ACT, CHADEMA na wenzenu, Msingi ni maslahi ya nchi siyo ya vyama

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,899
Siasa hubadilika na siku hazigandi. Siyo siri tulipo leo, tunaweza kuwa tuko pema zaidi kiukombozi kuliko wakati mwingine wowote kabla.

Ishukuriwe historia iliyotufikisha hapa pamoja na machungu yake. Kwamba hatimaye leo tunaweza kuyatarajia yaliyo mema zaidi, tena kwa nguvu zetu wenyewe.

Kwamba leo zinasikika sauti za wazi, za kizalendo na tena zenye kudhamiria kweli kweli?

Kwamba bila kujali vyama vyetu, wananchi tusimame sasa kuvinyakua vilivyo vyetu?

Kwamba kuna baadhi ya wenye kutaka kutukwamisha?

Kwamba wengine hao wanaojinasibu hivyo, kuwa ni wenzetu?

Kumbe Mungu atupe nini? Kulikoni ndugu zetu?

1. Wananchi tunataka katiba mpya sasa.
2. Wananchi tunataka ruzuku za vyama zifutwe (vyama viendeshwe na wanachama wao).
3. Wananchi tunataka malipo na marupurupu kwa wote yawe fair (yaani wabunge, mawaziri, raisi, majaji nk, yawe kama ilivyo kwa kada zingine zote kama walimu, wahandisi, matabibu, maprofesa nk).
4. Wananchi tunataka misafara ya viongozi iwe kama ilivyo kwingine kuliko staarabika (siyo hii ya kufuru na kero zao barabarani ).
5. Wananchi tunataka chaguzi za haki, huru na usawa.
6. Wananchi tunataka rasilimali za nchi kuwa kwa maslahi ya umma.
7. Wananchi tunataka kuwajibishwa kwa wezi wote wa mali za umma bila kujali nafasi zao wakati wowote kwa taifa.
8. Wananchi tunapinga ugumu wa maisha wa kutengenezeshwa kutokana na kukosekana uwajibikaji, ubinafsi, wizi, ufisadi, sera mbovu na vya namna hiyo.
9. Nk, nk (tuendelee kuongeza).

Kwani kama haya si ya msingi ninyi wenzetu mnaopinga jitihada kama hizi mnataka nini kumbe?

"Wapewe maua yao wote wanaowapigania au kuwaunganisha wananchi kujipigania."

F7fe5RYWgAA-wlI.jpeg


Kuongole TAL, Mwabukusi, Slaa, Mdude, Maria Sarungi, Ulimwengu na nyote wa namna hiyo. Haipo siri, jitihada zenu ni za kutukuka na historia itakuwapo kuwakumbuka.

Ama kwa hakika mlipo tupo!

Angalizo:

"Wenye kuzipinga jitihada takatifu hizi kwa ubinafsi wao tu, na wajitathmini kabla hawajapwelewa."
 
Back
Top Bottom