JF challenge ya "NO REFORMS, NO ELECTION": Target replies 3K

JF challenge ya "NO REFORMS, NO ELECTION": Target replies 3K

T-Shirts, Baseball caps, Key holders, Openers, Miavuli yenye nembo ya NRNE itengenezwe iuzwe wakati wote wa kampeni hii ikienda sambamba na kuandikisha wanachama wapya. Kitengezwe kitengo cha marketing haraka sana.... 🙏
Kaka niko tayari kulipia tshrt na kofia hata kesho.. nivae nikapost X ....
 
Demand ya mabadiliko ni kubwa mno, tuendako usishangae kuona polisi baadhi wakivua magwanda.... Ukisikia CCM BYE BYE ndio sasa.
Mafanikio yoyote yalipitia magumu...
Mjiandae kwa lolote coz wenye mamlaka huwa ni wagunu hawawezi kukubari kirahisi mpk nguvu kubwa itumike msikate tamaa nawaombea daily...


Msiniangusheee. Naungana nanyi soon..


Najua Kuna watu watasema tumenunuliwa Mara tunalipwaaa.... hayo maneno ya kawaida..
Ila mimi nikiwa kama mtanganyika mpenda maendeleo napambania mabadiliko kwa ajil ya kesho Ya watoto wangu hata me nisipokuepo... sitaki wao wapitie mateso tuliopitia sisi....
Mimi sio Chadema wala CCM ila mabadiliko yamenigusa kama mwananchi mwenye akili timamu..

Serikali inajitahidi kufanya mengi na mengine tunayaona ..... tunawapongezaaa ila mabadiriko lazima ili serikali yetu izidi kufanya vizuri..
Siamini kama CDM au CCM wakiwa madarakani basi nikiamka asubuhi nitakuta kiroba cha Unga mlangoni,HAPANA.
Natakiwa nipambane kwa ajili ya familia yangu kila jua linapokuchwa ndipo niweze kufanikiwa...

Lakini mabadiriko ni muhimu kwa Tanzania yetu ya Kesho.
 
#k
1749494204073.jpg

Baadhi ya watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania wameelezea kukerwa na maoni ya wafuasi wa kampeni ya “No Reform, No Election” yanayoachwa kwenye machapisho yao binafsi.

Miongoni mwao ni Wema Sepetu — Miss Tanzania 2006, msanii wa filamu, na mfuasi wa chama tawala CCM — ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni 11.9 katika mtandao wa Instagram. Kupitia chapisho lake la mwisho wa wiki, Wema aliwataka wafuasi hao kuacha mara moja kuchafua maudhui ya watu kwa maoni ya kisiasa, akisisitiza kuwa kila mmoja ana uhuru wa kuchagua anachokiamini.

Naye mchekeshaji maarufu jukwaani na mitandaoni, Hakika Ruben, ambaye anafuatwa na zaidi ya watu milioni moja kwenye Instagram, ameripotiwa kupoteza wafuasi wapatao elfu 40 katika siku chache zilizopita — hatua ambayo baadhi ya wachambuzi wanaihusisha moja kwa moja na msimamo wake kutounga mkono kampeni hiyo ya kisiasa.

Swali linalozuka sasa ni: Je, watu maarufu wanaoepuka au kupinga kampeni hii wanakabiliwa na adhabu ya kupoteza umaarufu wao, au huu ni upepo wa kisiasa unaopita❓️
 
Back
Top Bottom