoto wa pekee kwa mama yake? Sasa hebu fikiria ingekuwa wewe umepoteza mtoto wako wa pekee kwa sababu ya uchaguzi ungejisikiaje?

Watu wanaposema hawatashiriki uchaguzi bila mabadiliko, wamebeba maumivu mengi moyoni. Heshimuni hisia zao, si kuwatisha. Mkiwa kwenye hizo ofisi za umma huwa mnajisahau sana, lakini amin amin nakuambia Mungu yupo. Damu za watu walioumizwa, waliopotezwa na waliouawa kwa ajili ya uchaguzi zinaweza kugeuka laana kwako na vizazi vyako.

Chunga sana kauli zako ili kulinda vizazi vyako, maana Mungu mwenyewe amesema atapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha 3 na cha 4 (Kutoka 20:5). Kwa hiyo chunga sana kauli zako ili Mungu akianza kujibu, wajukuu zako wasije kujutia kuwa na babu wa aina yako. Sisi msimamo wetu ni uleule #NoReformsNoElection
Credit: Malisa GJ
FB_IMG_1749661970346.jpg
 
Uchaguzi hata wakienda watu wawili utafanyika tu. Ikiwa muendesha gurudumu yupo ndani, nini kimebaki tena
 
Back
Top Bottom