Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,893
- 3,200
Hili suala la jeshi kuamriwa kufanya usafi kila vyama vya upinzani vinapotangaza maandamano halikubaliki.
Wote tunalia hali ngumu ya maisha ikiwemo wanajeshi pamoja na familia zao na viongozi wa serikali wako kimya, halafu wanapotakiwa kufanya kitu walau hata kwa shinikizo la maandamano, wanakimbilia Kuomba wanajeshi wetu wakafagie barabara na kuokota makopo! Kweli jamani?!! Hapana. Hii haikubliki kabisa.
Wanajeshi tumikieni maslahi ya nchi na wananchi wake na wala siyo viongozi wa hovyo wanaotusababishia hali ngumu kutokana na matumizi yao ya anasa huku raia tunaumia.
Jitambueni nyinyi ni watu wa muhimu sana kwa nchi na mnapaswa kuheshimiwa na siyo kutumika.